Thursday, June 26, 2014

HIVI NDIVYO YALIVYOKUWA MAPISHI NA MLO WA LEO JION AU SASA HIVI.....

 Ndizi  mzuzu, viazi vitamu. mihogo
 Natanguliza samahani yangu ....hapa ni nyama ya kiti moto
 Ikifuatiwa na kachumbali ambayi ni nyanya, kitunguu, kabichi, limau na pilipili kwa mbaliii bila kusahau chumvi:-)
...na hivi ndinyo ilivyoonekama sahani yangu ...ooh nilisahau kulikuwa na uyoga pia...ila chakula bado kingi kwa hiyo karibuni sana. BASI WALE WENYE JIONI  WAWE NA JIONI NJEMA NA MCHANA WAWE NA MCHANA MWEMA PIA ASUBUHI BASI IWE ASUBUHI NJEMA.  PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA......KAPULYA

NIMEIPENDA RAMANI HII YA AINA HII YA AFRIKA...UBUNIFU HUO!!!

RAMANI YA AFRIKA
Imetengenezwa kwa kubandikizwa majani ya ndizi yaani ni asili kabisa ...ngoja niimbe na kawimbo haka ka afrika yetu:-
Mungu ibariki Afrika, Wabariki Viongozi wake,
Hekima Umoja na Amani, Hizi ni ngao zetu, Afrika na Watu wake,
Ibariki Afrika, Ibariki Afrika, Tubariki watoto wa afrika.
 
SIKU IWE NJEMA KWA WOTE...TUPO PAMOJA DAIMA

Tuesday, June 24, 2014

KAKA S. ANAMPONGEZA MTOTO WAKE KWA KUPATA KOMONIO YA KWANZA

KILINDA SAMUEL MBOGO
Jumapili  22/6 Kijana Kilinda alipata komonio yake ya kwanza. Bahati mbaya sikupata nafasi kwenda kuhudhuria siku hii. Ila nimehudhuria kwa kuangalia picha kama muonavyo. Nimetumiwa picha nami nimeona niwashirikishe wenzangu maana baadhi yetu tunakumbuka sana siku hii...HONGERA SANA KILINDA SAMUEL MBONGO KWA  SIKU HII...HII NI ZAWADI YANGU KWAKO....SHANGAZI YAKO YASINTA a.k.a Kapulya/kadala.

Monday, June 23, 2014

ILIKUWA 2007 NYUMBANI RUHUWIKO...NIMEONA IWE PICHA YA WIKI!!!!!

 Niliona ni bora nivae na kofia:-)
mmmhh haya ya kofia mimi siyawezi ....lakini sasa eti nimefumba macho sijui ndo nini?

Friday, June 20, 2014

CHAKULA KILICHONIKUZA MPAKA KUWA KAMA NILIVYO LEO....

Nimekitamani kweli chakula hili ..samaki, ugali na bamia..mmmhhh nausikilizia utamu wake.
JIONI NJEMA KWA WOTE

Tuesday, June 17, 2014

JIONI YA LEO NA UJUMBE HUU!!!

Kwanini ukubali starehe ya sekunde iharibu maisha yako na kuacha yatima?
JIONI NJEMA SANA KWA WOTE PAMOJA DAIMA.

Monday, June 16, 2014

Thursday, June 12, 2014

NI MUHIMU KUJUA LUGHA MBALIMBALI HASA KUOMBA MAJI....LEO TUANGALIA NAMNA YA KUMBA MAJI KWA LUGHA ZA MAKABILA MBALIMBALI TANZANIA

Kina mama wakitoka kuteka maji kisimani

Ndugu wasomaji wa kibaraza hiki, leo nataka tujifunze namna ya kuomba maji kupitia lugha za makabila tofauti tofauti.Si mnajua jinsi maji yalivyo muhimu kwa sisi biadamu. Yaani pale unapokuwa na kiu sana na kuomba maji inabidi utumie lugha pekee ambayo unatakiwa kuwasiliana na lugha inayotumika  haya ebu tuangalie baadhi ya hizi hapa chini ..Tuanze na KINGONI
 
Kingoni: Nimwomba manji ga kunywa/Nitangatilai manji mlongo wangu=Naomba maji ya kunywa/naomba maji ya kunywa ndugu yangu
Kihehe:Ndisuka Ululenga= Naomba maji ya kunywa
Kibena : Ninyilika/ninyilika Magasi= Naomba maji ya kunywa

Kimatengo: Naa masi kuunywa= Naomba maji ya kunywa

Kinyawezi:Nalilomba minze kakunwa=Naomba maji ya kunywa

Kichaga: Ngikundi Mringa= Naomba maji ya kunywa
Kipare: Nighenja mazi ya kunwa=Nisaidie maji ya kunywa
Kipogoro: Nyagu  Mashi ga kulanda= Naomba maji ya kunywa

Kisukuma: Nalilomba Minzi agung´wa/Kifogo=  Naomba maji ya kunywa

Kimanda: Nisuka Masi ga  kunywa= Naomba maji ya kunywa

Kinyakyusa: Ngusumo amisi= Naomba maji ya kunywa

Kisimbiti: Ndasabha amanshe ghukunywa= Naomba maji ya kunywa

Kimasai:Njaaghe Ngare= Naomba maji ya kunywa

Kimeru:Ngitelewa Mringa= Naomba maji ya kunywa

Kijaluo:Miaa pi= Naomba maji ya kunywa
Kihaya: Ninshaba Amaizi= Naomba maji ya kunywa
Naona na wenzangu jazieni hapo maana Tanzania kuna makabila mengi sana .....Pamoja Daima!! 

