Thursday, July 29, 2010

Nipo likizo na pia nimekuwa mkulima wa bustani na hapo mnaona matokeo yake!!

Mkulima ni mmoja na walaji ni wengi
Hapa mnaona matunda ni mboga ya maboga tena ile ya ubenani (Nyamuza)


Karibuni wote tujumuike kula ugali na mboga ya maboga na hapo kwenye boxi ni mchicha kwa hiyo likizo nzima ni mbogamboga tu na bila kusahau nitakuwa naweka akiba kwa wakati wa baridi. LIKIZO INAENDELEA NA TUNAPATA MVUA NYINGI SANA HAPA MWAKA HUU. TUTAONANA WAKATI MWINGINE KILA LA KHERI. NA KUMBUKENI SISI SOTE NI NDUGU.


Sunday, July 25, 2010

Barua fupi kwa wasomaji wa blog ya Maisha na Mafanikio!!

Nipo likizo jamani!!

Nina furaha kuandika waraka huu na kuwataarifu ya kwamba nitakuwa nimeadimika adimika. Katika ulimwengu huu kila mtu anahihitaji mapunziko. Kwa hiyo mama Maisha na Mafanikio amepata liki kikazi na atakuwa likizo akiambatana na familia yake.
Na nimeona ni vema niwaage nitajaribu kupitapita pale nipatapo wasaa. Nawatakieni wote kila la kheri kwa lolotw mtakalotenda na tukutane panapo majaliwa.
TUTAONANA BAADA YA MUDA SI MREFU....KAPULYA aka Yasinta na pia NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA !!!

Saturday, July 24, 2010

UJUMBE WA LEO NI KUTOKA IRINGA!!! UREMBO AU KUSOMA???

Je? utamaduni wetu upo wapi?

Kwako dada Yasinta, mimi ni msomaji wa blog ya maisha na mafanikio .Ninakuomba uufikishe ujumbe huu. Ni kwamba ningependa kupata maoni ya watu mbalimbali hapa ambapa hawa dada zetu wa
vyuo vikuu vya Tanzania wanafanya mashindano ya urembo. Kwa mtazamo wangu
watanzania tulipa gharama za hawa kusoma sasa ni kupoteza muda kufanya mambo ya
urembo.

Pengine cha kusitisha zaidi pamoja na kuwa ni mambo ya urembo pia hayana ubunifu
wowote ule. Inachoonekana hawa dada zetu wa vyuo wananukuru mambo ya
ulaya/Marekani kama yalivyo wanashindwa hata kufanya ubunifu ili waweke hata
utanzania kidogo. Kwanini wamevaa vikaputa badala angalau ya kufunga kanga au
kitenge au vinginevyo. Hata Japan au China mashindano haya yapo lakini
wameyafanyia marekebisho kidogo kuwa ya kichina/kijapani aidha kubadili mavazi
au vinginevyo. Sisi watanzania tena kama kawaida yetu tunanukuru tuu. Siyo
kwamba sipendi hawa watu waonyeshe urembo wao hapana ila tuwe tunaweka
u-tanzania kwenye hivi vitu la sivyo tutabaki kuwa watumwa wa tamaduni za watu
wengine.
Picha hii ni hisani ya Mjengwa blog. http://www.mjengwa.blogspot.com/

Wednesday, July 21, 2010

Mlevi anapolewa chakari na kuanza kuongea!!!!

"Mlevi anapolewa chakari na kuanza kuongea unapaswa kumsikiliza kwani wengi wao huongea yale yaliyoko mioyoni mwao. Uhusiano wa pombe na ufanyaji kazi wa ubongo husababisha mlevi kunena yale yaliyoko moyoni mwake bila ya simile"- Mwalimu Malekela, Tabora Boys 1994.
Swali ni kwamba, je utafaidikaje na uvumbuzi huu? Nadhani ni kwa kuchagua yale yatokayo kwenye kinywa cha mlevi kwani si yote yatakuwa ni yenye kujenga. Mengi yatokayo kwenye kinywa cha mlevi hutokana na migogoro iliyoko ndani ya mioyo yao. Mara nyingi migogoro hii inakuwa ni ile isubiriyo suluhisho.
Katika jamii yangu mara nyingi nimeshuhudia tabia ya baadhi ya watu pale inapotokea kutokuelewana na wenzao, basi huenda kunywa pombe na kisha kurejea kwa mabishano zaidi. Je kuhusu wale wanaume wanaopenda kupiga wake zao pindi wanapolewa? Je hii nayo inasababishwa na migogoro au inakuwa ni tabia ya kuzoea? Au pale daktari au mwalimu anapohitaji glasi mbili au tatu ili waweze kufanya kazi zao? Hii inakuwaje?? Je kuna uhusiano kati ya unywaji pombe na ufanisi katika kazi? Je umepata kusikia kuhusu yule daktari bingwa wa upasuaji ambaye ni lazima apate kinywaji kwanza ili aweze kutenda kazi yake vema?
Habari hii nimetumiwa na msomaji wa blog ya Masha na Mafanikio na kuniomba niiweka hapa kibarazani ili tujadili kwa pamoja. Haya wapendwa karibuni na tujadili. Umoja ni nguvu .....

