Wednesday, August 19, 2009

KUFA NA KUZIKANA

Sijui nianze vipi?:- Mila na desturi, kweli kila watu wana zao. Nimeishi hapa Sweden sasa miaka mingi kidogo. Lakini bado sielewi pale panapotokea msiba (mtu kufa)

Nina maana hapa Sweden mtu akifa basi wahusika watatangaza kwenye gazeti na pia wanaandika lini mazishi yatakuwa. Sasa hapo ndipo nisipoelewa mimi, yaani hapa sasa sio kwamba kila mtu kuhudhuria msiba huo? la hasha. Ni lazima ualikwe na unapoalikwa ni lazima utoe taarifa kuwa utafika. Sababu kubwa ya kufanya hivyo wanataka wajue kwamba waandae chakula cha watu wangapi.

Sio kama nyumbani TZ mtu ana safari zake au alikuwa shambani, mara akasikia kwa fulani kuna msiba, basi ni kuataacha kila kitu na kwenda huko na kuungana na wafiwa. Kusema kweli mila za huku hasa kuhusiana na misiba inanichanganya sana.
Kuna siku niliwakuta watu wanazika na walikuwa watu watano tu yaani hata ndugu akisikia ndugu yake amekufa haendi kwenye msiba anasubiri kualikwa. Huku mtu hawezi kwenda msibani au kuzika ni mpaka awe rafiki au ndugu na hapo pia mpaka aalikwe. Yaani hata awe jirani hakuna mtu anaenda kila mtu na lwake .

Kitu kingine tena ambacho ni ajabu kidogo kwa mimi sijui wenzangu mnalijua hili. Ni hiki kitendo cha watu wakiwemo ndugu wa karibu wa marehemu kuondoka kanisani na kurejea majumbani mwao baada ya misa na kuuacha mwili wa marehemu hapo, yaani kwao huko ndio kuzika, baada ya hapo shughuli ya mazishi hufanywa na wazikaji wa kukodi ambao hulipwa kwa kazi hiyo, tena hakuna hata kulala matanga, shughuli inakuwa inaishia kanisani. Tofauti na TZ, nadhani wote tunajua nyumbani tunafanya nini. Kwa sababu kama unaenda kuzika ni lazima kuzika kwa maana kuhudhuria mpaka makaburuini na kuhakikisha mwili unafukiwa sio kuuacha mwili kanisana, halafu? Naamini mazishi ni wajibu wa wote waliofika pale kumsindikiza mwenzao katika safari yake ya mwisho yaani katika shamba la Mungu (makaburini) na sio kukabidhi mwili kwa watu wa kulipwa na nyie kuondoka na hamsini zenu.

Pia hapa kuna mtindo wa kuchoma mwili na halafu yale majivu kwenda kuyamwaga sehemu ambayo marehemu alikuwa anaipenda kama vile ziwani au mlimani. Na wengine wanazika au wanaweka kwenye chupa na kuhifadhi kwenye nyumba maalumu (minneslund) sehemu ya makumbusho.

11 comments:

Nicky Mwangoka said...

Hii sasa kali sijawahi kusikia kabisa. Loh Dada wewe u makini katika habari.Unapata wapi haya? Hongera!

Fadhy Mtanga said...

Tembea uone, mwenzetu umetembea umeona.

Kuishi kwingi ni kujifunza mengi, nasi twaishi na kujifunza mengi.

Ahsante Sista Yasinta.!

chib said...

SASA HATA KWENDA HAPO KANISANI NDIO LAZIMA UPATE MWALIKO!!??
Kwetu Bongo ukifanya hivyo, nafikiri utasusiwa maisha yako yote pamoja na kuwa wewe ndiye uliyefiwa.
Wenzetu utu walisha achana nao kitambo

Coco said...

Dada Yasinta yote uliyoyasema ni kweli na mie pia nilishuhudia kabisa,nilishangaa mno roho iliniuma pale wote tulivyoondoka kanisani wala makaburini hatukwenda aah, Na hii mpaka ualikwe iliniacha hoi mi nilifikiri ni huku tu nilipo kumbe hadi huko.Kweli tembea uone!!!

Anonymous said...

NI KWELI TENA YASINTA UMENISEMEA YA MOYONI MWANGU DADA,SIKU MOJA MAMA MDOGO WA BOYFRIEND WANGU (WASWEDISH)ALIFARIKI HIVYO JAMAA AKANIAMBIA KAMA NATAKA TWENDE KANISANI KTK MAZISHI,BASI SBB HUYO MAMA ALIKUA ANANIPENDA SANA ILIKUA NI LAZIMA NIENDE,NKUFIKA KANISANI NILISHANGAA KUONA MBALI YA MUME WA MAREHEMU NI MIMI NA JAMAA 2 WENGINE ALIKUA NI MCHUNGAJI NA M2 ANAYEIMBA NA WENGINE HAWAFIKI WA5 AMBAO NI WAFANYAKAZI SIJUI WA KANISANI.NILILIA SANA KWA UCHUNGU KUONA BINADAMU HANA WA2 ZAIDI YA WA5 WAKUMSINDIKIZA KTK SAFARI YAKE YA MWISHO NA NDIPO HAPO NIKASEMA SIWEZI ZEEKEA HAPA KWE2 HATUNA KI2 LKN KUNA U2.HAPA WANA LIFE YA AJABU SANA.M2 ANAWEZA KUFA AKAOZA MIEZI 6 NA JIRANI MLANGO WA PILI AKAISHI KAMA KAWAIDA.WA2 HAWAJUI TU LKN KULE HOME NA UMASKINI WOTE LKN VICHEKO HAVIKAUKI.HAPA KUNA WA2 HATA SIKU YA CHRISTMAS HAWANA WA KULA NAYE NI YEYE PEKEE,

Mzee wa Changamoto said...