Wednesday, June 11, 2014

TANZANIA INA MAKABILA MENGI SANA NA LEO NIMEONA TUUNGANE NA NDUGU ZETU WAHADZABE AMBAO WANAISHI KASKAZINI YA KATI YA TANZANIA

Najivuna sana kuwa mTANZANIA/MWAFRIKA... ebu angalia hapa furaha teleeee HAKUNA KULALA HATA KAMA HUJALA....MMMHH MARA nikaona wanaimba  nikaona niweke hapa pia hata kama sielewi nini wanaimba....ebu sikiliza na wewe.:-)


na hapa hakuna ngoma wala nini  yaani mpaka raha nimekumbuka mbali sana. Kama nilivyosema hapo juu ni kwamba Wahadzabe wanaishi kaskazini mwa Tanzania karibu na ziwa Eyasi jirani na Serengeti. Kabila hili idadi yao haizidi 1000... Na kati ya 300-400 huishi kwa kutegemea uwindaji.

Tuesday, June 10, 2014

HAYA NDIYO MAENDELEO YA BUSTANI YETU

 FIGIRI
 NA HAPA NA MBOGA YA MABOGA
Na mwaka huu nimeongeza na ZABIBU 
Karibuni sana.
Mavuno ya kwanza ..figiri hiyo nimekula mchana leo:-) sijui hapo kama kununu ningelipa shilingi ngapi?
 

Saturday, June 7, 2014

VYAKULYA NILIVYOZOEA TANGU UTOTO!!


Sasa ni  ni msimu wa viazi vitamu (mbatambata) au wengine wanasema makapa...basi nakwambia mikate, chapati, maandazi nk nimevitupilia mbali kabisa nipo na vyangu nilivyovizoea tangu utoto...mihogo, ndizi na magimbi :-) TUONANE TENA WAKATI MWINGINE ....!!!!!!  JUMAMOSI NJEMA WANDUGU.

Wednesday, June 4, 2014


Siyo kila dalili ya mwanaume kupenda ni ya kweli…!

Nimeisoma habari hii na nimeona sijasoma tu ila nimejifunza kitu na nimeona niiweke hapa ili wasioisoma wasome pale mpatapo wasaa na kuweza kupata mawili matatu hasa kwa wale wanaotarajia kuwa katika mahusiano...Nimeipata  kwa mzee wa UTAMBUZI. Haya karibuni
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kuna wakati ambapo, wanawake wanajikuta wakikabiliwa na swali la, je, mwanaume huyu ananipenda kweli? Hii hutokea pale anapokutana na mwanaume ambaye, huenda amevutiwa naye. Pengine mwanaume naye anaweza kuonesha kuvutiwa na mwanamke huyo.
Kwa hiyo, mwanamke hujiuliza kama akubali ombi la mwanaume huyo na kukubali kuzungumza naye au kuanzisha naye uhusiano, kama mwanaume atakuwa amezungumza naye kuhusu jambo hilo. ni kweli kwamba, kuna ugumu kwa mwanamke kujua hasa ni kwa namna gani anaweza kujua kwamba, huyo mwanaume amempenda kweli au hapana.
Kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kuwa ni dalili ya kumpenda mwanamke, lakini wakati huo huo vinaweza visiwe.
 
1. Hebu tuchukulie kwamba, mwanaume ameonesha kuwa na tabia tunazoziita nzuri. Labda amekumbuka kirahisi jina la mwanamke, ameonesha kuwa msikilizaji mzuri, ameonesha kuwa anajali kuhusu kinachosemwa na mwanamke, na amekuwa anamuuliza maswali kwa dhati na utulivu. Hapa mwanamke anaweza kuamini kwamba, huyu mwanaume anampenda. Lakini ukweli huenda ukawa ni kinyume chake. Inawezekana huyo mwanaume ni muungwana tu, na anaonesha tabia hizo kutokana na uungwana wake na siyo kutokana na kumpenda kimapenzi mwanamke.