Tuesday, July 20, 2010

Ilibidi uchunguzi ufanyike kwanza ili kuja wapi vuvuzela zinatoka kabla ya kuanza kupuliza!!

Ungejua vuvuzela hiyo imetoka wapi?
Duh! Kumbe!!


Sasa unajua mwanzo wake ni wapi, kaazi kwelikweli


Monday, July 19, 2010

Siamini kama wewe ndiye yule kabla hatujaoana!

Je sijakuwa makini??
Inawezekana baada ya kuishi katika mahusiano ya uchumba sasa umeoa au kuolewa, Karibu sana kwenye chama kubwa, chama la ndoa, ulimwengu mpya kabisa, ambako mapenzi huchukua sura mpya ya uhalisia.

Sasa kila kile uliona si tatizo kwa mchumba wako unajikuta kinakuudhi, namna anavyotafuna chakula sasa inaudhi, namna anaweka muziki katika sauti ya juu sasa inaudhi, namna anaacha nywele kwenye sink bafuni sasa inaudhi, namna anaacha taulo lenye maji bila kulitundika ukutani inaudhi.

Namna anaacha kitanda bila kutandika inaudhi, namna anavyokoroma akilala usiku sasa inaudhi, namna anavyoacha drawer za makabati bila kuzifunga inaudhi sana, namna anavyoacha kuweka nguo na makoti kwenye hanger sasa inaudhi mno, namna anavyoongea bila break sasa inakuudhi sana, list inaendelea ..............................
Kumbuka wakati wa uchumba hivi vitu uliviona vidogo sana na kwamba hakuna tatizo!

Swali la kujiuliza je, nini kimetokea kwa ule upendo (fall in love)?
Ilikuwa ni illusions kukusababisha ujipeleke mwenyewe hadi kusaini mkataba wa ndoa na kukiri kwamba hadi kifo, katika raha na shida, katika afya na ugonjwa na inawezekana wewe ni mmoja ya wale ambao wanalaani sana ndoa walizonazo kwani wale ambao kwanza waliwaambia NAKUPENDA NA NITAKUPENDA wamewadanganya na sasa unajikuta upo kwenye ndoa ambayo kila siku hali ni mbaya.

Una haki ya kukasirika kwani ni kweli ulidanganywa na tatizo lilikuwa ulipokea information ambazo hazikuwa sahihi. Na hizo information zilikuwa ni ile hali ya kupendana (fall in love) ambayo katika ukweli si upendo wa kweli bali ni illusions.
Kale kakichaa ka kuamini kwamba tutapendana milele bila kuumizana wala kukwazana kangedumu na kuwa hivyo siku zote.
Katika asili “fall in love” ni mating character ya binadamu kuhakikisha mke na mume wanavutiana ili kuhakikisha species inaendelea (survival) na si upendo wa kweli.

Ulikuwa tayari kuacha kusoma kwa ajili ya mitihani ili kuwa na mpenzi wako maana yeye alikuwa muhimu mno.
Uliacha kwenda kwa rafiki zako hata ndugu zako kwa kuwa ulimpenda sana mchumba wako.
Uliacha hata kwenda kusoma au kwenda kazini ili kuhakikisha unampa mpenzi wako kile moyo wake unakipenda (to make her/him happy)

Kijana mmoja alikiri kwamba
“Tangu nimekutana na huyu binti, nimempenda, siwezi kufanya kitu chochote tena, siwezi kuwaza kuhusu kazi kwani kila wakati nawaza na kuota kuhusu yeye.
Hamu niliyonayo ni kumfanya yeye awe na furaha muda wote, nipo tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha anakuwa na furaha”.
Yaani mtu akili inahama hadi unajiona wewe ni Mama Theresa kwa maana ya kutoa kila kitu ili kuonesha upendo kumbe ni illusions.

Kumdondokea mtu (fall in love) ni hali ambayo hudanganya na kumfanya mtu ajione kweli yupo katika upendo wa kweli. Huamini kwamba hakuna tatizo linaweza kuwepo kila kitu ni shwari.

Baada ya hali ya kudondokeana (in love) kuchuja (kawaida baada ya miaka 2) ndipo mtu huanza kurudi kwenye ulimwengu halisi.
Ndipo unaanza kugundua yale unayapenda na kuona kumbe ni tofauti na yeye anayoyapenda.
Unajikuta wewe unapenda sex na yeye anajisikia kuchoka na hapendi.
Unapenda kununua gari kwanza na yeye anapenda mjenge nyumba kwanza.
Unapenda kutembelea wazazi wako yeye anasema hapendi mtumie muda mwingi kwa wazazi wako.
Unapenda kwenda kuangalia match ya mpira wa miguu (soccer), anakwambia unapenda mpira kuliko yeye.

Kidogo kidogo ule moto wa mapenzi ya kwanza (fall in love) huanza kuyeyuka na kila mmoja sasa anaanza kujikita kwenye kujipenda yeye na mambo yake, kujihisi na kuwaza kivyake na sasa mnazidi kuwa watu wawili tofauti.
Bila kufahamu namna mapenzi yanapanda na kushuka mnaweza kuishi kuachana

Nimeipenda mada hii na kwa vile wote tuna lengo moja nimeona si vema kama nikiweka katika kibaraza hiki cha maisha na mafanikio zaidi gonga hapa. Haya karibuni tujadili kwa pamoja.

