Monday, July 12, 2010

WANAWAKE NA VIPODOZI

Hivi kwa nini wanawake wanapenda sana kujiremba? Nimekuwa nikitafakari sana hili jambo na sasa nimeona ni bora niwaulize wasomaji wa kibaraza hiki cha Maisha na Mafanikio.

Mara nyingi nimekuwa nikishangaa kwanini sisi akina dada/mama au niseme wanawake kwa ujumla tunapoteza muda mwingi kwa kujioremba? Yaani kupaka wanja, kupaka rangi ya kucha, kupaka rangi midomo, kupaka poda nk. Nina rafiki amaniambia kwamba yeye hawezi kutoka nje ya nyumba bila kujiremba.

Hivi kwa nini tusiridhike kuwa kama tulivyozaliwa (NATURAL) Kwa nini kupoteza muda na pia zaidi kupoteza pesa?

6 comments:

MARKUS MPANGALA said...

Ipo kazi hapa jamani mwengaaaa. Haya kombe la dunia limaliki, nibwelili wamuyangu. Hodiiiiii mwavene.

watila said...

KWA SABABU HAMUJIAMINI WENYEWE HAKUNA KITU CHENGINE

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Watila kathema! Tuthikie toka kwa mudomo ya farasi sasa, ama?

Mary Amba said...

naomba mnambie dawa ya chunusi jamani. zinaninyima raha!!!!!!!!

Lulu said...

Wanawake ni mapambo ya dunia kama lady jay dee anavyowaita "maua" hivyo maua shurti uyamwagilie ndo yawe mazuri zaidi. Mi mwenyewe hujipodoa kiasi lakini si kwamba siwezi kutoka bila kupata vipodozi. Ila ukilinganisha na mwanaume, mimi napaka mafuta au lotion mwilini kote nag'arisha midomo yangu wakati mwanaume hana haja. Tunajiamini lakini nakshi ni asili ya mwanamke. (FARASI nimejibu)Chacha ridhika sas

Anonymous said...

SAWA NA CHACHANDU