Wednesday, May 20, 2015

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU BIBI YETU VALERIANA NGONYANI -MBAWALA!!!


ILIKUWA MARA YANGU YA MWISHO
KUONANA NA BIBI 2005 MWEZI WA NNE
Leo ni tarehe 20/5 ni miaka kumi imepita tangu bibi yetu mpendwa Valeriana Ngonyani-Mbawala atutoke. Kwangu ni kama vile jana tu. Alifariki 20/5/2005 katika hospitali ya Liuli. Sisi wajukuu wako wote, watoto wako ndugu na marafiki wote wanakukumbuka daima. Bibi Valeriana ni huyo aliyejifunika kitenge, katikati nadhani mnajua au basi ni mimi na mwishoni ni mama yangu mdogo, mdogo wake mama. TUTAKUKUMBUKA DAIMA KWA NJIA YA SALA ZETU. USTAREHE KWA AMANI AMINA. Na hapa naweka na huu wimbo kwa ajuli ya akina bibi wote walio hai na waliotutangulia ..........

TUWAOMBEE BIBI ZETU!


2 comments:

Nicky Mwangoka said...

Namwomba mungu ampumzishe palipo pema Bibi Yetu. RIP Bibi Valeriana Ngonyani

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Nicky ahsante sana kwa kupita hapa na kuacha yakivya moyoni. Pumzika kwa amani bibi!