Wednesday, February 12, 2014

MAISHA NA MAFANIKIO ILIVYOWAANDALIA JIKONI JANA JIONI: SUPU YA VIAZI!!!!

 Hapa ni maandalizi yz upikaji wa supu ya viazi, ambayo Kapulya mwenyewe kaivumbua. Na katika supu hii kuna:- Viazi 8, kitunguu 1, vipande viwili vya kitunguu saumu, tangawizi kiasi utakacho mimi natumia kama cm 2 hivi, pilipi kidogo hasa kama hupendi ukali sana na kama una watoto wadodo, Chumvi kijiko kimoja cha sukari (msk), binzari kijiko kimoja cha sukari (msk), mafuta vijiko viwili vya mezani, Paketi moja ya nyanya au nyanya freshi 3, maji lita moja na bila kusahau sufuria kubwa na mwiko wa kukorogea.
Ni  hivi: Menya viazi, kisha menya kitunguu na kitunguu saumu...Katakata viazi vipande vidogovidogo, na halafu vichemshe kwa dakika 5, weka pembeni. Katakata kitunguu, unaweza kutakata kitunguu saumu na tangawizi pia vipande vidogovidogo sana lakini safi zaidi kama una kakinu basi ponda ponda pamoja na pilipili pia chumvi kidogo kwa kurahisisha. Weka sufuria katika jiko na moto mkali kidogo na weka mafuta. Kaanga vitunguu, kitunguu saumu, tangawizi na pilipili mpaka vinakuwa laini ila visiungue. Weka binzari pia nyanya,  kama unatumia pakati weka nusu, ache vitokote dakika kama 5 hivi. Baada ya hapo chukua viazi na uchanganye kwenye chachandu na yale maji ulochemshia  na acha vichemke tena dakika 5 zaidi ila kwa moto kidogo sana. Na mwisho wake chakula tayari imechukua dakika 15 kupika na maandalizi kama nusu saa.

Na hapa unaona matokeo yake ...Ni Supu tamu na kama una haraka ni chapuchapu na ninauhakika watoto wako watapenda pia kwani wangu wanapenda sana. Kama katika picha unaweza kula kama ilivyo au na kipande cha mkate kama nilivyofanya mimi jana na pia ni kama mpenzi wa mikate. Kinywaji hapa ni maji ...ila ni chagua la mtu. Nakutakia MAJARIBIO MEMA..KWANI NAJUA kuna wadada na wakaka watajaribu tu:-) KILA LA KHERI NA NAJUA MTAIPENDA HII SUPU.

11 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Mmmmhh tamu sana,Asante kwa mapishi KADALA.

Anonymous said...

Hivi Dada Yasinta huna housegirl? manake sijawahi kumwona! Kama huna nashindwa kuamini maanake mwenzio ile baada ya kuoa tu wakati mke wangu bado hana kazi akanidai housegirl ile bado najiuliza sijatoa jibu nikastukia naletewa nianze kumlipa. Lakini nadhani alikuwa sahihi, "Mwanamke ni pambo la nyumba"

Anonymous said...

Da Yasinta, asante kutujuza supu ya viazi, kwa kweli hii ni nzuri sana kwa mabachala ambao wanafanya kazi na hawana mda wa kutengeneza chakula, na inaonekana tamu mno. By Salumu.

Manka said...

Dada yangu Yasinta asante kwa recipe,mie nitaijaribu kesho jioni.Asante kwa ku-share.

Yasinta Ngonyani said...

KACHIKI! Ni kweli ni tamu sana na rahisi jaribu tu...

Usiye na jina wa 3.34PM! HAPANA sina, sijawahi kuwa naye na sitegemei kuwa naye....

Kaka Salumu..yaani hakuna kula vyakula vingine vya haraka haraka. We jaribu ni tamu na ukisha jaribu hutapenda kuacha kupika kila mara:-)

Maka..ulipotea karibu tena ndugu yangu ..Kila la kheri hiyo kesho najua utaipenda:-)

Ester Ulaya said...

NITAYAJARIBU MAPISHI HAYA....INAONEKANA TAMUUU

Yasinta Ngonyani said...

Mama A! Jaribu na najua utapenda hata A pia.

Serina said...

Det ska jag prova... snabbt och enkelt! yaonekana supu nzuri ya kuondoa baridi :D

Yasinta Ngonyani said...

Serina! Prova det ...kommer nog att tycka om. ..ni kweli kabisa ya kuondoa baridi...:-D

Anonymous said...

Mie naomba kuuliza huyo aliyeuliza kama huna housegirl, je wewe mkaka unaishi nchi gani? Ukinijibu ntaandika nnachotaka kusema!

obat cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat penggugur