Monday, December 3, 2012

HIVI NDIVYO HALI YA HEWA ILIVYOKUWA FINLAND LEO!!!

Hali ya leo Finland...hapa kwetu bado haijaangua kihivyo ila kuna baridi kali sana kiasi kwamba ile kutoka tu nje pua inasinyaa kabisa....Mwaka huu itakuwa kali kwelikweli...JIONI NJEMA KWA WOTE.....

4 comments:

Malkiory Matiya said...

Duh, Yasinta kweli wewe ni mpekuzi :)Nicky Mwangoka said...

khe jamani poleni dada

batamwa said...

afadhali hilo baridi unajifunika bonge la blanketi halafu ukichanganya na blanketi chapa binadamu mambo yanakuwa mswano sio hapa dar joto utafikiri tuko jehanamu au kamavile jua limeshuka sentimita chache kuja chini,halafu kuwashwa mwili nahilojoto watoto hawalali kelele za joto,ukipandabasi ndio kabisa miharufu ya jasho dsm tabu kabisa jiji la raha na karaha

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Malkiory! ndo maana naitwakapulya:-)

kaka Nicky! yaani si mchezo unaisikia baridi mpaka kwenye mifupa..

batamwa! hii labada inatokana na kukata miti maana dar hakuna mti ukasema ngoja nipumzike hapa kwenye kamti...yaani hakuna miti ya kuleta kaupepepo...kwa siku kama hii nalitamani sana jua...:-(