Wednesday, December 5, 2012

MCHANA WA LEO NINGEPATA MLO KAMA HUU NINGEFURAHI SANA LAKINI SASA ITANIBIDI NILE KWA MACHO....

Ni ugali kwa mlenda uliochanganywa kwawa majani ya maboga na ambayo bamia. Halafu  bakuli la (ma)tembele la kuchemshwa kwa nyanya na kitunguu. Bila kusahau pilipili shamba.
Hakika hapa ni utamu, na tena ule wa asili kabisa ,yamu yamu yamu....NAWATAKIENI WOTE SIKU /JUMATANO NJEMA SANA.

10 comments:

Interestedtips said...

nikitoka kazini leo inabidi nikapike huu msosi, tena wakati wa kula unakaa chini ili ufaidi.........kudadadeki

emuthree said...

Haya KARIBU TWALA, KAMA CHA MTU CHALIWA!

Yasinta Ngonyani said...

Ester! wewe ndo unajua kweli kutamanisha mtu ...haya na halafu utapokula tumia mkono ndipo utakapoona utamu wake...na halafu usisahau ndimu/limau kwenye tembele ila iwe kwa mbaliiiii!!!!
emu-3! Ungo wangu mafuta yamekwisha yaani sasa hivi ungeniona nimetua..ngoja niulizie kama kuna anayeweza kuniazima:-)

Nicky Mwangoka said...

HUU NDIO UTAMU WA NYUMBANI, NDO MAANA ME NASEMA "KARIBU NYUMBANI"

Yasinta Ngonyani said...

kaka Nicky! hakika wala hujakosea nami nasema AHSANTE nishakaribia.

ray njau said...

Nyumbani eeh,nikukumbuka nyumbani eeh,moyo unaenda mbio eeh,nili nitafika nyumbani eeh?Nyumbani kwetu kwa baba na mama eeh,nyumba kwetu nilikozaliwa eeh!Nyumbani eeh!

Yasinta Ngonyani said...

kaka Ray! inawezekana pia ni sababu ya kutamani nyumbani..na sasa nadhani ule msimu wa mboga mboga kama unabidii ndo zipo nyingiiiii,,, Leo nakubali hata nisipopata samaki maana hapa ni patamu kwelikweli....

Rachel Siwa said...

Duuuhhhh da'Kadala yaani umenitamanishaaaaaaaaaaa!!!!!!

Mija Shija Sayi said...

Ukimaliza hapo lazima utafute kivuli cha mwembe kilipo kwanza...

Interestedtips said...

raha ya hii misosi ule kwa mkono...kwenye tembele lazima kalimao kwa mbaliii...mmmh