Friday, July 9, 2010

Ijumaa njema kwa wote/salamu toka Iringa


Maisha ni raha, starehe, musiki, kula na kunywa. Ila usinywe sana . Na vingine pia viwe wastani. Picha toka hapa. Karibuni komoni jamani!!! Haya ijumaa njema!!!

13 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hivi ni nani aliyebuni ulevi na vilevi???

EDNA said...

Ijumaa njema kwako pia,naona mnyalukolo mwenzangu ameshaianza weekend na komoni,lol.....wahehe oyeeeee!

Blackmannen said...

Hivyo "vingine" ni muhimu sana kufanyika katika kiwango cha juu kutokana na umuhimu wake maishani.

Tangu J3 hadi Ijumaa, wawili mnaonana kwa nadra sana kama vile mpo "Lupango". Ni wikiendi pekee ndiyo inayowapa nafasi ya kuonana na kuelezana yote kutoka moyoni jinsi ulivyom-miss mwenzio.

Wikiendi njema Dada Yasinta na wengine woooooooote!!!

It'sGreat To Be Black=Blackmannen

chib said...

Huyo Mzee, lazima ni mkibosho.
Weekend njema

Albert Kissima said...

Dah! Mzee alivyobize hapo, hata siafu wangemng'ata asingetamani kuliachia hilo "chubuku" sa sijui ni la "mbege". Kama ni mkibosho kama alivyokisia Ndugu Chib, lazima itakuwa ni mbege tu.

Nimekumbuka, kule Uru mlimani kuna baa moja ya mbege ilikuwa imeandikwa "inu wuuncha saiidii" maana yake, "ya leo(mbege) ni nzuri zaidi". Hahahahaha! Mbege niliiacha miaka kumi iliyopita.


Mama Maisha, nami nikutakie ijumaa njema, pamoja na wanablog wote.

Unknown said...

nawe pia dada Yas. Salamu kwa wote huko...

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

@Kamala: binadamu wewe!

PASSION4FASHION.TZ said...

Wanyalukolo utawajua tuu,Edna siuseme tu na wewe mate yamekujaa mdomoni? unakumbuka ulanzi nini? hahahahaaa wahehe oyeeee!mwipulika!

Yasinta leo umewachokoza watu flan hapa,kuna watu na watani zao humu ndani shauri yako, haya ijumaa njema na kwako.

Yasinta Ngonyani said...

Kamala:-)
Edna kamwene be wamlongo wangu! komoni komini...

Blackmannen ! Raha jipe mwenyewe!!
Kaka Chib! ni muhehe kaka.
Kaka albert umenichekesha kweli eti hata siafu wakimuuma hatajua...kaazi kwelikweli.

Ka´Mrope salam zimefika.

Mtakatifu!!MMMMMhhhhh:-(
Chacha! asante

Dada S. watu wanapenda ugimbi unajua.:-)

John Mwaipopo said...

post ya ugimbi haiwezi kupita bila kupata komenti yangu. yasinta umenikumbusha mbali. ngoja sasa niinuke niitafute hiyo 'loko' ilipo

Penina Simon said...

Kha hapa mtu kesha kamata kopo lote hilo kuna control kweli?,

RACHEL said...

HAHHAHAH!!EDNA OYEEEEEEEEEEEE!!