Monday, August 31, 2009

KUMBE MAISHA NDIO YAPO TOFAUTI HIVI?????

Ngoja leo niwasimulieni kitu ambacho nilipokuwa mdogo nilikuwa nakiwaza. Mimi nilikuwa nawaza hivi kupoje? Nilikuwa na ile picha kuwa maisha yao ni mazuri sana. Yaani wana kila kitu kama vile maisha mazuri, nguo nzuri, nyumba nzuri tena pengine niliwaza hata hawafanyi kazi yaani kazi za mashamba nk.

Nimeshuhudia mwenyewe sasa, watu wanalala njaakila siku, watu wanalala nje na kujifunika mabox (mangumi)na bila kusahau waombaomba .Pia kuna majambazi ambao wanakaa jela miaka na miaka, na kuna wabakaji wengi tu na tena waharifu wa kila aina.

Pia nilikwa nadhani kuna nyumba na tena zote za ghorofa tu. Eti nilifikiri hakuna misitu na wala wanyama wakali. Eee! Bwana, kuna misitu tena leo nilikuwa mstuni kuchuma uyoga na nikakutana na nyoka wacha nikimbie.

Nikakumbuka kuna siku moja nilikuwa nawasimulia ndugu zangu wa Ruhuwiko hali ya huku yaani maisha ya huku si ya kawaida. Nguo unahitaji kuwa na nguo za misimu mitatu:- ni (vinter ), baridi unahitaji nguo nzito sana na maviatu makubwa, makofia, nk…. (Vår) , joto kiasi, (sommar), ”joto” na (höst), ni hali ya hewa ambayo ni mchanganyika wa vyote. Lakini hawakunielewa kabisa. Kwa hiyo kwa mtindo huu hapa kama mpo wengi katika familia kazi kwelikweli. Maana hapo bili, chakula, nk bado hujalipia mmmh sisemi sana kila kitu kinabidi uvumilivu.

Lakini watu wabishi, kuna minongóno watu wanafikiri mimi ni mjanja nawadanganya ile wasije huku ili nifaidi peke yangu. Ya kwamba eti kama kungekuwa kama nisemavuo basi nisingeweza kuishi.

10 comments:

Faith S Hilary said...

Dada Yasinta mbona watu wengi wako hivyo, namaanisha hiyo part ya mwisho mwisho ya watu wa nyumbani kudhani kua hutaki wao waje huku na kuwatisha na hizo "factors". It's ridiculous na wanapoamua kuzamia, ujanja wote kwisha. Binadamu bwana, can't be described sometimes.

Nicky Mwangoka said...

Ni ngumu kuridhisha hata ueleze vipi dadangu. Basi tu ni wakati mwingine unaomba Mungu nao wapate bahati hiyo wajionee wenyewe.

Anonymous said...

Yasinta, pole sana kwa sikitiko. Hali uliyoizungumzia hapa si ya kukuhusu wewe binafsi, ni hali inayowakumba watu wengi wanaojitahidi kuelezea maisha yao ya ng'ambo. Mara nyingi maneno na picha na hadithi za mafanikio za baadhi ya watu wanavyozisikia huwa hawalinganishi na kundi kubwa ambalo lipo kimya kwa kusumbuka na kutaabika ili kukamilisha siku.
Baadhi ya watu wanashindwa kuelewa kuwa mtu anapokuwa amehamia ng'ambo akakutana na hali ngumu huamua kubaki kwa kuwa aidha hakuna utofuati na atakaporudi nyumbani, au, ameamua kubaki katika mfumo ambao angalao unaeleweka kwa unachokipata na kazi inayofanyia kile kinachokatwa kodi, au wanaobaki kutokana na mazingira ya kufaa ya elimu na wengine huamua kubaki kwa kuzoea tu ama kwa kuamua kutokutaka kurudi walikotoka, ndiyo maamuzi yao.
Ndugu mmoja aliwahi kusafiri kwenda kwa nduguze Ulaya, alipofika huko alianza kulala na kujitahidi kula na kutizama TV bila kufanya kazi, alipotakiwa kuhama akajitegemee akaanza kulalamika kuwa ananyanyaswa, ndugu yake alipompa bili na mkataba wa nini kitafanyika ikiwa bili ya pango, maji, umeme, internet haitalipwa na kutakiwa kuanza kujitegemea, siku chache tu baadaye alisema anataka kurudi Tanzania akafikirie upya. Ni mwaka wa tatu sasa hataki kusikia habari ya kwenda Ulaya zaidi ya kutembea na kurudi.
Yasinta, usisikitike, huwezi kuwaridhisha watu wote kwa wakati wote hata siku moja. Hata na hivyo, umeuelezea ukweli ulivyo, ni uamuzi wa mtu kuamua kusikiliza ukweli na kujipanga vyema. Kipindi cha watu kuambiwa maneno wanayotaka kusikia ya kufurahisha na uzuri kimepita. Endelea kusimulia maisha kadiri utakavyo na kadiri upendavyo!

chib said...