Sunday, July 18, 2010

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE KWA UJUMBE HUU!!!!

Mungu akapanda bustani akaweka mtu ndani yake: Mwa 2:8
Ua hili ni zuri na linapendeza. Hata nyuki amevutiwa nalo. Ni mfano wa Kristo aliyefufuka kutoka wafu. Nasi tuvutike kwenda kwenye utukufu wake.
Jumapili njema kwa watu wote na mwisho mwema wa juma hili. Na kumbukeni wote mnapendwa!!!!

Friday, July 16, 2010

HATIMAYE JANA NIMESUKWA TENA BAADA YA MIEZI SITA, KAAZI KWELIKWELI!!

Mtaka cha uvungoni sharti ainame

Masaa sita na nusu baadaye nilikuwa hivi. Kuchoka pia :-)
Ijumaa njema tutaonana wakati mwingine!!!!!!!


Thursday, July 15, 2010

KILIO CHA MAUAJI YA ALBINO!!!

Festo kaduma ni mlemavu wa ngozi (Albino) ambaye amelazimika kuishi kwa mganga wa kienyeji Dr Antony Mwandulami ili kuyanusuru maisha yake na waauwaji wa maalbino tukio ambali linaelezewa kwa majonzi makubwa wa wadau mbali mbali akiwemo Bibi Yasinta Ngonyani mtanzani anayeishi nchini Sweden mwandishi wa makala haya Bw Francis Godwin anaelezea zaidi."..Nimekaa na kufanya tafakari ya kina kuhusiana na mauaji ya ndugu zetu Albino yanayoendelea kuisakama Tanzania. Dhana mbili zinajitokeza katika tafakari hiyo.
Moja ni dhana nzima ya ubaguzi wa rangi na pili ni tathimini yangu kuhusu mikakati ya serikali ya Tanzania kuwahakikishia usalama ndugu zetu Albino"Ukiangalia ubaguzi wa rangi uliokuwepo Afrika Kusini enzi za Makaburu, watu walipangwa katika makundi kutokana na rangi zao; weupe ( Wazungu ), watu wa rangirangi (coloured ) na weusi ( Waafrika ). Huduma zote, ikiwa ni pamoja na elimu, zilitolewa kwa kuzingatia rangi ya mtu.
Kulikuwa na kumbi za starehe kwa ajili ya watu weupe, ambapo mtu mweusi hakuruhusiwa kuingia. Kuna sehemu zingine ambazo mwafrika hakuruhusiwa hata kukanyaga kabisa. Akikamatwa, alipewa kipigo kikali na hata kutupwa lupango ( jela).
Ubaguzi wa rangi, hususani dhidi ya Mwafrika, ulikuwepo hata katika nchi za Magharibi. Nakumbuka nimeona picha zilizoandika “only for blacks and dogs here.” Hii ilikuwa hatari sana, kwani mtu mweusi alinyimwa haki zake kutokana na rangi ya ngozi yake .
Sasa tujiulize.Hivi Albinno ni mtu wa namna gani? Anaweza tambuliwaje kwa muonekano wake? Sintopenda kuingia ndani zaidi kuchimba sababu za kibaiolojia zinazo mfanya mtu azaliwe Albino. Hata hivyo mtu haitaji microscope ( darubini) wala elimu ya Chuo kikuu kumtambua Albino.
Nionavyo mimi, naamini bila pingamizi lolote kuwa mauaji ya Albino yanayoendelea kuitikisa Tanzania “Kisiwa cha Amani” ni mwendelezo wa dhambi ya ubaguzi wa rangi, lakini huu ni ubaguzi mkali zaidi katika historia ya mwanadamu kushinda hata dhambi ya biashara ya utumwa.
Nasema nimkali zaidi kwani unalenga kuondoa maisha ya mwanadamu kwa ukatili wa kunyofoa viungo, tofauti na ule wa kumzuia mweusi kutembelea mitaa fulani au katika upandaji wa mabasi n.k !Ni kwa kuangalia rangi ya ngozi yake, unaweza kumtambua Albino.
Kwa bahati mbaya, Albino anayezaliwa Afrika, ni tofauti na yule wa nchi za Ulaya na Marekani, kwani Albino wa nchi hizo, hatofautiani sana na mtu wa kawaida. Rangi yake inarandana na ya mzungu . Si ajabu kama naye angefanana na mwafrika, angebaguliwa na kuuawa.
Kinachonishangaza mimi, ni kwanini Tanzania au Watanzania kwa ujumla hatusemi ukweli kuwa mauaji ya Albino yanayoendelea, ni ubaguzi wa rangi ili tuweze kupambana nao ipasavyo na Jumuiya ya Kimataifa iweze kutoa msaada sawawa na ambavyo jumuiya ya Kimataifa, hususani Tanzania, ilivyojitoa muhanga kung’oa mzizi wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini?Kwa mtazamo wangu, Watanzania tumeaminishwa kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani na hivyo sisi ni bora zaidi kuliko Taifa lolote kiutamaduni na kimaadili.
