Sunday, February 21, 2016

LEO NI KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWA BINTI YETU CAMILLA ANATIMIZA MIAKA 18 HONGERA SANA BINTI TEYU....


Mwaka 1998 tarehe 21/2 alizaliwa binti huyu. Ni siku ambayo familia hii haitaweza kusahau. Twamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote. Na twazidi kumwomba amwongoze binti yetu Camilla katika kila akifanyacho ili kiwe vema. Pia twamshukuru Mungu kwa kutuongoza sisi wazazi/walezi katika malezi ya binti Camilla. TWAKUTAKIA SIKU YAKO IWE NJEMA SANA. HONGERA Binti, dada, rafiki, mjukuu nk.
 Nyumbani Ruhuwiko 2015...naenda kwa babu kuomba mboga (mandondo) maharage si mnaona eti nimechukua na bakuli yangu kabisa/Poti:-)
Keki nayo haikukosa katika kumbukumbu hii ya leo ya miaka 18....Duh  mama  sasa najiona ule uzee/utu uzima unazidi kupiga hodi. Haya karibuni tujumuike kumpongeza binti Camilla!!

17 comments:

Baraka Chibiriti said...

Hongera sana sanaaaaa Mdogo wangu kwa kutimiza miaka 18, nakutakia maisha mema sana na yenye upendo mwingi daimaaaa!!!!

- Mama hongera sana kwa kukuza.

Yasinta Ngonyani said...

Niandika kwa niaba kama nilivyotumwa...Kaka Baraka AHSANTE sanaaaa kwa kunitakia yote mema pia kwa upendo wako. Nami mimi mama Camilla nasema Ahsante sana.

Mbele said...

Kwa niaba ya wajomba wote, kuanzia wa-Nyasa, wa-Ngoni, wa-Matengo, na kadhalika, nampa hongera binti Camilla, na hongera kwenu wazazi.

Anonymous said...

Hongera sana binti Camila. Kuanzia sasa uachane na mambo ya kitoto. By Salumu.

Anonymous said...

Hongera sana kwa kukuza, mungu azidi kumuweka binti yetu Amin. Grattis Camilla.

Denis Ntyangiri said...

Happy birthday Camilla

Yasinta Ngonyani said...

Kwa niaba ya mtimiza miaka maana kaande shule:-
mjomba Mbele Ahsante sana. Nasi wazazi twasema AHSANTE

Mjomba Salumu Ahsante Nitazingatia ushauri wako.

Usiye na jina wa 9:48AM Ahsante ndugu yangu. Naye Camilla nasema TACK SÅ MYCKET!
Mjomba Ntyangiri! AHSANTE.

Unknown said...

Hongera sana tena mno.Ninakutakia maisha mema yenye baraka na upendo daima dawamu.

Yasinta Ngonyani said...

Usiyejulikana wa saa 9:28AM ahsante sana baraka zako. Nawe Uwe salama.

Anonymous said...

Happy Birthday Camilla,
ushauri kwa wazazi mle likolo kwa wingi mtoto asiwapite urefu
hongera kwa kukuza
nilikupoteza zaidi ya mwaka nimekupata furaha ilioje

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina wa 6:36PM! Kwa niaba ya Camilla nasema Ahsante...Umenichekesha mno eti tule likolo kwa wingi ili tusipitwe urefu na wanetu:-) Nasi wazazi twasema Ahsante kwa pongezi!....KARIBU TENA NA TENA SANA

Penina Simon said...

Hongera , Umekuza mdogo wangu

Yasinta Ngonyani said...

Dada P.....Ahsante kwa kweli namshukuru Mungu.

Anonymous said...

Hongera ya kuzaliwa tototoooooooo cammila.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina wa 9:15 PM! Kwa niaba ya dada Camilla Nasema ahasante sana.

NN Mhango said...

Huyu bi mkubwa nilimtakia heri ya kuzaliwa lakini sioni ujumbe wangu au nilisahau kubonyeza kitufe cha publish your comment. Woooi basi mpe hongera zangu hata kama zimechelewa.

Yasinta Ngonyani said...

Bi mkubwa kanituma kwa niaba nikushukuru mjomba Wake na kasema wala hujachelewa kabisaaa. Ahsante njomba:-)