Tuesday, February 5, 2013

KWA WALE WANYWAJI WA KAHAWA SASA KUNA YA KIKOMBE KIMOJA KIMOJA...MAANA KILA MARA NAONGELEA KUHUSU CHAI KWA VILE MIMI NI MPENZI WA CHAI...

 

 
KAHAWA KUTOKA TANZANIA TANICA CAFE NA AFRICAFE KWA KIKOMBE KIMOJA
Hata hivyo sikuweza kuacha bila kusema kuhusu chai....kwa kikombe kimoja kimoja pia. Haya karibuni mchagua ni ipi ikufaayo..mimi nachagua chai:-)

13 comments:

ray njau said...

"Kahawa na chai ni mapacha wa mama mmoja lakini baba zao ni tofauti."
Changamka na daima burudika na bidhaa kutoka Tanzania.

Rachel Siwa said...

Africafe..dada KADALA...duhhh harufu mpaka hapa naipata..hizo nyingine sizijui/sijawahi kuonja.....

Nifungulie mlango baathii

Mija Shija Sayi said...

Mapacha wa mama mmoja lakini baba tofauti... Nimeitafakari nikagundua mambo yote yanawezekana chini ya jua lakini hili nina wasiwasi...

Nimeipenda sana hii...@Ray Njau

ray njau said...

Wasiwasi wako ni changamoto tosha kwetu.........@Mija

Anonymous said...



Haѵe a looκ at my site payday loans
Also see my website :: payday loan online

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! hapa hata mimi nimejiuliza sana ni mapacha kivipi? kwa kuchangamsha mwili au???

KACHIKI! we ingia tu mlongo mbona upo wazi ....karibu je watumia sukari na madhiwa??

Mija! hakuna kisichowezekana..si unakumbuka tulikuwa tukisema chai ya kahawa..sijui ndo hilo kaka Ray analisema kuhusu huo umapacha...???

Ray:-)

ray njau said...

Kahawa na chai kila kimoja kwa nafasi yake chaweza kuburudisha mhitaji.

Yasinta Ngonyani said...

kaka Ray! Je unaweza kufafanua ni mapacha kwa aina gani?

ray njau said...

Ustadi wa Kutayarisha Kahawa ya Spreso

Kahawa imekuwa moja kati ya vinywaji vinavyopendwa zaidi ulimwenguni kwa kuwa watu wanakunywa vikombe bilioni kadhaa vya kahawa kila mwaka.

KWA wanywaji fulani wa kahawa, spreso ni “kahawa murua sana,” linasema jarida Scientific American, “kwa kuwa inatayarishwa kwa njia ya pekee inayotokeza vizuri ladha yake.” Inatayarishwa kwa kupitisha kwa nguvu mvuke au maji moto kwenye kahawa iliyosagwa hadi ikawa laini kabisa.

Mtaalamu mmoja wa kutayarisha kahawa alimwambia hivi mwandishi wa Amkeni!: “Watu wanaofurahia kunywa spreso iliyotayarishwa kwenye mikahawa wanataka kuitengeneza nyumbani kwao.” Kwa sasa kuna mashini za kutengenezea spreso nyumbani. Kwa sababu hiyo, watu wengi zaidi wanakunywa spreso iliyotengenezewa nyumbani.

Je, wewe ni mnywaji wa kahawa? Je, ungependa kujifunza kupika spreso? Unahitaji kufanya nini ili kutayarisha kikombe murua cha kahawa? Mwandishi wa Amkeni! aliwauliza swali hilo John na baba yake, Gerardo ambao ni magwiji wa kukaanga kahawa, wanaoishi huko Sydney, Australia.

Mbinu ya Kutayarisha Kahawa

“Kati ya mbinu zote za kutayarisha kahawa, spreso ndiyo mbinu rahisi zaidi lakini wakati uleule ngumu zaidi,” anaeleza John. Ili mtu atayarishe spreso nzuri zaidi anahitaji kufanya mambo matatu kwa usawaziko kabisa: kusaga buni (1), kushindilia kahawa iliyosagwa ndani ya kikapu cha kuchujia kilicho ndani ya mashini ya kupika kahawa (2), na kumwaga kahawa yenyewe (3). “Ni muhimu sana kusaga kahawa kwa njia inayofaa,” anasema John. “Kahawa ikisagwa kidogo, spreso itakuwa majimaji sana. Ikisagwa sana, kahawa itakuwa na ladha chungu na iliyounguzwa. Katika visa vyote, spreso inapomwagwa, povu linalotanda juu yake litaonyesha ikiwa mafuta yaliyo ndani ya buni yametolewa kwa njia inayofaa.”

Baada ya kusaga buni chache, John anatumia kifaa fulani kuzishindilia ndani ya kikapu cha kuchujia na hivyo zinakuwa laini. Kisha anaingiza kikapu ndani ya mashini na kuiwasha. Kahawa moto inaanza kutoka. Mara moja, John anagundua kwamba buni hazikusagwa vya kutosha. “Mara nyingi unahitaji kujaribu mara kadhaa ili utayarishe spreso nzuri zaidi,” anasema. “Hebu tujaribu tena tukitumia buni zilizosagwa sana. Pia, tutashindilia buni zaidi ili kahawa itoke polepole.”

John anafanya marekebisho hayo na kuwasha mashini tena. Kahawa yenye povu nzito sasa inatoka ikiwa na uzito unaofanana na wa asali yenye joto. Harufu nzuri inapotanda hewani, tabasamu la John linaonyesha kwamba hiyo kahawa ni murua. “Ni muhimu sana tuache kumimina kahawa wakati rangi yake nzito inapoanza kuisha,” anasema. Hiyo inachukua muda usiozidi sekunde 30. “Ukiendelea kumwaga kahawa zaidi,” anasema, “unapata kahawa yenye ladha chungu na kafeini nyingi zaidi.”