Hii si kweli na huu ni mtazamo potofu ambao tusipokuwa makini, utatufikisha pabaya.Kwa uzoefu wangu, kitendo cha ubaguzi kikifanywa na Taifa jingine mfano Burundi, Kongo, Afrika Kusini, Ujerumani, M arekani ama Israeli, tunawanyooshea kidole kuwa wamepotoka huku tukitamka wazi kuwa nchi hizo zinafanya ubagauzi wa rangi.
Je, kwa nini kitendo hicho kikitendeka Tanzania kama cha mauaji ya Albino, tunapata kigugumizi kutamka wazi kwamba ni kitendo cha ubaguzi wa rangi na tunaanza kutafuta majina mengine kama vile “unyanyasaji wa Albino” na k.n yasiyotoa picha halisi ya mambo yanayoendelea?Kwani ubaguzi wa rangi lazima kitendo kifanywe na mtu mweupe ( mzungu ) dhidi ya mweusi ( mwafrika ) ili kistahili kuitwa ubaguzi wa rangi? Vipi kama kitendo hichohicho kitafanywa na mtu mweusi dhidi ya mtu mweupe ( mzungu / albino ), hakiwezi kuitwa kitendo cha ubaguzi wa rangi?Au kama mtu mweusi atafanya kitendo cha kumbagua mweusi mwenzake kutokana na rangi yake kama vile mweusi sana , mweusi tiii! mweusi wa kati, nacho hakiwezi kuitwa ubaguzi wa rangi? Na vipi kama mtu mweupe ( mzungu ) akimbagua na kumnyanyasa mweupe mwingine kama vile Mchina , Mwarabu n.k, kitendo hicho kitaitwaje?Kwa uzoefu wangu, hasa baada ya kuangalia matukio ya hivi karibuni ambapo Waafrika Kusini waliamua kuwavamia na kuwaua wahamiaji kutoka nchi nyingine za Afrika, Tanzania ilikuwa mstasri wa mbele kukemea vitendo hivyo.
Tanzania ilitoa tamko kali na kwa uwazi kabisa ikisema, “ Dhambi ya ubaguzi bado inaitafuna Afrika kusini.” Nikaanza kuangalia mambo mengine ninayoyashuhudia kila kukicha huku Marekani. Mtu akifanyiwa kitendo fulani, kwa mfano, ikiwa ni mweupe kakifanya, hukimbilia kusema ni ubaguzi wa rangi. Sasa mimi najiuliza.
Je endapo Mtanzania mweusi mmoja ataenda nchi yoyote ya Magharibi kama vile kusoma au kufanya kazi halafu akauliwa na kunyofolewa viungo kama wanavyofanyiwa Albino, Tanzania itasemaje? Haina ubishi , kila mtu atasema “amebaguliwa na kuuwawa kutokana na rangi yake.” Swali langu la msingi ni hili:
Kitendo cha Albino kunyofolewa viungo vyake kinyama na hatimaye kuuawa na mtu mwenye rangi nyeusi kisa rangi yake ni tofauti na cha mtanzania mweusi aliyebaguliwa na kuuawa ugenini hususani katika nchi za magharibi? Kwa nini mauwaji ya Albino yasitajwe kama ubaguzi wa rangi? Maana Albino naye hutambuliwa kwa rangi yake! Kama tumefikia hatua ya kuuana kutokana na rangi zetu; moja nyeusi, nyingine ya rangirangi ( coloured ) na wote ni binadamu tena watanzania, tuanaelekea wapi ndungu zangu?Serikali ya Tanzaia inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kupambana na janga hili la mauaji ya albino.
Uamuzi wa kugawa simu kwa albino wote, pengine waweza kusaidia kwa kuwawezesha kupiga simu polisi wanapovamiwa.Lakini Serikali inawasaidiaje albino waishio kijijini ambako hakuna umeme? Simu hiyo inachajiwa kwa teknolojia gani? Je simu hizo hizitakuwa kivutio kingine na hivyo kuwafanya wavamiwe zaidi?Kama imefikia hatua albino hawezi kutembea peke yake au kutembea baadhi ya masaa hususani jioni, kama imefikia hatua Mbunge maalum ambaye ni albino lazima apewe ulinzi maalum ili asinyofolewe viungo vyake, falsafa ya Tanzania kama kisiwa cha amani iko wapi?Ndugu zetu wa Marekani wanaelekea kuishinda dhambi ya ubaguzi wa rangi, kwani hatimaye wamefikia hatua ya kumchagua mtu mweusi kuwa Rais wao kwa kuangalia uwezo wake, hoja zake na si tena kigezo cha rangi kama Dr. Martin Luther King Jr aliposisitiza katika ndoto yake ( I HAVE A DREAM). Mwaka 2010 kama mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa albino, tutakuwa tayari kumpigia kura endapo atakuwa na sifa za kutuongoza? Tafakari, Chukua hatua.

