Thursday, December 6, 2012

JINSI WATOTO WA KIKE WANAVYOJIFUNZA MAISHA ...

....mtoto umleavyo ndivyo akuavyo..ila kuna wakati katika jamii yetu huwa tunazidisha kidogo..mtoto anakuwa kama mtu mzima kabisa. Kwa maana hiyo anakosa ule muda wa kuwa mtoto. Ila tumejifunza mengi na tumekuwa kwa kiutu uzimauzima si kama sasa..au wenzangu mliopitia maisha haya mnasemaje?..Duh!  siku zinakimbia tayari leo ni Alhamisi ya tarehe 6/12/2012..KILA LA KHERI WANDUGU!!!!

5 comments:

Mija Shija Sayi said...

Yaani wee acha tu watoto wa vijijini kazi wanayo hawana pakupumzikia, wakienda shule walimu wanawatuma wakawatekee maji, wakirudi nyumbani ndo balaa..

Duuh..

Yasinta Ngonyani said...

Dada mkuu msaidizi! halafu hapo hapo inabidi ukaokote kuni kwa ajili ya kesho yake kupeleka shule ...sasa hapo kweli kitabu kitafunuliwa kweli??....

penina simon said...

Binafsi haya maisha nayafagilia sana, kwa sababu mtoto wa kike unakuwa ukijiamini, mama akienda shambani hana wasi wasi atakuta umefagia nyumba umepikia watoto uji/chakula, maji umeteka na jioni unajiandaa kwenda kukusanya kuni (hasa wakati wa likizo). hivyo hata ikifika muda unapata nyumba yako unakuwa ni mwanamke kamili.

Utashangaa mabinti wa siku hizi anamaliza STD 7 hajui kusonga ugali,kuisha vyombo, kupika mboga na hata kufua nguo zake mwenyewe, ni aibu kubwa sana hata akiolewa.


Salehe Msanda said...

Siku hizi wazazi wengi tunalea watoto wetu kidot .Com,then tunakuwa wa kwanza kulalamika na kulaumu kuwa watoto wa siku wanamatatizo abc,wakati tumetoka katika mstari wa malezi mema ya watoto,

Kazi za watoto wanadai ajira za watoto kazi kwelikweli.

Yasinta Ngonyani said...

Dada P! Yaani umesema kweli kabisa miaka ile mtoto wa miaka 6 anaweza kusonga ugali kabisa wa kula familia yote lakini sasa hata kukaanga yai sifuri kabisa...

Kaka Salehe ni kweli watoto wa siku hizi hata kucheza michezo hakuna wao na simu pia kompyuta tu..ila inauma kwa kweli.