Wednesday, July 14, 2010

Huu ni ujumbe wa leo Jumatano!!

Kupenda kunaanza na tabasamu, kunastawi/kunakua kwa mabusu, na kunaishia na machozi. Wakati ulipozaliwa wewe ulilia na kila mtu aliyekuwepo karibu yako alitabasamu. Ishi maisha yako ili utakapokufa, utakuwa unatabasamu na kila aliye karibu yako atalia.
Picha kwa hisani ya blog hii http://mbilinyi.blogspot.com

5 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

unaweza usiwe sahihi na ukisemacho juu ya kulia na kufurahi na sio kila msiba watu woote hulia, wengine huchekelea,. akifa /akiuwawa kibaka anayekuibia mchuzi wako wa dagaa kila siku utalia?? au likifa lile limama linalomtega mumeo mpaka akalipatia dude na kukunyima wewe, utalia??

je hakuna wakati unaliaga wakati umefurahia?

Blackmannen said...

"Gindu Ng'wanamboje" ni binti yangu wa mwisho, ambaye nililia kilio cha furaha alipokutana na upepo wa duniani na kuungana nasi, alipozaliwa tarehe 01 machi 2010 saa 1600. Ninampenda sana, sina neno jingine mdomoni la kusema kuhusu upendo huu.

Upendo huu haujapunguza upendo wangu kwa wanangu Nshoma, binti yangu, Mhoja na "Babu" Zephania, vijana wangu. Wanangu, Wote ninawapenda sana.

Ujumbe wa Jumatano umenifanya nifikiri tena na tena kuhusu wanangu wapendwa. Ahsante sana Yasinta.

It's Great To Be Black=Blackmannen

emuthree said...

Ni kweli na naongezea kwa kusema, kutabasamu huongeza nuru usoni, na kuongeza uhai wa mtu. Ni vyema kila mara tuakawa tunatabasamu, hata kwa mbaya wako, ukitabasamu huenda zile hasira au chuki zilizopo kwake zikayeyuka.
Ahsante sana kwa ujumbe wako huu murua

emu-three

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Blackmannen: una hakika ni wa mwisho?...lol!

Ama wa mwisho kwa sasa tu na baadaye vitaongezeka vingine kama 11 hivi?

Sorry, ndo ndoto yangu ya kuwa na vitoto 12 (timu ya mpira yenye reserve 1 na mpuliza kipyenga mimi na mshika kibender mama yao)...lol!

Yasinta Ngonyani said...

nawshukuruniwote kwa kuwa nami kwa maoni mazuri na kutoc hoka kutembea blog hii ya maisha na mafanikio.