Kwa upande wake Bw Kaduma anasemakuwa ameona ili kujiokoa na wauwaji hao kuishi kwa mganga huyo ambaye ndiye aliyemuokoa kuuwawa baada ya kuwekewa mtengo na mkazi mmoja wa Mbarali ambaye alitaka kumuua na kuuza viungo vyake kwa zaidi ya shilingi milioni 2.

Kaduma anasema kuwa yeye alikuwa hajua chochote juu ya mpango huu ila alishangaa kuona polisi ,magnga huyo na mtuhumiwa wakifika kijijini kwao na kudai kuwa wamekuja kumwokoa baada ya mtuhumiwa huyo kukili kutaka kufanya mauwaji.

Bw Kaduma ambaye kwa sasa amekuwa akiishi nyumbani kwa mganga huyo na kufanya kazi ndogo ndogo huku akitembea na kisu kama ngao ya kujilinda na wauwaji hao ameomba serikali kuwawajibisha waganga wanaochochea mauwaji hayo ya maalbino na kuwabakiza waganga kama Dr Mwandulami ambaye ameonyesha kuchukizwa na mauwaji hayo na kujikita katika kutetea uhai wa maalbino.

Usikose wiki ijayo kupata undani wa tukio hili na maisha ya albino huyo pamoja na mwanamke mwenye familia ya watoto wanne anayeishi kwa mganga huyo akikwepa kuuwawa kijiji kwao.

Makala hii ilishawahi kusomwa lakini nimeona si mbaya kama tukiirudia tena basi gonga hapa

Wednesday, July 14, 2010

Huu ni ujumbe wa leo Jumatano!!

Kupenda kunaanza na tabasamu, kunastawi/kunakua kwa mabusu, na kunaishia na machozi. Wakati ulipozaliwa wewe ulilia na kila mtu aliyekuwepo karibu yako alitabasamu. Ishi maisha yako ili utakapokufa, utakuwa unatabasamu na kila aliye karibu yako atalia.
Picha kwa hisani ya blog hii http://mbilinyi.blogspot.com

Tuesday, July 13, 2010

Warembo wa wiki hii:- Je? unaona nini katika picha hizi? sijui hawa ni mapacha?:-)

Hivi huyu yupo wapi na ni nani?
Na huyu pia sijui ni nani ila kuna kitu hawawatu wanafanana au? Je ni kipi ambacho hawajafanana?

Monday, July 12, 2010

WANAWAKE NA VIPODOZI

Hivi kwa nini wanawake wanapenda sana kujiremba? Nimekuwa nikitafakari sana hili jambo na sasa nimeona ni bora niwaulize wasomaji wa kibaraza hiki cha Maisha na Mafanikio.

Mara nyingi nimekuwa nikishangaa kwanini sisi akina dada/mama au niseme wanawake kwa ujumla tunapoteza muda mwingi kwa kujioremba? Yaani kupaka wanja, kupaka rangi ya kucha, kupaka rangi midomo, kupaka poda nk. Nina rafiki amaniambia kwamba yeye hawezi kutoka nje ya nyumba bila kujiremba.

Hivi kwa nini tusiridhike kuwa kama tulivyozaliwa (NATURAL) Kwa nini kupoteza muda na pia zaidi kupoteza pesa?

Sunday, July 11, 2010

Jumapili njema na ujumbe huu:-Tenda wema

Kuna wengi walimwengu, kujaa dunia nzima,
Muumba ni yeye Mungu, kila moja na karama,
Wenye maisha machungu, huhitaji tendwa mema,
Tenda wema nenda zako.

Wale walio shidani, kamwe sije watupa,
Waondoe majonzini, usijaribu wakwepa,
Wafanye was'ende chini, maisha wakaogopa,
Tenda wema nenda zako.

Yale walopungukiwa, ambayo wewe unayo,
Usisite kuyatowa, kadiri uyawezayo,
Upate kuwaokowa, yale yawasumbuayo,
Tenda wema nenda zako.

Wale walio na njaa, usisite kuwalisha,
Waso nguo za kuvaa, ukapate kuwavisha,
Waliokata tamaa, imani kuwahuisha,
Tenda wema nenda zako.

Wale wanaoumia, ukawafute machozi,
Ili waache kulia, wayahimili majonzi,
Hao 'sije wakimbia, peke yao hawawezi'
Tenda wema nenda zako.

Ila utendapo wema, usingoje shukurani,
Tena 'sigeuke nyuma, ungoje kitu fulani,
Tena usije kupima, ujuwe yake thamani,
Tenda wema nenda zako.

Kamwe usihesabu, Mungu ndiye anajuwa,
Kwa hilo ukawe bubu, nawe utabarikiwa,
Timiza wako wajibu, moyo kutopungukiwa,
Tenda wema nenda zako.

Ukitaka mashairi zaidi gonga hapa
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NDUGU ZANGUNI!!!!!

Friday, July 9, 2010

Ijumaa njema kwa wote/salamu toka Iringa


Maisha ni raha, starehe, musiki, kula na kunywa. Ila usinywe sana . Na vingine pia viwe wastani. Picha toka hapa. Karibuni komoni jamani!!! Haya ijumaa njema!!!

