Monday, August 24, 2009

NI MALI YA MTOTO AU MUME AU MKE?

Matiti hutoa chakula cha mtoto.

9 comments:

Simon Kitururu said...

Ukiniuliza mimi nitasema ni mali ya mke .

Labda mara mojamoja mwanamke akitotoa[samahani:akijifungua] toto linaruhusiwa kulilia na ni kwa muda wa kabla halijajulia kukata tonge.

Kwa wanaume wanaazima tu KIFUNDO kwa adoado kuonyesha maringo yao au tu kwa kumuhakikishia mwanamke kuwa nyonyo ni lake hasa kama huyo mwanamke nyonyo humsaidia katika kumuandaa kishughuli au HUCHOCHEA kufurahia shughuli maridhawa vizuri hasa kama chuchuz ni moja ya eneo lake lenye nukta ya kitekenyeo cha utamu!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Simon?? umeyasema yote mkuu. no more

Kibunango said...

Ni mali yake mwenyewe mama/mke... Hao wengine hupata nafasi tu kwa muda fulani kufaidi

www.tanzaniasports.com said...

Ni mali ya mwenye naye, na ni juu juu ya mwenyewe kuamua mteja wake awe ni nani na kwa wakati gani!.

Unknown said...

Yasinta nawe kwa uchokonozi!!!

Nicky Mwangoka said...

Ya mwanamama! kwani yako wapi?

Anonymous said...

Jamani hii yote yote imetokana na kuharibika kwa maadili. Hata wewe Ngonyani umechapia kuleta mada hii. Maadili yanakwisha ya jamii yetu na dunia nzima kwa kuchukua sana ya wageni na ya kwetu tukaacha.
Wewe umekaa huko nje ukaona watu wanavyothamini sehemu za maumbile yao na kuonesha kwamba sehemu fulani ni ya fulani tu.Mfano umemtoa huyo mama kama mfano kwa matiti yake kuwa nje. Na ukuona uanzishe mjadala wa hisia za uigaji wa tamaduni zisizo na miguu wala mkia.

Kwa wenzetu huko uliko ziwa ni sehemu ya mme pekee kuona. Ndo maana hutakutaka binti au mama anaonesha sehemu hii nje nje kama kwetu hapa uswazi. Maana ndo tamaduni zao. Kwetu sisi, haya ni maumbile tu ambayo mwanamke anayo kama ndevu kwa baba.Ni tofauti za maumbile. Na kila mtu anabeba mzigo wake aliopewa na Mungu.

Kumbe inategemea unatoa swali hili ukiwa na utamaduni gani kichwani na dhamiri ipi. Wasiwasi wangu kwako wewe uliotoa mada hii kwanza umemdharirisha mwananamke Muafirika bila kujua. Ukaona uulizie vile kwako kitu hiki ni muhimu sana kwa mlengo wa tamaduni za magharibi. Ni ya spice na kichocheo cha ngono na kwa kuwa baba hukishika shika na kunyonya kwa raha zenu ukaona utuulize.

Lakini laiti ungemuuliza huyo mama angelikupa majibu yake mwenywe moyoni ya kiafrika kabisa.
Mimi nimemuona bibi yangua akisaga unga kwenye jiwe la kusagia bila kuwa na nguo kwenye matiti..yalikuwa yakicheza cheza ..Lakini yeye hakuona ni shida. sawa na huyo wakati wa kunyonyesha hauni shida. Shida iko kwako na kwa wadau hapo juu..Yeye hilo halioni kwamba ni shida. Kumbe inategemea unatokea wapi kimantiki kuliongelea hilo.
Ndo maana hata wakati wa tendo ..kimila viungo hivyo havikuhusishwa kabisa na tendo la hilo la umbaji. Hadi wapo wamissionari walipopeleka dini katika visiwa vya Caribean wakawafundisha watu kufanya tendo hilo huku wakiwa wanatazamana na kushikana shikana..ndo maana namna ya kufanya tendo "style" ya tendo la ndoa..ikaanza kuitwa Missionary style. Ndo kuanzia hapo wenzetu wazungu walipata kupenda sana maziwa kama sehemu laini za kumshika mama. na baadaye basi ndo kila mtu akaanza kuongeza zingine kama taxi to soweto nk.

Ukikumbuka haya yote na mengine nitayaongea baadaye, usingeweza kutoa mada hii. maana inachochea chembe chembe ya kuwaza ngono tu kwa watu kama ulivyo wewe. Umeitoa hii unajua nini kinaendelea akilini mwako. Ushauri wangu..usitoe mada kama huna utafiti na hujui faida na maudhui ya hayo unayotaka kusema.

Umuombe msamaha huyu mama umedharirisha vya kutosha..kumlinganisha na fikira mbaya. kama zako. Yeye kazi yake ilikuwa ni kunyonyesha tu. basi mengine..hajui..ndo kazi msingi ya kiungo hicho.. Kama wewe unaiita ni mali ya mpenzi..basi ni msimamo wako..

Kumbuka huyo hapishani kabisa kimsingi na Mama zetu.Na juzi tu umetuomba tumuombee mama yako. Leo unasaliti maumbile ya mwanamke kwa kuyapa mjadala hewa. Umenikosea haki hasa mama yangu.

Nawakilisha.

Faustine said...

...Chakula ya mtoto...Kina baba wanadandia tu...LOL!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni kwa kutochoka kuitembelea blog hii. Tupo pamoja.