Thursday, February 7, 2013

ULIJUA KWAMBA SABABU YA KUWAITA JINA "WAZUNGU" LILITOKANA NA-----

Kuna mzungu aliniuliza maana ya neno mzungu. Nikamwambia haihusiani kabisa na rangi bali inatokana na wale weupe wa kwanza waliofika Afrika na hawakujua wanakwenda wapi, hivyo walikuwa wanazunguka ovyo! Kuna stori nilisimuliwa nikiwa mdogo, kuna kundi la wazungu walifika kijijini. Walikaribishwa vizuri na Chifu wakaondoka. Baada ya wiki mbili wazungu hao hao wakarudi pale kijijini. Chikfu kauliza, "Jamani, hao si ndo tuliwaaga majuzi!" Mzungu kashangaa hakufika popote bali anatembea katika mduara!
Imenukuliwa kutoka kwa Da’Chemi kwenye
blogu yake - “SwahiliTime”.

5 comments:

Interestedtips said...

ila nakumbuka nilihadithiwa kuwa Mzungu lilitokana na kabila moja ni neno la mshangao, walikuwa wanawashangaa jinsi walivyo weupe kwa neno Mzungu.....ndo likwa hivyo hadi leo

Yasinta Ngonyani said...

Ester..lakini kama alishangaa uepe wake kwanini wazungu na sio weupe?
Unajua nimekuwa nikijiuliza sana swali hili kwanini waitwa wazungu na sisi tuitwa majina tofauti weusi na waafrika?...

Anonymous said...

kihaya"omujungu,omwela,omtuku,rutuku

ray njau said...

Nakumbuka stori moja rafiki yangu akisema waafrika tukitatizka kidogo tuwageukia wazungu ili watusaidie na jina mzungu ukiondoa hiyo herufi z unapata jina lingine.

emuthree said...

Ukuchunguza sana, majina haya unaweza kupata maana nyingi, kwani kuna mmoja alisema jina `waafrika,' lilikuwa la kama kukashifu,...`afriti'...kitu kama hicho, na wengine wakasema linatokana na `ufukara' lakini enzi hizo nijuavyo mimi Afrika ilikuwa tajiri, wagunduzi wa pesa, kulikuwa na madini,....nenda huko Misri wasomi wa kubwa....kwahiyo hayo majina sizani kuwa ndivyo kama wanavyotafsiri sasa, ila kweli wazungu, inawezekana inatokana na `kuzunguka'....Tupo pamoja mpendwa