Tuesday, May 19, 2015

PICHA KUTOKA KITABU CHA DARASA 5 TUJIFUNZE LUGHA YETU! KWA DARASA LA NNE...

Na kitabu chenyewe kinaonekana hivi kwa nje....Picha ya kwanza ni  hadithi ya jogoo aliyesema, ya pili ni Sadiki na Sikiri, ya tatu nimesahau  sijui kuna anayekumbuka anisaidie?.ya nne ni Sizitaki mbichi hizi

10 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yasinta usitake kuniliza. Maana umenikumbusha mwaka 1973 nikiwa darasa la tatu., We acha tu.

Yasinta Ngonyani said...

Mwaka 1973 la tatu mmmhhh kumbe ww wa kadeni..(kingoni) unakaribishwa hapa kwetu maana kuna kitabu cha darasa la tatu mpaka la sana ,,,,

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ulildhani mie ni yanki siyo? Ni kujitunza tu vinginevyo ni kababu fulani maana kitegemezi changu cha kwanza kiko chuo sasa.

Yasinta Ngonyani said...

Unaonekana yanki ama kweli wajua kujitunza nipe siri nami nionekana yanki wakti kitemezi changu kikianza chuo:-)

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Usijuruhusu kukasirika au kutishwa na lolote. Kula vizuri hasa kwa kuepuka chumvi mafuta na sukari. Lala vya kutosha, kunywa maji. Hata hivyo, wakati mwingine ni majaliwa yake Muumba japo tunaweza kupendekeza tuliyopendekeza. Huwa nina falsafa moja kila linitokeapo jambo hasa lile baya: It is not the end of the world.

Anonymous said...

Ni kitabu cha darasa la tatu hicho. Unajua darasa la kwanza tulikuwa tunatumia Kitabu cha kwanza cha kusoma na Kitabu cha pili cha kusoma. Darasa la pili tulitumia kitabu cha tatu cha kusoma na Kitabu cha nne cha kusoma. Darasa la tatu ndio tukaanza Tujifunze lugha yetu kitabu cha tano. Kwa hiyo hicho kitabu cha 5 kwenye picha si kwamba ni cha darasa la tano, ni cha darasa la tatu. Darasa la tano kuna habari za Umoja ni Nguvu, Kapulya Mdadisi (uwimbombo na ulindi), Hekaheka mtoni, Safari yenye mkosi, Mafuriko ya mto Rufiji, Ulinzi na Usalama, Asiyesikia la mkuu huvunjika guu (nganenepa sasa Kandi, shime chakula changu), Kuheshimu bendera ya taifa, Mapinduzi ya Unguja, Sauti ya Tanzania Dar-es Salaam (hapa tunapata wimbo maarufu wa "Tanzama ramani utaona nchi nzuri"), Mwasimba katika mapango ya amboni, Chilunda apambana na chui...

obat vimax said...

vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg

Unknown said...

samahani Nilikuwa natamani kujua mwandishi wa hiki Kitabu alikuwaga Nani?

Mtanzania halisi said...

Kitabu kiliandikwa na wizara ya elimu ya taifa kwa kukusanya mashairi na hadithi mbalimbali zilizotungwa na watu tofauti

Anonymous said...

Aisee uko vizuri,ulivyotaja hizo hadithi kwa hicho kitabu ni as if niko tena kwa class