Saturday, February 23, 2013

MAISHA NA MAFANIKIO YATIMIZA MIAKA MITANO /5 LEO :- 23/2/2008-23/2/2013!!!!

Kama mchezo nilizanza kublog  Jumamosi tarehe 23/2/2008 na leo ni Jumamosi 23/2/2013 imefika mika mitano..(5) hapa ni siku ya kwanza nilivyoanza ... bonyeza hapa Hakika Maisha na Mafanikio imetoka mbali ..JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE...KAPULYA

15 comments:

Anonymous said...

Hongera sana Yasinta. Ila nadhani kuna kosa kidogo nikihesabu ni miaka mitano na sio sita!kama ulivyoandika,kutoka Feb.2008 mpaka Feb.2013. Nakutakia kilala heri katika kublog.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana usiye na jina ....inategemea unaanza kuhesabu vipi ukianza siku na mwaka 2008 basi itakuwa sita na ukianza mwaka ufuatayo basi itakuwa mitano...Ahsante kwa yote

Shalom said...

Hongera dada yasnta mbona inakuwa miaka mitano na sio sita

Yasinta Ngonyani said...

Haya jamani naona hesabu si somo langu ngoja nibadili ..Ahsanteni hii ndiyo raha ya kublog na raha ya kuwa wazi..NAPENDA

Shalom said...

Haya dada hongera sana na mungu akutangulie uzidi kusonga mbele.

Anonymous said...

Hongera sister Yasinta. Nakutakia mafanikio wewe pamoja na familia yako na blog yako izidi kung'ara na kumulikia njia wana jamii wote! By Salumu.

Anonymous said...

Tunashukuru umebadilisha, mana ukicheki mwaka jana mwezi huu uliandika ilitimiza miaka minne na hesabu ilikuwa vema, naona mwaka huu umeongeza zaidi, au ndio unazeeka? Umri umeenda dada na ni kawaida tu kukosea. Maisha na mafanikio mema.

sam mbogo said...

Au madeni yamezidi mpaka mahesabu hayaendi vizuri? usikonde hongera sana kwa kublog .unatupa nafasi nasisi wasomaji kujifunza mengi ndani ya hii blog yako.haya nakutakia lizombe njema katika kusherehekea blog yako.ndimi wako mtiifu nilie chini ya miguu yako kwa unyenyekevu na sema asante!! kaka s.

sam mbogo said...

Au madeni yamezidi mpaka mahesabu hayaendi vizuri? usikonde hongera sana kwa kublog .unatupa nafasi nasisi wasomaji kujifunza mengi ndani ya hii blog yako.haya nakutakia lizombe njema katika kusherehekea blog yako.ndimi wako mtiifu nilie chini ya miguu yako kwa unyenyekevu na sema asante!! kaka s.

Sm said...

Ww kaka s unafanya nn chini ya miguu ya dada ako usije ukamchungulia bure.

Yasinta Ngonyani said...

shalom! ahsante sana na karibu sana sana hapa kibarazani:-)

Salum! Asante sana na karibu sana.
Usiye na jina wa 4:24 umenichekesha kweli..Inawezekena ni uzee kweli:-)
Kaka Sam!..tupo pamoja ...nawe umenichekesha na nikanza kuangalia chini ya miguu yangu ila sijakuona..LOL

Sm!..Nadhani kaka S atakuambia maana yake hata mie nasubiri..-:)
AHSANTEN WOTE KWA KUWA NAMI KATIKA SIKU HII.

Shalom said...

Asante dada nashukuru kwa kunikaribisha japo nilisahau kupiga hodi. Jamani hodi kibarazani naomba mnipokee

Yasinta Ngonyani said...

Shalom! usiwe na shaka ushakapokelewa tena kwa mikono miwili.KARIBU SANA ..PAMOJA DAIMA

Shalom said...

Ahsante nimeshakaribi wangu.

ray njau said...

Kila kuendako hisani hakurudi nuksani bali shukrani.Blogu ni divisheni yenye mashiko katika tasnia ya habari na mawasiliano kwa ummma.Blogu ya maisha na mafanikio imeendelea kutimiza hayo yaliyotajwa hapo juu na matarajio yetu ni kuwa mgema asifiwa siyo lazima alitie tembo maji.Yasinta ni matarajio ya wadau wa kibaraza chako kuwa utaendelea kuwapatia kile kilicho bora kabisa bila ya kutafuna maneno wala kupepesa macho.