Monday, May 18, 2015

JUMATATU YA LEO NIMEKUMBUKA HAPO ZAMANI NIKIWA NA UMRI KAMA HAWA WASICHANA....

Nachotaka kusema ni kwamba watoto wa siku hizi hawawezi  kazi kama hizi, yaani kuchota maji, Kutwanga, kupika chakula  wala hata kuwaangalia wadogo zao wazazi wawapo shambani. Yaani najiona kama ni mimi huyo mwenye ndoo ya kijani. Kizazi cha zamani/enzi hizo watoto walikuwa wakakamavu na wenye afya njema, ila watoto wa kizazi cha sasa ni walegevu mno

2 comments:

Christian Sikapundwa said...

Hiyo Dada yangu ndiyo hali halisi ya Mwafrika,na tamaduni zake,lakini hali hiyo ya watoto kubeba vitu ,kuni,maji na vitu vingine vijijini bado hali hiyo ipo hadi leo.
Kasheshe ipo Mijini,watoto watwike ndoo kichwani mbona haiwezekani. wanaona kama wanaonewa au jamii itawacheka ukiongeza na utanda wazi basi tumishiana.
Nashukuru kama utaendelea kuwaelimisha na kuwa kumbusha wajibu wao.na wapi walikotoka Baba na Babu zao. Chenjelai.

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kabisa watoto wa mjini wataona wanaonewa sio kutwika ka ndoo ya maji tu hata kupika nk! Ama kweli chenjelai :-)