Tuesday, December 15, 2015

UJENZI WA NYUMBA ....MKIONA NASUASUA BASI MJUE NIPO KATIKA ZOEZI LA UJENZI WA NYUMBA.....MBINGA

 HAPA NI MSINGI WA NYUMBA INAANZA ...NI SEHAMU YA MABANDA NIMEANZA
 BAADA YA SIKU KADHAA ILIFIKIA HAPA NI  KAMA MUONAVYO NI MATOFALI YA KUCHOMA
 HAPA NYUMBA IPO TAYARI NA SASA KENCHI ZINAPANDISHWA....NA NI MWONEKANO KWA NYUMA,,
 HAPA WAWEZA KUONA KENCHI ZIMEKWISHA PANDISHWA NA NI MWONEKANO KWA MBELE......
HAPA TAYARI TUMEEZEKA ...KAMA NILIVYOSEMA NIMEANZA NA MABADA  NA NI NUSU TU YA SAFARI........PICHA ZAIDI ZITAKUJA:-) KILA LA KHERI  PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU.

9 comments:

Anonymous said...

Hongera sana kwa ujenzi dads...mbinga hiyoooooooooooooooooo
Ndio mana upo kimya kimya Fulani hivi. Je upo Tz au unajenga kwa remote dada? Ubarikiwe sana.

Mbele said...

Safi sana. Ninavyoona picha hizi, ninawazia kuharakisha ustaafu wangu nikaishi sehemu hiyo. Je, uko Mbinga wakati huu?

Anonymous said...

Mabanda una maanisha nini? Nipe mojawapo mie nikaishi huko kwenye banda lako. Ila sijaelewa mabanda, nieleweshe? Nimezoea kusema mabanda ya kuku! Ila hayo sio naona ni nyumba, nisaidie nielewe.

Anonymous said...

Hongera da Yasinta. Imechukua muda gani kuanzia msingi mpaka kuezeka? By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu zangu kama nilivyosema nitakuwa napoteapotea...Usiye na jina 5.48 ahsante sana kwa mchango wako. Unajua wakati mwingine unaweza kufanya kitu ikiwa upo katika sehamu ile kimawazo na akili na sio kimwili:-) najua umenielewa...

Prof. Mbele..nakuelewa jinsi unavyojisikia...Na jibu kwako pia ni kama nilivyompa aliyetangulia hapo juu ..

Usiye na jina wa 11.31 PM.. Mabanda sijajua ni sehemu zote Tanzania huwa wana mjengo huo wa nyumba ni kwamba watu huwa wana mazoea ya kujenga nyumba kubwa (self conterned) na pia kwa pembeni unaeza kujenga vyumba viwili- vitatu kuzunguka nyumba..natumaini umenielewa...

Kaka Salumu! Kwanza za siku? Pili Ahsante kwa pongezi ninajipigapiga hivyo hivyo..Na mwisho ni kwamba imechukua kama miezi miwili na nusu hivi...

Penina Simon said...

Hongera,
Hakika wewe ni jembe

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante dada najikokote....nichukue nafasi hii kukutakia kheri ya Krismasi!

Nicky Mwangoka said...

hongera sana dada

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kaka Nicky!