Thursday, July 29, 2010

Nipo likizo na pia nimekuwa mkulima wa bustani na hapo mnaona matokeo yake!!

Mkulima ni mmoja na walaji ni wengi
Hapa mnaona matunda ni mboga ya maboga tena ile ya ubenani (Nyamuza)


Karibuni wote tujumuike kula ugali na mboga ya maboga na hapo kwenye boxi ni mchicha kwa hiyo likizo nzima ni mbogamboga tu na bila kusahau nitakuwa naweka akiba kwa wakati wa baridi. LIKIZO INAENDELEA NA TUNAPATA MVUA NYINGI SANA HAPA MWAKA HUU. TUTAONANA WAKATI MWINGINE KILA LA KHERI. NA KUMBUKENI SISI SOTE NI NDUGU.


18 comments:

Unknown said...

Kila la kheri na ukulima dada Yas. Tunakusubiri kwa hamu sana hapa kibarazani. Wasalimie wote...

emu-three said...

Ni kweli ukulima ndio jadi yetu na anayedharau ukulima kadharau mila zetu.
Tunasubiri kwa hamu mambo ya huko, upige picha nyingi ili uje utugaie kama zawadi

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Ingekuwa huku ungeota magaga kwenye mikono...naona kwa kuogopa magaga unavaa glavs...lol!

hongera sana kumbe nikija huko sitalala njaa...mboga kwa wingi saana!!!

Likizo njema!

EDNA said...

Hongera kwa mbogamboga mie nimepanda nyanya nazisubiri kwa hamu,ICA MAX,WILLY`S COOPS hawataniona kwa muda kununua nyanya zao hahahaaa.

Simon Kitururu said...

Kila la kheri!


ONGEZEO katika mtazamo baada ya kudeku pichazako mwanana Da Yasinta:

Natamani kweli vijijini kwetu bongo wakulima wangekuwa kwa kawaida wamevaa ulimbwende kama wewe.

Kwa maana kwetu WALE wa kupenda wadada walaini inaleta sana tabu katika tamanio ukikuta mdada ambaye hata kabla hujampa kauli katika kumsabahi TAYARI mikono yake inakwaruza.Si unajua tuko wenye FETISH za mikono kama tu wapendao Dimpoz?:-(

Samahani ni kipenda roho tu kwa hiyo mpendao wadada waliokomaa mikono msitishike!SI kuna wampendao Caster Semenya kuliko Rihanna?:-)

NOTE: kuna kamdhaa kwenye comment yangu kwa hiyo usitishike!

IJUMAA, wikiendi na LIKIZO NJEMA!

nyahbingi worrior. said...

Dada,kwa mtazamo wangu mi nadhani unafanya mazoezi.

Amani dada.

chib said...

mkulima wa sweden huyooo,
Mie nimevuna mahindi. Nafaidi mapapai na mapera. Viazi vilinigomea. Lakini inafurahisha kilimo ndani ya jiji.
@ Chacha :-)
@ Simon :-0

Mija Shija Sayi said...

Yasinta bado najiuliza kama mi na wewe tunapishana urefu.

Vinginevyo nakupa hongera kwa bidii yako ya kuijenga familia yako na kuhakikisha hailali njaa.

Maisara Wastara said...

Lov u my Sis.
nakutakia likizo njema...

Matha Malima said...

habari jmapili naonalikizo yako unaitumia ipasavyo.Nimependa sana hizo mboga unanikumbusha mbali sana wakati tumnalima makemba nakumbuka katika kichuuguu flani kulikuwa na mboga hizo zilikuwa hazikauki mpaka mnafikia kuvuna na maindi mboga bado unamuonekano mzuri asee ingekuwa vizuri ukanichumia na kunipostia.asante sanakwa pich nzuri ambayo umeweka ktika blog ya maisha na mafanikio.nakutakia j njema na mungu awalinde mnapoendelea kuweka matumaini kwake kwamba mungu bado anatupenda.

malkiory said...

Kule kwetu ukiona jembe lina mpini mrefu kama wa Yasinta basi watakuita wewe ni mvivu. Ila jembe likiwa na mpini mfupi basi watakuita mkulima wa hodari, maana wanaamini unaweza kuinama na kulima kwa kasi zaidi.

Kumbuka, ni suala tu la utamaduni wala haimanishi kuwa yasinta ni mvivu, mimi naelewa fika kuwa Wangoni ni wakulima hodari sana.

Binafsi kwa mara ya kwanza niliona jembe la mpini mrefu kama hilo wakati nasafiri kwenda kwa watani zetu wa jadi kule Singida, ilikuwa ni mshangao mkubwa kwangu,nilikuwa najiuliza hivi mtu atawezaje kulima wakati amesimama.

Na mpangala said...

Mlongo iyo kali mi pangekuwa karibu mbona ungenikuta mlangoni kama mambo yenywe ni hayo.
kazi njema. mdawa wa bambu

Yasinta Ngonyani said...

ndiyo wandugu nipo hapo nalima bustani yangu na likizo inaendelea kwa hiyo madukani hawataniona kununu mamboga yao na kwanza hayapo hayo mamboga. Yaani mpaka raha natoka nje na kwenda bustanini na kuchuma tu mboga na halafu kenda kupika na kula. afya afya afya. raha kweli kweli.... karibuni wote tujumuike.

Anonymous said...

这是非常有趣的阅读。我要注明你在我的博客文章。它可以吗?而你等一个Twitter帐号?

Anonymous said...

可爱的尖锐文章。没想到,这是这并非易事。尊重你!

kenproducts said...

May you try Low Cost Greenhouse kwa matokeo bora zaidi? Just contact me. +255652402665

yanmaneee said...

moncler
adidas ultra
huaraches
yeezy
kd shoes
cheap nfl jerseys
jordan shoes
jordans
cheap jordans
michael jordan shoes

shoatea said...

h7o53p8c79 v3d34z0c00 u3l91z8v87 r9j52t9x46 m3x22h7t15 l1h73c4f71