Friday, December 14, 2012

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIA KUTOKUWA HEWANI KWA MUDA ..NAKWENDA KULA LIKOLO LA NANYUNGU:-)NYUMBANII NI NYUMBANI!!!

Hali ya hewa ndivyo ilivyo leo  DAKIKI/DAKIKA MBILI ZILIZOPITA...yaani mtu unaonekana mnene kama vile tembo kwa ajili ya kuvaa mingua mingi ili usisikie baridi. Nina furaha kuachana na hali hii kwa muda .. nisemapo hivi ni kwamba BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIA INATAKA KUSEMA HAITAKUWA HEWANI KWA MUDA KUTOKANA NA MAMA WA MAISHA NA MAFANIKIO ATAKUWA SAFARINI. Nachukua nafasi hii kuwatakieni wote CHRTITMAS NJEMA NA PIA MWAKA MPYA NA PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA HAPO MWAKANI 2013.
Labda tu Remmy Ongala afichue wapi nakwenda..... na kipande hiki cha mziki..

Narudi nyumbani eeeeh nakwenda kula likolo la nanyungu....wangoni wote myumwike..nyumbaniiiiiii

25 comments:

Ester Ulaya said...

KILA LA HERI DADA, TUTAKUMISS KWELI

Yasinta Ngonyani said...

Ester usiwe na wasiwasi nakuja huko uliko...nami nitawamiss munooooooooooo!!

Anonymous said...

Usisahau kutuletea senene na mihogo.

Anonymous said...

Karibu dada twakukaribisha lkn hilo dakiki(dakika) umeliandika kingoni kabisa ha ha ha nimefurahi sana kweli jasiri haachi asili!

sam mbogo said...

Haya safirini salama.kulia sikukuu ya noweli nyumbani ni muhimu. hapa unikumbusha misa zao zinavyokuwa ndefu nyumbani,unakuta wakati wa sikukuu inaweza kufika hata ma saa 2-3! lakini inapendeza kila mtu kijijini anakuwa na furaha,mara ya mwisho kula krisimasi nyumbani 2006 kidogo nifunge mtaa! kijijini pombe za kienyeji ni bei poa sana,niliweka namuziki wa kukodi we acha tu ,siku hiyo nilijisikia raha sana,kidogo nipate wazo la kugomea ubunge!??.kaka s

ray njau said...

Dada Yasii kaolewa kurudi nyumbani kuja kutembea!!

NN Mhango said...

Nakutakia msafara mwema. Wasalimie wazazi ndugu na jamaa wambie mwe! huko ulaya barafu mwe!

Emmanuel Turuka said...

nakutakia safari njema wasalimie wote huko na ifurahie likizo yako na sikukuu zote za xmass na mwaka mpya usisahau kupitia likonde na wape Hi wote; inafaa kidogo kuikimbia baridi

John Mwaipopo said...

safari njema na karibu bongo.

Anonymous said...


Aiyaya kuolewa utarudi nyumbani kutembea x2, kwa heri baba yangu kuonana majaliwa
Aiyaya kuolewa utarudi nyumbani kutembea,x2
kwa heri ndugu zangu kuonana majaliwa
Aiyaya kuolewa utarudi nyumbani kutembea x2 da Yasinta!
Haya na tunakukaribuisha nyumbani kutembea kwa mwezi mmoja tu usizidishe na ukiisha urudi huko huko kwa mume wako.

Jamani Dada Yasinta si uniachie hizo nguo zako za baridi kuanzia kichwani kofia mpaka viatu, mana kweli ni baridi hasa mwaka huu!Si utaviweka tu ndani au utasafiri nazo zote? aaahh

SAFARI NJEMA NA MUNGU AKUTANGULIE NA FAMILIA YAKO.

isaackin said...

DA YASINTA USITUKIMBIE BANA,UNAWEZA KUTU-UPDATE HATA UKIWA HUKO lunyungu,usisahau picha za kutosha huko njiani mpaka kijijini na msosi angalau tule kwa macho.wasalimie sana

steven Bulamu said...

nashukuru safari njema----

Rachel siwa Isaac said...

Nenda nenda salama eeehh nakuombe salamaaaaaaa!!!!!!MUNGU awatangulie na wasilimie wooote!!!!

duuhh nakuonea Wivu Xmas na Mwaka mpya huu hatuta wasiliana tena?...........haya nitazima kasimu kangu mwehhh KADALA!!

batamwa said...

karibu sana dada Yasinta lakini joto la hapa dar ni balaaaaa,safari njema ufike salama sio vibaya ukawa unatuapdate ukishafika hapa nyumbani karibu sana

Simba Deo said...

Karibu sana. Itakuwa furaha kukuona nyumbani. Kwa hali hiyo ya baridi huko, naamini uta-apreciate joto la huku. Karibu sana.

Anonymous said...

Aah Dada witila mbepu penapo maana mwe muvii ku North hamsphere nde wakati waki weniu, haya bwana safari yivyaa ya salama katigegelai mangatungu ne mbaka mwezi wa march - Nabambu Mbawala

Anonymous said...

WOW just what I was looking for. Came here by searching for weightloss clinic
My web page > la weight loss

Baraka Chibiriti said...

Safari njema Dada Yangu, ukiwa Bongo nitafute na namba hii: 0767-191275. Karibu sana TZ.

Markus Mpangala said...

Karibu nyumbani. karibu sana

Anonymous said...

Mlongo kila la heri, husisahau kunibebea likolo la nanyungu, na mangatungu. pitiku, na mabuni, mapotopoto......

Ester Ulaya said...

Dada Yasinta anawasalimia sana na kuwamiss sana.......mliotaka mabuni anasema msikonde mtapata

Ester Ulaya said...

Halafu kasema atawajuza karibuni yanayojiri,yupo poa sana, msichoke tu kudhuru humu ndani

Anonymous said...

Hey! This post couldn't be written any better! Reading this post reminds me of my good old room mate! He always kept talking about this. I will forward this write-up to him. Fairly certain he will have a good read. Thanks for sharing!
Also visit my web blog ; Home Design

Yasinta Ngonyani said...

ahsanteni wote na samahani kwa kutowatafuteni majukumu yalizidi kuliko nilivyotumaini...Pamoja daima.

Anonymous said...


Hi! I just wish to offer you a huge thumbs up for the excellent info you have got right here on this post. I will be coming back to your blog for more soon.