2. Kuna watu ambao wana upendo, wamekomaa kihisia na wanajua kuhusiana vizuri na watu. Hii haina maana kwamba, kumwonesha mtu tabia hizo, kuna maana ya kumpenda au kumpenda sana mwanamke. Dalili hizi ni nzuri na inawezekana zikawa zinaonesha mwanaume kumpenda mwanamke, lakini mwanamke asilichukulie jambo hilo kwa namna hiyo.
3. Mwanaume anaweza kuonesha kuwa na udadisi kuhusu mwanamke kwa maana kwamba, kutaka kujua mambo yake, kumfuatilia au kuulizauliza kuhusu habari za mwanamke. Hii haina maana kwamba mwanaume amempenda kimapenzi. Inawezekana mwanaume akawa amevutiwa kimapenzi na mwanamke ndiyo maana akaonesha tabia hizo, lakini siyo lazima iwe hivyo. Kumbuka kwamba, mwanaume anaweza kuvutiwa na mazungumzo ya mwanamke, akavutiwa hata na namna alivyo usoni, hivyo akapenda kuzungumza naye lakini siyo kwa sababu anampenda.
4. Kuna wanaume ambao wana wake au wapenzi, lakini wanajisikia vizuri kusikiliza wanawake wengine au kujua tu habari za wanawake wengine, bila kuwa na haja ya kuanzisha uhusiano nao. Mwanaume anapompa mwanamke ‘ofa’ hasa ya chakula cha mchana au usiku, ni dalili ya wazi ya kuvutiwa naye. Hapa kuna uhakika mkubwa zaidi, labda tu kama mazungumzo yanayotajwa kufanywa wakati huo wa chakula yanafahamika, na ni ya shughuli maalum. Kwa hiyo ‘ofa’ ya chakula ni dalili nzuri na yenye uhakika. Lakini kuna jambo ambalo ni muhimu kwa mwanamke kulifahamu katika hali kama hii. Kuna wakati mwanaume kumpa ‘ofa’ mwanamke kwa chakula cha mchana au jioni, kunaweza kusiwe na maana ya moja kwa moja kwamba, uhusiano utaundwa. Inawezekana katika kutoka outing huko, mwanaume akaghairi. Kwa wengine huchukua muda hadi kuamua kuhusu kuunda uhusiano au hapana.
5. Hata mwanaume kuamua kumpeleka mwanamke kwa familia yao na kumtambulisha kama rafiki yake, ni hatua yenye kuonesha kwamba, mwanaume ameamua kumpenda mwanamke huyo. Lakini wakati mwingine hii inaweza ikawa ni janja yake kutaka tu kumthibitishia mwanamke ili amhadae vizuri, na wala hakuna maana ya uhusiano wa kudumu.
6. Kuzungumza kwa pamoja kuhusu masuala ya baadaye ya kiuhusiano, kama vile, idadi ya watoto na mambo mengine ambayo mara nyingi huzungumzwa na watu ambao tayari wako kwenye uhusiano ni dalili ya mwanaume kuvutiwa mwanamke. Lakini tatizo la jambo hili ni kwamba, kuzungumza masuala ya baadaye inaweza kuwa ni njia ya mwanaume kutaka kujisikia au kujua jinsi inavyokuwa katika mambo hayo. Inaweza kuwa pia ni njia yake ya kutaka kupima wanawake wanavyosema kuhusu masuala hayo. Lakini inaweza ikawa mwanaume huyo anatafuta kujua misimamo ya mwanamke huyo ili hatimaye afanye uamuzi. Kwa hiyo, bado haioneshi kuwa amevutiwa na kuamua tayari.
 
Mara nyingi wanawake hudanganywa na dalili fulani zinazooneshwa na wanaume wakati wanapoanza kuzoeana nao. Dalili hizi huwafanya kuamini kwamba, wanaume hao wamewapenda tayari, wakati siyo kweli. Kwa kuangalia baadhi ya dalili hizo kama nilivyozitaja, mwanamke anaweza kuwa makini wakati anapoanzisha uhusiano, ili asikurupuke na kujikuta amedanganyika. Ni kweli, kuna wakati ni dalili zinasema kweli, lakini kuna wakai zinadanganya kuhusu kupenda au kupendwa.
 
 

Tuesday, June 3, 2014

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MWANETU,KAKA, MJUKUU, RAFIKI YETU ERIK

HONGERA KUTIMIZA MIAKA 14 ERIK
Nachukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa nguvu sisi wazazi/walezi kwa kuweza kumlea mtoto/kijana Erik na leo ametimiza miaka kumi na nne/14. Hakika miaka inaenda  nikiwa kama mama naona kama ilikuwa juzi tu alizaliwa kijana huyu. Mwenyezi Mungu azidi kuwa naye katika masomo, na mengine yote afanyayo ili yawe mazuri. Ampe oyo wa upendo kwa walezi, ndugu jamaa na marafiki. Samahani nimeshindwa kupata picha yake yupo shule. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA ERIK!

Sunday, June 1, 2014

JUMAPILI IWE NJEMA KWA WOTE :- MAENDELEO YA BUSTANI YA KAPULYA

Jumapili ya leo nawaonyesheni bastani yangu nilipofikia. Mwaka huu mboga zangu zipo nyuma kidogo hadi leo tarehe 1/6 bado sijaonja. Hapa ni figiri

na hapa ni vitunguu  na vitunguu saumu