Monday, February 15, 2016

WIKI HII TUANZE NA KUTEMBELEA ALIKOZALIWA KAPULYA WENU KIJIJI CHA LUNDO/ WILAYA YA NYASA


 Hapa ni kilimo cha maksai katika kijiji cha Lundo Wilaya ya Nyasa
Na hapa ni Beach ya BioCamp-Kijiji cha Ndengere Wilaya hiyo hiyo ya Nyasa...  yaani nimefurahi, furahi mno kupata tena taaswira ya vijiji hivi  Ndengere, Lundo, nk...ni sehemu zangu nilizokulia yaani  nimekumbuka  mengi sana hasa mlo wa samaki na ugali wa mhugo:-)  hapa ndipo nilikotoka...

2 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kapulya pulika, umenikumbusha mbali dugu yangu. Hata ndugu Mbele atapenda hii kitu bila shaka. Je wajua kuwa ziwa Nyasa ndilo ziwa lenye samaki aina mbali mbali kuliko maziwa yote duniani?
Ubarikiwe na kuwe na kumbukumbu njema ingawa hao maksai nawaonea huruma. Kuna haja ya kununua matrekta mkaachana na utesaji huu wa wanyama.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango uli bwanji!
Nilijua tu utafurahia hiyo kumbukumbu pia. Kuhusu ziwa Nyasa kuwa ni lenye samaki wa aina mbalimbai duniani hilo sikulifanyia utafiti..Ahsante kwa taarifa. Nakubaliana nawe hao maksai ni huruma juu ya huruma ni kweli inabidi hili jambo lifanyiwe kazi.