“Nafikiri tumetayarisha spreso bora zaidi,” anasema John, akitazama povu nzito, laini, na iliyoshikana kabisa. “Je, ungependa kikombe cha kahawa?”

Watu fulani wanaopenda sana kahawa halisi, hawapendi kuongeza chochote isipokuwa tu labda sukari kidogo. Hata hivyo, wengine huongeza maziwa moto ili kutokeza cappuccino, latte, au aina nyingine za spreso. “Leo, zaidi ya asilimia 90 ya kahawa inayouzwa ni ile iliyochanganywa na maziwa,” linasema gazeti Fresh Cup Magazine.*

Kuwa na mazungumzo mazuri huku mkifurahia kunywa chai au kahawa, ikitegemea unapenda kunywa nini, ni moja kati ya mambo yanayofurahisha zaidi maishani. “Vinywaji vyenye ladha nzuri vinawaunganisha watu,” anasema John. “Huenda hilo ndilo jambo linalopendeza zaidi kuhusu vinywaji hivyo!”

ray njau said...

Chai Ilitoka Wapi?
Chai ambayo huitwa Camellia sinensis, hukua porini nchini China na Japani, na miti yake hukua kufikia kimo cha meta tisa hivi. Mmea maridadi wenye majani ya rangi ya kijani-kibichi yanayong’aa na maua ya waridi, meupe au mekundu unaoitwa camellia (Camellia japonicus) ni wa jamii ileile ya chai. Kwa kweli, Wachina huuita mmea huo cha hua, yaani, “ua la chai.”
Lakini chai tunayojua hutoka wapi? Kulingana na The Encyclopedia Americana, chai inatajwa kwa mara ya kwanza katika kitabu kinachoeleza kuhusu maisha ya ofisa mmoja Mchina aliyekufa mwaka wa 273 W.K., ingawa inadhaniwa kwamba chai ndio mmea uliotajwa katika kitabu kilichohaririwa na Confucius, aliyeishi yapata mwaka wa 551 K.W.K. hadi 479 K.W.K. Chai ilitajwa mara ya kwanza katika Kiingereza na R. Wickham, mwakilishi wa Kampuni ya East India ya Uingereza, mwaka wa 1615. Katikati ya karne ya 18, Thomas Garway, mmiliki wa mkahawa mmoja huko London ambao baadaye uliitwa Garraway, alinunua chai nyingi.
Chai hukuzwa katika sehemu nyingi ulimwenguni. Waholanzi walipeleka chai huko Java, katika mwaka wa 1826, nao Waingereza wanaojulikana kuwa wapenzi wa chai, wakaipeleka huko India yapata mwaka wa 1836. Kisha katika miaka ya 1870, chai ilikuzwa badala ya kahawa baada ya miti ya kahawa ya Sri Lanka kuharibiwa na kuvu.
Mkahawa wa Chai
Hatujawahi kutembelea mkahawa wa chai, hivyo tunaamua kutembelea mkahawa mmoja. Mikahawa fulani ina bustani maridadi ambazo wateja hufurahia wanapokunywa chai. Mikahawa mingine iko milimani, na mandhari nzuri hufanya mtu afurahie hata zaidi kunywa chai.
Tunaamua kwenda kwenye mojawapo ya milima inayozunguka Taipei na kunywa chai katika mkahawa wenye kuvutia ulio na mazingira yanayofanana sana na ya China. Orofa ya pili ina vijito vya maji vyenye samaki wengi wanaoitwa goldfish na inatubidi tukanyage mawe machache yaliyo ndani ya vijito hivyo ili tuingie ndani ya chumba kidogo ambako tutakunywa chai yetu. Tunaweza kunywa chai pamoja na keki tamu zilizopikwa kwa maharagwe (maharagwe mekundu au meupe yaliyopondwa pamoja na sukari), mbegu za tikiti-maji, tofu iliyokaushwa (maziwa ya maharagwe), keki za mchele, au matunda yaliyokaushwa au yaliyotiwa siki na chumvi. Tunaamua kula mbegu za tikiti-maji, embe lililokaushwa, na plamu zilizochachishwa kwa majani-chai. Utamu wa vyakula hivyo unapatana na ladha ya chai. Tunapotiliwa chai, tunawazia jinsi Wachina wa kale walivyokunywa chai.
Manufaa ya Kunywa Chai
Kulingana na Wachina wengi, chakula humeng’enywa haraka zaidi mtu anapokunywa chai. Inadaiwa kwamba kwa kiwango fulani jambo hilo husaidia mtu asiongeze uzito. Ikiwa ni kweli, basi chai ina manufaa kwelikweli! Hivi karibuni, watafiti wamedai pia kwamba chai ya kijani-kibichi inaweza kupunguza hatari za kupatwa na kansa. Manufaa nyingine ya kunywa chai ya oolong na ya kijani-kibichi ni kwamba aina hizo humwacha mnywaji akiwa na ladha tamu na yenye kupendeza kinywani.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Ahsante kwa utafiti wake wengi tumefaidika..hii ndiyo safi kutonyimana elimu...

ray njau said...

Hapa ni kibaraza cha maisha na mafanikio, elimu kwanza.

Anonymous said...

Ce savant chimiste a base son opinion sur les viagra france, sur de la potasse ou sur la soude chautiees a la, autores de las Meniorias que se inserten en los, cialis en farmacias, que esas instituciones se asumen como las, mai osservato nulla di simile. comprare viagra, e composta di elementi perpendicolari eiterige und zahe Flussigkeit cialis bestellen, und alle Reste der Schwefelsaure wegzubringen,