Kuna watu wana ubishi wa kinasaba, huwawezi hao.
Lakini ni vyema uendelee kuwaelimisha.
Kwa sasa ndugu zetu watasha ambao wako hohehahe wakikuona mtaani uko smart kidogo hawakosi kuja kukupigia mizinga na kuwaacha wenzao, maana wenzao roho kutu, wakti sie bado tuna ka huruma. Mie nimeyashuhudia kote huko nilikopita.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndio chib, kuna mijabaa inabishia redio mpaka wanabadilisha taarifa ya habari kwa kufuata rijamaa litakavyo.


kwa nini unawatishia maisha hao uwatishiao kuwa ulaya sio wakati wewe unaishi na unasavaivu kama kawa?

acheni mikwara hiyo bwana. kama ulaya kungekuwa kubaya basi nawewe ungekuwa marehemu. wao wanataka kubadili mazingira nyie mwawapiga mkwara???

ni sawa na wadhungu wanaoangalia bibisi na kuona vita afrika wakaamini kote ni vita wakija wanakuta watu wazuuri wenye upendo, amni nk.

nikiamua kuja swedeni sitojali mikwara yako Yasinta, nitakuja tu na kwataarifa nitafikia nyumbani kwako na kukuaa miezi sita ya mwanzo!!!!!

Koero Mkundi said...

Ukitaka kujua uhondo wa ngoma basi ingia ucheze, hivi kwa nini msiwaache watu waingie wacheze wenyewe, kuliko kuwatisha kuwa mirindimo ya ngoma sio mizuri na haichezeki?

Kamala Miezi sita kwa Yasinta kula kulala....Duh!!!
Kaaaazi kweli kweli......

Mzee wa Changamoto said...

Tobaaaa!!!
Hivi kuna vitisho hapa ama fikra za anayetafuta sababu ataona vitisho? Labda nikumbushe tuu yaliyosemwa na huyu mtu kuwa "All truth passes through three stages. First, it is ridiculed. Second, it is violently opposed. Third, it is accepted as being self-evident."
Arthur Schopenhauer (1788 - 1860)

Kisha nami nijifanye "smart" kukumbusha niliyoandika kuhusu haya haya hapaaaaa (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/01/them-i-them-lucky-dubethe-other-side.html)

See ya NEXT IJAYO

Fadhy Mtanga said...

Tobaa! Takribani wiki nzima sikupata nafasi ya kusoma blog hizi. Kumbe nimekosa mambo lukuki.
Enhee! Kwa hiyo unataka kusema mawazo kuwa Ulaya ni kuku kwa mrija ni kujidanganya? My God, kumbe ndo ilivyo.
Bora umesema. Lakini watu wabishi unawaacha kama walivyo.
Ni hayo tu!

Anonymous said...

Apa ni kazi, mlongo, mawazo yako nafikili kila mtu ambaye hajawai kufika uko anamawazo kama ayo na nivigumu kumwelewesha mtu ambaye hajafika kwani wanaoishi uku wakifika nyumbani uwa hawasemi ukweli licha ya hivyo wakisha chanji ela zao za uku ingawa ni kidogo lakini kwa nyumbani unamzidi ata anayefanya kazi ya maana ingawa wewe uku utakuwa mfagiaji au mmbeba mabox. ni vizuri watu kujionea wenywe kama anavyosema bwana Kamala bila kujionea hakuna atakaye kuamini au kukuelewa. Mlongo mi mwenzio sasaivi nimejilimia kamchicha na likolonyungu huwezi kuamini ukifika apa kwangu ungekuwa kalibu ungepittia kuchuma. kama kunyumba.

Yasinta Ngonyani said...

Nawashukuruni wote na nadhani hata hivyo naona wengi wanaona niutani tu. Basi mimi nasema hivi karibuni sana tena nina jumba kubwa tu kwa hiyo wote mtapata nafasi. Kamala unakaribishwa kukaa hapa mwaka mzima:-)

Ahsanteni woooteeee. Samahani kama nimewatisha lakini sijawatisha ni ukweli.