Monday, December 28, 2015

PALE HALI YA HEWA INAPOBADILIKA...LEO ASUBUHI ILIVYOKUWA/DET SNÖAR!

Mila na desturi au nisema ni mazoea ya nchi nyingi za Ughaibuni/ulaya siku ya Krismas kuwa na thaluji yaani kweupe huko nje lakini krismas hii haikuwa hivi hasa Swedan badala yake theluji imeanguka jana 27/12 mpaka leo 28/12 na kamera ya maisha na mafanikio imebahatika kupata picha hizi kama uonavyo...
Wakati mwingine ni safi kuacha gari na baiskeli na hapo ndipo utakapofaidi mambo angalia hii picha  hapa nilikuwa nikitoka mazoezi ya asubuhi:-) pia ni vizuri kutembea/kimbia na kamera......

 Basi nikalipokaona hako kajua nikaanza kuimba kala kawimbo ka mchakamchaka ....Jua lile...nikabadili nikaanza kuimba Idiamini akifa mimi siwezi kulia......Kama nilivypsema Ujenzi unabana ila leo nimepata kamuda...na pia sasa nitapumzika kidogo na ujenzi mpaka huu mwaka uishe ndo tutaendelea...Bado siku 4-3½ hivi kuufikia mwaka  mpya...TUOMBEANA  ILI TUWEZE KUUONA ...NI MIMI KAPULYA WENU!!


3 comments:

Anonymous said...

Kwa kweli mwaka huu baridi haijawa kali kiasi hicho. hii inadhihirisha mabadiliko ya "Tabia nchi" kama wasemavyo. By Salumu.

Anonymous said...

Hongereni sana na snow! mana msipoiona mnapooza huko majuu! hahaha, si unajua mazoea. Mbona sijakuona kwenye huzo picha mana umesema unakimbia ila nimejaribu kucheki sijamuona yasinta?

Heri ya Christmass na mwaka mpya 2016 mpendwa wetu na dada.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu ni kweli "tabia nchi" ila hata hivyo watu hatuna shukrani. ...sasa wanalalamika wanataka joto/jua.

Usiye na jina wa 4.01 Pm...nilishindwa kujipiga picha huku nikikimbia. ..xmas njema kwako pia na mwaka mpya 2016 unapenda...Nachukua hii nafasi kukushukuruni wote kwa michango yenu.