Duh!! Sijui hili ni tatizo ama namna tuonavyo tatizo ndio tatizo?
Kwa sisi tuliokulia nyumbani tunaona hi kama haipendezi lakini kwao wanaona sisi tunaendekeza mambo yasiyokuwa na uhai. Kuna aliye sahihi kati yetu na wao?
Zamani nilikuwa nikilia mtu akifa. Nililia kwa kuwa alikuwa amekufa na niliamini hakustahili. Sasa nalia mtu akifa. Lakini si kwa sababu atakuwa amekufa , bali kama hakubahatika kutimiza baadhi ya malengo yake makuu. Kwa mtu nimpendaye saaana, naamini nitahuzunika kutokua naye, lakini kama hilo ndilo pumziko pekee analohitaji, basi ntamuombea apumzike na sitataka kumlilia saana kwani (kama anasikia) ataendelea kuteseka kuwa ameacha watu tukiwa hatuna msimamo. Niliwahi kuandika kuhusu mjomba wangu ambaye nilimlilia na sasa nalia kuwa nilimlilia (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/05/bado-nalia-kuwa-nililia.html) na sasa nimeshamuomba msamaha kwa hilo na NINASHEREHEKEA MAISHA NA KAZI ZAKE KULIKO KUMLILIA.
Naamini ni mitazamo kiasi. Kwa imani zetu, kama wafao HUANGALIA CHINI / JUU KUTUONA (TOKA HUKO WALIKO), basi vilio vyetu ni mateso kwao na pengine tunastahili kuwashukuru na kusherehekea maisha yao. Lakini kumuacha akawa kama HAKUWEPO nalo laweza wajione kuwa hawathaminiki.
Sina hakika ni nani aliye na asiye sahihi kati ya hao wa-Swidi na sisi waTanzania. Lakini nijualo ni kuwa yawezekana kama kuna tatizo hapa, basi THE WAY WE SEE IT IS THE PROBLEM

Ramson said...

Na ndio maan naipenda blog hii ya maisha, mara nyingi napata habari mpya za kiuchunguzi, mimi haya sikuyafahamu kabisa, lakini hiyo habari ya asiye na jina inasikitisha zaidi, marahamu kuzikwa na watu watano? nakumbuka kijijini kwetu iliokotwa maisti ya mtu asiyefahamika na baada ya Polisi kutoa ruksa ya kuzika mzee mmoja aliruhusu maiti ile ifanyiwe taratibu za mazishi nyumbani kwake na kutokana na umaarufu wa mzee yule watu wengi sana walijitokeza kumzika marehemu yule asiyejulikana, kwa huko Sweden naamini maiti ili ingetupiwa mbwa.....labda nimeends mabali lakini hiyo ndiyo picha niliyo nayo kutokana na makal hii na maoni ya baadhi ya wasomaji...

Dalili ya mvua ni mawingu.......
Dada Yasinta usishangae hata huku kwetu hilo la kuhudhuria mazishi kwa mualiko linakuja na linaanzia jijini Dar, nimeshuhudia mahali fulani.....
Si siku nyingi tutayashuhudia hayo.....

Born 2 Suffer said...

Hata mimi nashangaa sana hawa watu huwa wanaishi vipi yani ukitazama upande mwingine huwa wanafanya mambo hayana mwelekeo kabisa, kitu kinachowasaidia ni rangi yao tu hatuwezi kusema wanafahamu na wanjua kila kitu, na pia siwafahamu wanaamini kweli kama kuna mungu utakuta wana act film zao katika kanisa mambo ya upuuzi wanafanya humo ndani ni vitu havingii akilini yani.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mimi nikifiwa hata wewe yasinta ukifa au mzee wa changamoto, nitafurahi kujulishwa baada ya mazishi ili tusisumbuane.

hivi karibuni nimefiwa na bibi yangu aliyekuwa na umri mreefu kiasi. nilishangaa kuona wazazi wangu wanalia! yaani mizee mizima na mi mama inalia kama vile haikujua kuwa itakuja siku afe.

basi bwana, siku moja niliwahi kumwambia bibi yangu kuwa anaugua sana kwa sababu ya uzeee, we, we, we!1 alinishitakia kwa kila mwanae na kuongeza kwamba nimesema hasitibiwe kwa sababu ni mzee na uzee na hivyo nimwache hafe, imajini, mtu wa miaka lukuki anaogopa kufa utadhani mimi ndo mwenye kauli ya mwisho juu ya uhai wa mtu!!!!!!

anyway, siku hizi mzee mzima siudhurii harusi ya mtu wala msiba. naishi kama yesu aliyemwambia jamaa waacheni wafu wazike wafu wao Matayo 8;22

Unknown said...

NIMEJIFUNZA JAMBO KWA MAKALA HII NA MAONI YA WENZANGU PIA.....

Yasinta Ngonyani said...

Asanteni sana, ni kweli tembea uona lakini pia inasikitisha sana kuona jambo hili najua kuna wengine watasema we unasema hivi kwa vile hutaki na sisi tuje huko HAPANA hii ni hali halisi kabisa.Kila la kheri wote na TUPO PAMOJA.