Monday, August 24, 2009

JE? DALILI ZA KUZEEKA NI ZIPI?

Nimeamka na nikaanza kujiangalia kwenye kioo....lol , nikaona uweupe wacha nishtuke nikaanza kuwaza hivi ni kweli nimefikia umri wa kupata MVI? Maana kuna usemi usemao ukiwa na MVI basi ni dalili ya uzee....lol

Nimeona si vibaya kama tukisaidiana kujadili hili swala la uzee. Inasemekana pia watu wengi hawataki kuamkiwa SHIKAMOO kwa vile wanajiona ni wazee. Na wengine hawataki kuwa na makunyanzi. Na hapa ndo wanaanza kutafuta mafuta(lotion) za kuondoa makunyanzi usoni ili kuonekana vijana. Hawakumbuki kuwa siku moja ni LAZIMA watakuwa na makunyazi yaani hatuwezi kuisha maisha yote tukiwa vijana tu. Hapa duniani kuna mambo.

Kuhusu MVI je? inawezekana ni urithi? Nisaidieni sio kwamba naogopa kuwa mzee hapana ila nataka kujua tu.

Hapa nimeona si vibaya kama nikiambatanisha na mada hii hapa ambayo Mzee wa Changamoto aliiandika siku si nyingi. Nayo inaongelea kuhusu kuzeeka:-

Kipi chazeeka kwanza, miili ama akili????

Nikiwa kazini na "rafiki" yangu (ambaye ana umri mkubwa), tulikuwa tukiongelea jinsi watu wanavyoukimbia muonekano wa umri wao. Na yeye alionekana kutetea hilo na kusema kuwa awali alikuwa akionekana ana mvi nyingi kichwani na alijihisi MZEE. Lakini baadae akapata dawa ya kubadili rangi ya nywele zake na hilo likamrejesha katika "ujana" aliokuwa akiutaka. Na baada ya kuonekana kuwa kijana zaidi, akaanza kujihisi kuwa na hata nguvu na uwezo wa kufanya mazoezi. Sasa hivi anakimbia dk 30 za mapumziko ya mchana kazini na amebadili mfumo wake wa chakula, amebadili mfumo wa maisha na kwa hakika sasa anaishi "maisha ya afya" zaidi kuliko ilivyokuwa awali. Hakuna anayebisha kuwa KUJIONA KIJANA kumemsaidia kubadili mfumo mzima wa maisha. Lakini kwangu swali likabaki kuwa alizeeka mwili ama akili? Ni kweli kuwa kabla hajajiona kuwa kijana zaidi mwili wake usingeweza kutenda mazoezi afanyayo sasa? Na je! kama angekuwa amezeeka mwili, angeweza kutenda atendayo hata kama angekuwa anapenda kufanya hayo?
Ninawaona wengi ambao kwa kujiona "wamezeeka" hawajiendelezi na shule, hawawekezi maishani na hata hawafanyi mengi mema ambayo yangewasaidia miaka michache ijayo. Wanaokimbia vivuli vyao kwa kujifanyia upasuaji kutafuta muonekano wa ujana, kutumia makemikali "kijijananisha" na hata kuvaa ki-ujanaujana wakiamini hilo litawapa HISIA nzuri za namna walivyo. Pengine inawasaidia kwani wapo ambao wakishakuwa katika "ujana" wautakao huanza kutenda yale ambayo ni ya manufaa kwa maisha yao na zaidi kwa wale wategemezi wao lakini ambayo wangekuwa wamefanya ama walistahili kuyafanya kabla "hawajajibadilisha."
Haya na mengine mengi hunifanya nijiulize tena na tena.
KIPI CHAZEEKA KWANZA? MIILI AMA AKILI?

6 comments:

chib said...

Dada Yasinta kuna watu husema akina mama wengi hasa wazungu ukiwauliza umri wao hawasiti kuusema, lakini kikomo ni miaka 40, baada ya hapo husema tu ya kuwa wana miaka zaidi ya 40 lakini hawasemi tena 45, 51, 59 nk. Sasa sijui ndio kama ile kataa shikamoo ya kwetu au...

Unknown said...

Dada umesahau, unajua hata kusahau sahau ni dalili ya uzee....LOL

Jamani hata mie naogopa kuzeeka yaani kila nikiona vibabu vizee vilivyo na makunyanzi na mikongojo yao ya kutembelea. nashusha pumzi na kujiuliza "Hivi na mimi kama nitakuwa na umri mrefu hapa duniani nitakuwa kama hawa wazee!"

lakini yote ni heri tu.....ila wasiwasi wangu ni hiki kizazi tulicho nacho.
Nakumbuka zamani wazee walithaminiwa na kutumika kama visima vya kuchotea busara lakini siku hizi wazee hawafai, wamekuwa waongo na matapeli ajabu, siku hizi ukienda kununua shamba au kiwanja nje ya mji jihadhari sana na vizee, kwani vina ndimi kali za kushawishi na usipokuwa makini uatatapeliwa na hutakuwa na la kufanya.

Jamani samahani simaamishi wazee wote ndivyo walivyo bali baadhi yao ndio wanaoharibu sifa hii ya uzee........

Yasinta Ngonyani said...

Upo sawa kabisa kaka Chib wengi hawapendi kabisa hilo. Lakini sijui hawawazi kuwa hawatakuwa vijana milele na lipi ni tatizo la kuwa mzee?

kaka Shabani, Kusahau si uzee kwani hata mtoto mdogo anaweza kusahau au vijana wadogo. Hahahahah!! eti mi naogopa kuzeeka utazeeka tu.....LOL haya naacha isije nikaharibu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

utaogopaje kuzeeka? si ni halali yako? kwaniwewe nikijana? jiandae hata kufa ikibidi.

mimi siogopi kuzeeka kwani sikuwahi kuogopa kuwa kijana nilipokuwa mtoto. ila du

Koero Mkundi said...

Kamalaaaa....kama vile nakuona utakapozeeka, maana utakuwa na kimkongojo chako na ugoro wako kibindoni halafu unabwia ugoro wako na kutema mate pwaaa,.....njiani......LOL

Mwenzwenu mie nishaanza kuzeeka na mvi hizooo naziona zinaninyemelea.
....LOL

Simon Kitururu said...

Mimi na mvi tokea Mtoto!

Ni hilo tu!