Friday, December 7, 2012

TUANZE MWISHO WA JUMA HILI NA WIMBO HUU MALAIKA NAKUPENDA NA MIRIAM MAKEBA....


NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MWISHO MWEMA WA JUMA NA MATUMAINI YANGU TUPO PAMOJA...KAMA UTAKUWA UNAENDESHA WALE WENYE THERUJI ENDESHENI TARATIBU MAANA KUNA AJILI NYINGI ZIMETOKEA MPAKA SASA..IJUMAA NJEMA....

Nilipoendelea kutafuta zaidi wimbo huu wa MALAIKA...nikakutana na hawa nadhani ni wachina nao wanaimba ebu wasikilize ukipata muda....

Kweli kiswahili sasa kinaenea dunia nzima....haya kila la kheri!!!!

4 comments:

sam mbogo said...

Malaika. hakika ni nyimbo nzuri sana, hasa baada ya kuuimba huyu mama.Pia nimefuatilia katika uimbaji wake ni yeye pekee amabaye ameimba kwa kwa kiswahili fasaha.Ametamka maneno vizuri sana kuliko wengine wote walio fuata baada ya yeye. katika nyimbo zake ninao upenda sana ni ule unaoitwa" hapo zamani sikuwa hivyo".hatakama nilikuwa nimekasirika nafurahi tu, nikiusikia huo wimbo. asante dada Yasinta kwa wimbo. kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kabisa kaka Sam, maana nimesikiliza wengine, wanasema malaika nakupendi na wengine pale waimbapo ningekuoa wanaimba ningekuua...kazi kwelikweli ila Mama huyu kweli anaimba kama inavyotakiwa...Ahsante kaka S kwa kugundua hilo pia:-)

Anonymous said...

halafu hapo dada Kapulya umeharibu lugha yetu kwa kusema MWIMBO HUU sio hivyo ni WIMBO HUU......??????!!!!!!UPO HAPO?

Yasinta Ngonyani said...

Nipo nimerekebisha ahsante kwa kunijuza...usiye na jina sijui ni dada au kaka?