Friday, November 15, 2013

HAYA NI MAPISHI YA IJUMAA YA LEO KUKU.....KARIBUNI

Ijumaa ya leo itakuwa kuku ambayo ni:- kuku mzima, viazi, karoti, kitunguu, kitunguu saumu, tangawizi, nyanya kopo, binzari, mafuta, chumvi na maji..... Picha zaidi zinakuja baada ya muda tu....Kwa hiyo mnakaribishwa kujumuika nasi.

Na hapo ndivyo ilivyoonekana sahani yangu...wali, kuku, kiazi, karoti na mboga majani /figili ambayo imeliwa na mikono yangu mwenyewe......Karibuni chakula kipo kingiiiii kweli. Jioni njema sana na panapo majaliwa tutaonana tena kesho.

7 comments:

Rachel Siwa said...

Mmmhhhh..Tamu saana,Asante.

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki, kipo bado kingi tu karibu, karibu, karibu sana

Mija Shija Sayi said...

Mwanamke mapishi babuee!! Mungu aubariki mkono wako dada Mkuu!

Anonymous said...

Jamani jamani mie hicho chakula cha leo kinaonekana ni kitamu sana sana! Hongera kwa mapishi safi na yenye ladha. Siku ipo ntafika hapo kwako kuonja mapishi yako. Na hiyo kuku na figili jamani vilivyo vitamu.

Unknown said...

duh... huo msosi unaonekana ni mtamu kweli... mi niko njiani hivyo tena..

Penina Simon said...

UMENITAMANISHA!

Yasinta Ngonyani said...

Dada Mkuu msaidizi! Unena..Ahsante.

Usiye na jina....Nakusubiri kwa hamu kweli kweli..Ahsante sana.

Kaka wa mimi Mrope! Msosi ulikuwa mtamu mno ila nasikitika sikuwa na ugali:-( Twakusubiri karibu kaka.

Dada P! Karibu sana chakula kipo kingiiii.