Friday, February 21, 2014

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA BINTI YETU CAMILLA:- MIAKA 16 LEO!!!

 Mwaka 1998 tarehe 21/2 alizaliwa binti huyu. Ni siku ambayo familia hii haitaweza kusahau. Twamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote. Na twazidi kumwomba amwongoze binti Camilla katika kila akifanyacho ili kiwe vema. Pia twamshukuru Mungu kwa kutuongoza sisi wazazi/walezi katika malezi ya binti Camilla.
Katika maisha ukiwa na marafiki  basi nao hawakosi kuwa nawe katika kila litokealo. Asubuhi hii marafiki wawili kabala ya kwenda shule nao walijumuika na Camilla kwa siku hii. Walikuaja kumpongeza na kula chakula cha asubuhi pamoja. Hivi ndivyo siku ya dada Camilla ilivyoanza .....
....kaenda shule sasa...TWAMTAKIA SIKU YAKE IWE NJEMA SANA. HONGERA Binti, dada, rafiki, mjukuu nk.

11 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Hongera sana da'Camilla,MUNGU azidi kukulinda na kukubari katika Maisha yako,Uwe baraka kwa Wazazi na Jamii pia.

Hongereni sana Wazazi MUNGU azidi kuwapa Hekima,Busara,Maarifa katika Malezi yenu.

Wenu Ma'mdogo KACHIKI na Familia ya Mubena.

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana Kamila kwa siku yako ya kuzaliwa, Mungu azidi kukubariki akupe miaka mingi ya kuishi. Amen!

Camilla said...

Mama mdogo Rachel! kwanza shikamoo! Ahsante sana kwa baraka zako nzuri pia kwa pongezi. Wape salamu wote hapo nyumbani.

Na mama mdogo Mija! shikamoo nawe pia na ahsante sana kwa baraka pia kunipongeza..mpe HONGERA Mija pia kwani tuna tarehe moja:-)

Ausal said...

Hongera sana Camila, Mungu azidi kukupa afya njema!Hongera pia wazazi kwa malezi bora kwa Camila Allah awape umri mrefu ili muweze kutimiza mahitaji yake kutoka kwenu.

Anonymous said...

Happy Birthday Camilla. Nakutakia mafanikio katika maisha yako na ujitahidi katika masomo yako. By uncle Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

KACHIKI! AHSANTE SANA KWA BARAKA ZAKO...:-)

DADA MKUU MSAIDIZI! AHSANTE NAJUA NAWE HII SIKU KUNA MTU INAMUHUSU MPE SALAMU:-)
Ausal! Ahsante najua dada Camilla atapita tu hapa..Ila kama mzazi nasema ahsante sana kwa HONGERA PIA BARAKA.

kaka Salumu! Ahsante sana.

NN Mhango said...

Happy Birthday Camilla. Muhimu sasa unaanza kukua hivyo inabidi uanze kujitambua na kutambua kuwa kukua na kuongezeka kwa majukumu ukiachia mbali kuongezeka uhuru uendanao na uwajibikaji.
Mungu azidi kukulinda na kukuongoza ukue uwe mfano na tegemeo kama wazazi wako.

stephanie Haule said...

Hongera! Camila na mama.
Maisha Je una kaa wapi? natokawapi, kabila garni? Ahsante kwa pikcha ya likungu ni kweli tamu sana!
Basi sasa

Manka said...

Heri ya siku yako ya kuzaliwa Camilla,Mwenyenzi Mungu akupe Maisha mema na yenye Baraka.Hongereni Wazazi kwa kukuza.

Camilla said...

Mjomba Mhango!Ahsante kwa wosia/ushauri wako mzuri nitafanya hivyo.

Stephanie! Ahsante sana ...

Manka! Ahsante kwa HONGERa nilikuwa na siku nzuri sana

Yasinta Ngonyani said...

Ngoja nami nitoe shukrani zangu kwa wote kwa kuwa nasi katika siku hii kumpongeza dada Camilla. Hakika ninyi ni ndugu wa kweli...Mwenyezi Mungu na awabariki na KUWAONGEZEA UPENDO.