Thursday, July 8, 2010

Nasema ahsante sana

Nakushuru sana Mungu, mema umenijalia,
Ewe muumbaji wangu, sifa nakurudishia,
Bariki maisha yangu, uniangazie njia,
Nasema ahsante sana.

Nakushukuru sana mama, kwanza ni kwa kunizaa,
Umenilea kwa wema, kwa nyota inayong'aa,
Nitashukuru daima, umeniwashia taa,
Nasema ahsante sana.

Nakushukuru mwandani, mpenzi wa moyo wangu,
Kwangu unayo thamani, kwani u sehemu yangu,
Daima uwe pembeni, sitoweza peke yangu,
Nasema ahsante sana.

Ndugu nawashukuruni, mnanithamini sana,
Tangu mwangu utotoni, tungali tukipendana,
Ninawapenda moyoni, na mbarikiwe sana,
Nasema ahsante sana.

Nashukuru marafiki, Mungu amenijalia,
Tungali tupo lukuki, pamoja twafurahia,
Kwa raha ama kwa dhiki, ndani ya hii dunia,
Nasema ahsante sana.

Siku niliyozaliwa, ambayo naadhimisha,
Furaha niliyojawa, ninyi mmesababisha,
Kwa umoja tumekuwa, imara kwenye maisha,
Nasema ahsante sana.

Upendo ndiyo silaha, hakika tunapendana,
Upendo una furaha, kweli twafurahiana,
Na hivyo huleta raha, raha kifani hakuna,
Nasema ahsante sana.

Ahsante pasi kipimo, nawashukuruni sana,
Upendo pasi kikomo, ninawapendeni sana,
Furaha tele iwemo, maisha marefu sana,
NASEMA AHSANTE SANA.

Nawashukuruni sana, mara zisizo na idadi kwa upendo wenu muuoneshao kwangu, siku zote. Ninatamani kusema maneno mengi kuonesha wingi wa furaha na shukrani zangu kwenu, lakini maneno hayajitoshelezi. Ninasema, nawashukuruni sana, ninawapenda sana, na ninawaombea furaha na mafanikio daima.
Pamoja sana.

Shairi hili limeandikwa tarehe 14/11/2009 na mtani wangu Fadhy Mtanga ukitaka kusoma mashairi yake zaidi tembelea hapa. Nakuhakikishia hutapenda kukusa kutembea mara kwa mara.

Wednesday, July 7, 2010

Jamani, Jamani, Jamani BadoTU??????????

Maisha haya bado tu jamani, tuache kupigana tuishi kwa amani, upendo na tupendane.

Tuesday, July 6, 2010

ZAHANATI YA GOMELO KIJIJINI KISAKI

Huduma zetu za afya
Hapa ni "wodini" katika Wilaya ya Morogoro, Tarafa ya Bwikila Kata ya Kisaki kijijini Gomela. Kweli hapo mgonjwa atapona au atapata nafuu?- Kitanda cha ngozi ya ngómbe au mbuzi "teremke tukaze". Na uvunguni mwa kitanda tunaona besen/karai ni kama choo hapo. Ukiangalia dirishani ndio sehemu ya kutundukwa drip zaidi tembelea blog ya Fautine, mzee wa Changamoto na Lukwengule. Je huu kweli ni uungwana? Viongozi wetu wapo wapi???? Je?? mnasikia vilio vyetuuuuu???????

Monday, July 5, 2010

Siri ya herufi ya mwanzo ya Jina lako

Je Unajua Siri ya herufi ya mwanzo ya jina lako?. Soma hapa utaweza kuelewa Tabia zako au tabia za rafiki au mpenzi wako.

>HERUFI A
>Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira. Herufi A inawakilisha Nyota ya Punda.
>HERUFI B
>Mwenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake. Herufi B inawakilisha Nyota ya Ngombe,
>HERUFI C
>Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano Herufi C inawakilisha Nyota ya Mapacha,
>HERUFI D
>Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo. Herufi C inawakilisha Nyota ya Kaa,
>HERUFI E
>Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu. Herufi E inawakilisha Nyota ya Simba,
>
>HERUFI F
>Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi. Herufi F inawakilisha Nyota ya Mashuke,
>HERUFI G
>Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu. Herufi G inawakilisha Nyota ya Mizani,
>HERUFI H
>Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi. Herufi H inawakilisha Nyota ya Nge,
>HERUFI I
>Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka. Herufi I inawakilisha Nyota ya Mshale,
>HERUFI J
>Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo. Herufi J inawakilisha Nyota ya Mbuzi,
>HERUFI K
>Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha. Herufi K inawakilisha Nyota ya Ndoo,
>HERUFI L
>Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara. Herufi L inawakilisha Nyota ya Samaki,
>HERUFI M
>Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika. Herufi M inawakilisha Nyota ya Punda
>HERUFI N
>Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana. Herufi N inawakilisha Nyota ya Ngombe
>
>HERUFI O
>Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia. Herufi O inawakilisha Nyota ya Mapacha
>HERUFI P
>Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi P inawakilisha Nyota ya Kaa
>HERUFI Q
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana. Herufi Q inawakilisha Nyota ya Simba
>HERUFI R
>Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani. Herufi R inawakilisha Nyota ya Mashuke
>HERUFI S
>Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa. Herufi S inawakilisha Nyota ya Mizani
>HERUFI T
>Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika. Herufi S inawakilisha Nyota ya Nge
>HERUFI U
>Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mshale.
>HERUFI V
>Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mbuzi.
>HERUFI W
>Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari. Herufi W inawakilisha Nyota ya Ndoo.
>HERUFI X
>Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi X inawakilisha Nyota ya Samaki.
>HERUFI Y (YASINTA)
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha. Herufi Y inawakilisha Nyota ya Punda
>HERUFI Z
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo. Herufi Z inawakilisha Nyota ya Ngombe.


