Thursday, February 27, 2014

MAISHA NA MAFANIKIO LEO NA UJUMBE UFUATAO:-......!!!

Ishi maisha rahisi,  Onyesha mapendo/upendo kwa ukarimu wa kweli,  Onyesha upendo kwa undani na kujali, Ongea kwa huruma,  Mengine yote mwachie Mungu.
KWA UJUMBE HUU NAPENDA KUWATAKIENI WOTE SIKU NJEMA SANA!

5 comments:

Rachel Siwa said...

Asante kwa ujumbe mzuri...Nawe uwe na wakati mwema pamoja na familia.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante KACHIKI WA MIMI...NAWE NA FAMILIA PIA.

Emmanuel Mhagama said...

Mimi hiyo picha tu. Nahisi kama ukiiangalia sana hata kama ulikuwa na majonzi unaweza kufarijika ghafla.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Shukrani kwa falsafa hii ingawa siyo kila kuongea kwa huruma kuna heri. Matapeli wengi hasa wa kidini siku hizi wanaongea kwa huruma lakini wanaumiza wengi. Wapo hata wanasiasa wanaosifika kwa kutabasamu na kucheka cheka lakini ni wakatili Mungu anajua. Wapo wanaowahadaa wenzao kuwa wanawapenda tena kwa lugha tamu na kuwaharibia maisha. Wasichana wa shule za Msingi ambao rais Jakaya Kikwete alisema wanapata mimba tokana na kiherehere chao wanalijua hili vizuri. Wakati wa kampeni wanasiasa huongea kama wachungaji na mashemasi. Baada ya kupata walichotaka huongeaje? Anyways, ni uoni wangu tu khususian ana chui kwenye ngozi ya kondoo hasa usawa huu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhagama! ni kweli kabisa na hii ndiyo sababu kuu:-)

Kaka Mwal.Mhango..hakika usemacho ni kwelikabisa hasa hawa wanasiasa hii tabia sijui itaisha lini na kwa nini wasicheka kila wakati si wakati tu wanapohitaji kupata kitu.
Nimesikitika hii ya Kikwete kusema wasichana wanapata mimba kwa sababu ya kiherehere... Natamani kama ningegombea ubunge na nifanye kitu kuhusu jambo hili hasa hili kuhusu wasichana---ipo siku Mungu mkubwa.