Tuesday, February 4, 2014

USIJE UKADHANI NI MJI KASORO BAHARI:- NI MOROGORO YETU YA SONGEA/PERAMIHO!!

Ndiyo:- najua wengi mtashangaa, lakini msishangae sana. Tulio wengi tunafahamu Morogoro hii kutokana na HOSPITAL maalumu/MAARUFU ya  wagonjwa wa ukoma.  Si mbali kutoka Peramiho kama sikosei ni km 5-8 hivi.

2 comments:

Fadhy Mtanga said...

Nakumbuka pia Songea kuna kijiji chaitwa Tanga. Vile vile kule Tukuyu mkoani Mbeya kuna sehemu zaitwa Tandale, Bagamoyo na Dar es Salaam.

Hapa Iringa kuna sehemu yaitwa Ilala.

Yasinta Ngonyani said...

Mtani! Basi Songea kuna sehemu inaitwa LONDON