Sunday, December 15, 2013

TUMEPATWA NA MSIBA LUNDUSI/PERAMIHO KWA AKINA NGONYANI

PUMZIKA KWA AMANI BIBI NAPINGI
Hapa ilikuwa 2001 nyumbani Lundusi/Peramiho. Ni baba yangu mkubwa na mke wake na mjukuu wao. Lakini kwa vile baba yangu alilelewa na wao basi sisi watoto wake tumezoea tangu utoto kuwaita babu na bibi...hii ni historia fupi sana. Kwa hiyo leo asubihi mapema nimetumiwa taarifa kuwa bibi hatunaye tena. Amekuwa ameugua muda mrefu sasa. Bibi tutakukumbuka daima kwa yote mema na mazuri uliyotuachia. Sisi tulikupenda lakini Mungu anakupenda zaidi. Lihidimiwe jina lake. PUMZIKA KWA AMANI BIBI TUPO KATIKA MAOMBI.  MUNGU AIPE FAMILIA YA NGONYANI KOKOTE ILIPO NGUVU KWA KIPINDI HIKI KIGUMU.

14 comments:

Kuelekeautajiri. said...

Poleni sana kwa kumpoteza bibi yenu mpendwa,hilo ni fundisho kwetu sisi sote wanadamu kwamba, ni lazima iko siku tutaonja mauti.Mungu ampumzishe kwa Amani AMEN

Anonymous said...

Pole sana Yasinta na familia yote. Mungu awape faraja.

Yasinta Ngonyani said...

Kuelekeautsjiri! Ahsante ..ni fundisho kwa kweli. Wote tupo safari moja...

Usiye na jina ....ahsanta kwa pole

Kajunason said...

poleni sana shemeji yangu...

Mija Shija Sayi said...

Poleni sana Yasinta kwa msiba, Mungu awatie nguvu wanafamilia wote.

RIP bibi.

Yasinta Ngonyani said...

Shem kajuna...ahsante.

Mija...ahsante ndugu yangu. Tuzidi kumwombea bibi

EDNA said...

Pole sana kwa kumpoteza bibi, Mungu na ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante Edna..kwa kutupa moyo...naamini tupo pamoja katika sala

Anonymous said...

Pole da Yasinta! Mungu amlaze bibi mahali pema. By Salumu

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kaka Salumu...na kwa taarifa mazishi ni Jumatano...

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Poleni sana Da Yacinta Mungu atawapa faraja

Yasinta Ngonyani said...

Mwal. Mhango .. ahsante sana jindi mnavyotufariji ndivyo faraja inaongezeka. Mungu daina na milele...amina

Juma Thomas Nyumayo said...

Dada Yasinta poleni sana, nimechelewa kukupatia pole tokana na Computer yangu kuwa na shida. Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kaka Nyumayo..wala hujachelewa. Chilawu vihindika