Monday, December 3, 2012

MWANAFUNZI ABAKWA MPAKA ANAPOTEZA FAHAMU MKOANI RUVUMA!!!

JESHI LA POLISI mkoa wa Ruvuma limefanikiwa kumtia mbaroni Daud Ndunguru (19) wa mtaa wa Hoahoa uliopo Mbinga mjini na linaendelea kumsaka na mwingine jina lake ambaye halikufahamika mara moja linaendelea kumsaka kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kike wa umri wa miaka 12 (jina lake limehifadhiwa) anayesoma darasa la nne katika moja ya shule za msingi zilizopo Mbinga mjini na kumsababishia maumivu makali na kupoteza fahamu.

Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Msimeki zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea desemba 2 mwaka huu huko katika mtaa wa Kihaha nje kidogo ya Mbinga mjini ambako mwanafunzi wa kike inadaiwa alibakwa na watu wawili akiwemo Daud Ndunguru ambaye alikamatwa muda mfupi baada ya kumfanyia kitendo cha kinyama msichana huyo na mwenzake ambaye jina lake halikuweza kufahamika alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Habari zaidi za tukio hilo zimefafanua zaidi kuwa watu hao wawili akiwemo Ndunguru majira ya saa 4:30 usiku walimvizia njiani msichana huyo na kumlazimisha atoe nguo alizokuwa amevaa na kisha kumfanyia kitendo cha ubakaji jambo ambalo limesababisha msichana huyo kupata maumivu makali sehemu za siri na kusababisha kupoteza fahamu.

Hata hivyo kamanda Msimeki alisema kuwa kufuatia kuwepo kw purukushani hizo majirani watoka na kwenda kwenye eneo la tukio ambako walifanikiwa kumkamata Ndunguru na mwenzake alikimbia huku msichana huyo akiwa amepoteza fahamu na walimchukua na kwenda nae kituo cha polisi cha kati cha polisi ambapo walichukua hati ya polisi ya matibabu (PF3) na kwenda nae hospitali ya serikali ya wilaya ya Mbinga ambako amelazwa na anaendelea kupata matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Kamanda Msimeki alisema kuwa mtuhumiwa Ndunguru anatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi upelelezi wa tukio hilo utakapo kamilika na jeshi la polishi mkoani Ruvuma linaendelea kumsaka mtuhumiwa mwingine wa tukio hilo anayedaiwa kukimbia na kutokomea kusikojulikana baada ya kumfanyia kitendo cha kinyama msichana huyo
Habari hii nimeipata hapa

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Habari hii imenugusa mno ukizingatia ni mama na pia ni mwanamke..mtoto wa miaka 12 kaaazi kwelikweli yaani hapa ameshamwaribia maisha yake kabisa. Watu kama hawa sijui huwa wanawaza nini kwa kweli lazima itakuwa wana shida katika vichwa vyao...ngoja niachie hapa maana nina mihasira sana ....

Emmanuel Mhagama said...

Hakuna siku tutamwona shetani akikatiza mtaani, lakini ni rahisi kumwona akiwa amejificha nyumba ya sura za wanadamu wenzetu. Hii siyo tabia ya binadamu wa kawaida, bali ni tabia ya kishetani kabisa. Na haiwezekani kuwepo tabia ya kishetani bila shetani mwenyewe kuwepo. Tusipokuwa tayari kumrudia Mungu shetani ataendelea kututumia kufanya unyama wa namna hii kwa watu ambao ni ndugu zetu walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Mungu na atukumbuke.

ray njau said...


Hii ni stori ndani ya stori kwa kuumiza mioyo ya wazazi wote.
===================================

Steven Bulamu said...

Daa inaumme sana akika binadamu wa sasa nikama wanyama awanna utu ata kidogo,