
Kuondokana na hisia za mapenzi dhidi ya mpenzi uliyetokea kumpenda sana lakini mkaachana katika mazingira ambayo hukuyatarajia, si jambo rahisi na hasa kama wewe ndiye uliyeachwa. Unaweza kujiambia kwamba amekosea sana kukuacha na kamwe hatoweza kumpata mwanamke atakayempenda kama ulivyompenda wewe. Lakini kiukweli ndani ya moyo wako unampenda na kitendo cha kukuacha bado kinakuumiza na kukutesa. Inawezekana pia ukawa unatamani sana akurudie kwa sababu ulimpenda sana na unahisi upweke moyoni. Kwa mwanamke aliyeachwa, kuwaza hivyo ni jambo la kawaida kabisa, labda kama hukutokea kumpenda mwanaume huyo. Lakini kama miezi na miaka inapita na bado unaendelea kuwa na mawazo ya aina hiyo, basi hilo litakuwa ni tatizo, na hapa chini nitajaribu kueleza namna ya kuondokana na mawazo ya aina hiyo na kuendelea na maisha, kwani kuachwa na mpenzi sio mwisho wa dunia.
1.Unamuwaza muda wote Hili ni jambo la kawaida, lakini duh, kama unajikuta unamuwaza mpenzi aliyekuacha muda wote na kujikuta unashindwa kufanya mambo yako ya msingi kwa ustawi wa maisha yako, basi hilo ni tatizo ambalo linahitaji kupatiwa ufumbuzi. Ingawa waswahili husema “lisilo machoni, halipo moyoni,” lakini mimi nasema sio kila lisilo machoni halipo moyoni, kwa swala la mapenzi nadhani iko hivyo. Ukweli ni kwamba hujui yuko wapi, anafanya nini au yuko na nani na hapo ndipo utakapojikuta ukitafuta picha mlizopiga mkiwa pamoja wakati wa kilele cha mapenzi yenu, na wakati mwingine unaweza kusikia wimbo fulani ambao aliupenda sana ukakukumbusha tukio lililowakuta mkiwa pamoja ambalo linahusiana na wimbo huo. Kwa kifupi ni kwamba, ni jambo la kawaida sana kumkumbuka mpenzi mliyeachana mara kwa mara baada ya kuachana. Lakini kama mawazo hayo yanaonekana kukuumiza na kukupotezea muda basi jua kwamba, jambo hilo linaweza kukuletea matatizo makubwa sana kiafya. Namna gani utaondokana na tatizo hili: Muda ni nyenzo muhimu sana katika kuponya. Kama unashindwa kupata suluhu ya namna ya kuondokana na mawazo ya huyo mpenzi mliyeachana naye, basi jipe muda, kwani kwa kujipa muda zaidi unajipa nafasi ya kuponya majeraha ambayo yanaonekana kukutesa. Kwa jinsi muda unavyochukua nafasi ndivyo unavyomudu kusahau na ndio maana waswahili husema yaliyopita si ndwele tugange yajayo Endelea kusoma zaidi HAPAhttp://kaluse.blogspot.se/2013/07/mwanamke-je-bado-una-hisia-za-kumpenda.html JUMATANO NJEMA SANA WOTE!!!