Je Unajua Siri ya herufi ya mwanzo ya jina lako?. Soma hapa utaweza kuelewa Tabia zako au tabia za rafiki au mpenzi wako.
>HERUFI A
>Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira. Herufi A inawakilisha Nyota ya Punda.
>HERUFI B
>Mwenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake. Herufi B inawakilisha Nyota ya Ngombe,
>HERUFI C
>Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano Herufi C inawakilisha Nyota ya Mapacha,
>HERUFI D
>Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo. Herufi C inawakilisha Nyota ya Kaa,
>HERUFI E
>Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu. Herufi E inawakilisha Nyota ya Simba,
>
>HERUFI F
>Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi. Herufi F inawakilisha Nyota ya Mashuke,
>HERUFI G
>Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu. Herufi G inawakilisha Nyota ya Mizani,
>HERUFI H
>Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi. Herufi H inawakilisha Nyota ya Nge,
>HERUFI I
>Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka. Herufi I inawakilisha Nyota ya Mshale,
>HERUFI J
>Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo. Herufi J inawakilisha Nyota ya Mbuzi,
>HERUFI K
>Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha. Herufi K inawakilisha Nyota ya Ndoo,
>HERUFI L
>Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara. Herufi L inawakilisha Nyota ya Samaki,
>HERUFI M
>Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika. Herufi M inawakilisha Nyota ya Punda
>HERUFI N
>Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana. Herufi N inawakilisha Nyota ya Ngombe
>
>HERUFI O
>Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia. Herufi O inawakilisha Nyota ya Mapacha
>HERUFI P
>Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi P inawakilisha Nyota ya Kaa
>HERUFI Q
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana. Herufi Q inawakilisha Nyota ya Simba
>HERUFI R
>Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani. Herufi R inawakilisha Nyota ya Mashuke
>HERUFI S
>Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa. Herufi S inawakilisha Nyota ya Mizani
>HERUFI T
>Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika. Herufi S inawakilisha Nyota ya Nge
>HERUFI U
>Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mshale.
>HERUFI V
>Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mbuzi.
>HERUFI W
>Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari. Herufi W inawakilisha Nyota ya Ndoo.
>HERUFI X
>Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi X inawakilisha Nyota ya Samaki.
>HERUFI Y (YASINTA)
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha. Herufi Y inawakilisha Nyota ya Punda

>HERUFI Z
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo. Herufi Z inawakilisha Nyota ya Ngombe.


Habari hii nimeipata Jamii Forum ......

Sunday, July 4, 2010

UJUMBE WA LEO:- MADIRISHA MANNE KATIKA MAISHA

Unajua na labda hutaki kuzingatia

Leo katika pitapita zangu nimepata kumsikiliza Mshairi mahiri wa Tanzania Mrisho Mpoto. Katika kumsikiliza maongezi yake ambayo yalifanyika na Bongo Tanzania TV 3/12/ 2009. Aliyatamka maneno haya ambayo katika maisha kuna milango yenye madirisha mnne. Nimeupenda sana usemi huu na nimeona nigawane na wenzangu na madirisha hayo ni:-



1. wewe unajua mimi sijui

2. Mimi najua wewe hujui

3. Wewe unajua mimi sijui

4. wewe hujui na mimi sijui.



Kwa hiyo ukijua ni diriasha gani zuri la kukufanya uishi vizuri na watu basi utaishi kwa raha mustarehe, shangwe na nderemo na mashasha katika nafsi yako.


NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII YA KWANZA YWA MWEZI HUU WA SABA NA/ TAFAKARI YA LEO: IMANI KATIKA NENO TAKATIFU


Nabii Eliya katika maombi

Baada ya kutafakari kwa kina nimepata wazo la kuanzisha kipengele cha Tafakari ya Leo, ambacho kitakuwa kikuzungumzia neno takatifu la Mungu. Kipengele hiki kitakuwa kikiwajia kila siku ya Jumamosi ambapo ni siku yangu ya kupumzika na kumtumikia Mwenye enzi Mungu.

Katika kukumbushana huko, nitaelekeza fikra zangu juu ya maandiko matakatifu na hata nukuu mbalimbali kutoka kwa Wanafilosofia waliowahi kuishi hapa duniani wakiwemo Manabii.

Jana nilishindwa kuweka kipengele hiki kutokana na mtandao kupata kwikwi. Lakini kwa kuwa leo mtandao umetulia ninawaletea kipengele hiki kama ifuatavyo, naomba tutafakari kwa pamoja:

Leo ninaanza na somo la imani, hebu tuangalie 1Wafalme 18:42, nitanukuu,
“Naye Eliya akamwambia Ahabu, Haya! Inuka ule, na unywe; kwani pana sauti ya mvua tele”

Mwisho wa kunukuu.

