Monday, February 11, 2013

JUMATATU HII TUANZA HIVI:-DHULUMA KWA WATOTO YATIMA...


Je huu kweli ni uungwana... tutafakari pamoja..kila la kheri!!

4 comments:

ray njau said...

Haki ya Yehova Inachangamsha Moyo
===================================
Haki ya Yehova si sifa inayochukiza, bali ni sifa ya kupendeza inayotuvuta kwake. Biblia inaeleza waziwazi kwamba haki au uadilifu wa Yehova unaambatana na huruma. Hebu tuchunguze baadhi ya njia za Yehova za haki zinazochangamsha moyo.
Haki kamilifu ya Yehova humchochea kuonyesha uaminifu na ushikamanifu kwa watumishi wake. Mtunga-zaburi Daudi alipata kuelewa na kuthamini wonyesho huo wa haki ya Yehova maishani mwake. Daudi alifikia mkataa gani kutokana na mambo yaliyompata na yale aliyojifunza kuhusu njia za Yehova za kufanya mambo? Alitangaza hivi: “BWANA hupenda haki, wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele.” (Zaburi 37:28) Ahadi hiyo inatia moyo kama nini! Mungu wetu hatawaacha kamwe wale walio waaminifu kwake. Kwa hiyo, tunaweza kuwa na hakika kwamba atatutunza kwa upendo na hatatuacha kamwe. Jambo hilo ni hakika kwa sababu yeye ni mwenye haki!—Mithali 2:7, 8
14 Mungu huzingatia mahitaji ya wale wanaotaabika kwa sababu yeye ni mwenye haki. Sheria ambayo Yehova aliwapa Waisraeli inaonyesha kwamba anawajali wanaotaabika. Kwa mfano, Sheria ilitaja mipango ya pekee ya kuhakikisha kwamba mayatima na wajane walitunzwa. (Kumbukumbu la Torati 24:17-21) Huku akitambua magumu ambayo yangekumba familia hizo, Yehova aliwajali akiwa Hakimu na Mlinzi wao, ambaye ‘anamfanyia yatima na mjane hukumu ya haki.’ (Kumbukumbu la Torati 10:18; Zaburi 68:5) Yehova aliwaonya Waisraeli kwamba endapo wangewatesa wanawake na watoto hao wasio na msaidizi, angesikia kilio chao pasina shaka yoyote. Alisema: “Hasira yangu itawaka moto.” (Kutoka 22:22-24) Ijapokuwa hasira si mojawapo ya sifa kuu za Yehova, hasira yake adilifu huwaka anapoona watu wa hali ya chini na wanyonge wakionewa kimakusudi.—Zaburi 103:6
15 Yehova pia anatuhakikishia kwamba ‘hapendelei nyuso za watu, wala hakubali rushwa.’ (Kumbukumbu la Torati 10:17) Yehova si kama wanadamu wengi mashuhuri na wenye mamlaka ambao huangalia utajiri au sura ya mtu. Hana ubaguzi wala upendeleo wowote. Fikiria uthibitisho huu wa pekee ambao unaonyesha kwamba Yehova hana upendeleo. Hakuwapa watu wachache tu wenye elimu nafasi ya kuwa waabudu wake wa kweli wenye tumaini la kuishi milele. Badala yake, “katika kila taifa mtu ambaye humhofu na kutenda uadilifu akubalika kwake.” (Matendo 10:34, 35) Watu wote wanaweza kuwa na tumaini hilo zuri ajabu bila kujali wadhifa wao katika jamii, rangi yao, au nchi wanamoishi. Je, huo si uthibitisho bora kabisa wa haki ya kweli?

emuthree said...

Hiyo sio hekima kabisa

sam mbogo said...

Hakika chozi limenitoka, nimeudhunika sana na kusikitika sana kutokana na igizo/ mchezo hili hakika nimeguswa vibaya mno yaani sijuwi ni semeje.hi ndo hali halisi ya maisha ya waliowengi inapotokea swala mirathi dhuluma huwa mbele. jamaa wamejitahidi sana kufikisha ujmbe kwa kweli wamefanikiwa naujumbe umefika. haki,na sheria na taratibu katika swala zima la mirathi ni muhimu kuzingatiwa.mitazamo ya walio wengi pindi ndugu awe baba/mama/kaka/dada na hata rafiki anapo fariki mawazo na mitazamo huwa kama ya hao watu tulio waona kwenye igizo/mchezo hawa wa jali wale watoto walio achwa na wazazi wao.serikali inabidi itamke hadharani haki na wajibu katika mirathi,kisheria. dah nimeguswa sana.kaka s

Yasinta Ngonyani said...

ndugu zangu mliotangulia nakubaliana naye asilia zote huu si uugwana kabisa nimeangalia hii filamu huku machozi yakitiririka...