Kama tulivyosoma fungu hilo hapo juu, Nabii Eliya akimwambia Ahabu ainuke ale na anywe kwani pana sauti ya mvua tele.

Ukweli ni kwamba kulikuwa hakuna mvua, pia mawingu yalikuwa hayaashirii kuwepo kwa mvua, pia hata upepo ulikuwa hauvumi kuashiria kwamba kungenyesha mvua. Lakini Nabii huyu wa Mungu Eliya alisema, “Nasikia sauti ya mvua tele”

Kwa kauli hiyo ya Nabii Eliya inanionyesha kuwa katika swala la imani, kusikia ni dalili muhimu kabla ya kuona kile unachokitarajia.

Tatizo la kwa nini sisi tunakuwa na imani haba kiasi cha kutofanikiwa katika kila tulitendalo ni kutokana na kutaka kuona kile tunachokitarajia kabla ya kusikia kwanza.

Nabii Eliya Alisema kuna sauti ya mvua tele, hebu tuliangalie kwa makini neno “Sauti” kwa sababu neno sauti anazungumzia kelele na matokeo yake.

Pia ni vyema ukijua kwamba sauti aliyokuwa akiisikia sio halisi bali ilikuwa ni ya rohoni.
Katika biblia tunasoma kuwa Nabii Eliya alimwagiza mtumishi wake kwenda kuangalia iwapo kuna dalili ya mvua, na mtumishi huyo alikwenda mara sita kuangalia, lakini alirudi na jibu lile lile kuwa kulikuwa hakuna dalili ya mvua.

Labda wewe unayesoma hapa leo uko katika hali hiyo hiyo, umeshajaribu kila kitu na una imani katika kufikia malengo yako lakini imani yako imekuwa ni bure kabisa.

Hakuna kinachotokea na maisha yako yamekuwa ni yale yale, kama vile ilivyokuwa kwa mtumishi wa Nabii Eliya alivyokwenda kuangalia dalili ya mvua mara sita lakini akirudi na jibu lile lile la hakuna dalili ya mvua.

Labda kwa upande wako imekutokea katika kazi yako, biashara zako, ujuzi wako, elimu yako, na unaanza kupoteza imani kwa mungu au unafikiria kuachana na mungu na kutomwamini.

Nataka nikwambie leo hii kuwa kama imani yako ikisema ndio, hakika hata mungu hawezi kusema hapana.

Nabii Eliya alisema,… “Nasikia…” na hakusema….. “Naona….” Hii inaonyesha kuwa Nabii Eliya alikuwa anajua kanuni ya kuwa na imani.

Kwa hiyo na wewe ili dalili ya imani yako kufanya kazi ni lazima kwanza usikie ile dalili ya kupata majibu kutoka kwa mungu ni lazima ujiandae kuisikia dalili hiyo kutoka kwa mungu.

Lakini tatizo walilo nalo waumini wengi ni la kusikia. Katika biblia tunasoma katika Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”

Biblia haikusema kuwa “imani huja kwa kusikia neno” Kiasi gani utasikia inategemea na umbali unaoweza kuona.

Hebu tuangalie nyuma kidogo kwenye historia ya Abrahamu katika kitabu cha mwanzo 15:1. Mungu alimwambia Abrahamu “Usiogope Abrahamu, mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana”.

Lakini Abrahamu akamwambia mungu, “utanipa nini il hali sina hata mtoto”
Naamini kuwa tunafahamu kuwa hatimaye Abrahamu alikuja kupata mtoto.

Lakini hata hivyo kabla ya kupata mtoto, tuliona jinsi mungu alivyomchukuwa Abrahamu hadi ufukweni kuhesabu mchanga na pia alivyomchukuwa hadi nje wakati wa usiku na kumwambia ahesabu nyota. Unaweza kujiuliza kwa nini afanye yote hayo?

Naamini ni kwa sababu Mungu alitaka kubadili picha aliyokuwa nayo Abrahamu ya kutokuwa na mtoto.

Kwa somo hili naamini wote tumeona ni jinsi gani imani inavyoweza kufanya kazi iwapo tutafuata kanuni kama nilivyoeleza.

Tukutane Jumamosi ijayo……………

Mada hii nimeichukua kutoka kwenye kibaraza cha VUKANI, cha mdogo wangu Koero, nami nimevutiwa nayo nikaona sio vibaya kuirejea ili kujikumbusha. jumapili njema kwa wote.

Friday, July 2, 2010

Nawatakieni Ijumaa njema kwa wimbo huu!!



IJUMAA NJEMA WAPENDWA NA MWISHO WA JUMA MWEMA!!!!

Thursday, July 1, 2010

Tufungue mwezi huu wa saba nahawa Warembo wa kihimba/picha ya wiki hii!!

Kwa kweli ukitaka kupendeza ni lazima uwe mvumilivu. Angalia nywele/rasta za akina dada hawa. Halafu nimeipenda picha hii WAHIMBA wao hawahitaji nguo wapo kiasili kabisa.