Tuesday, June 8, 2010

UPENDO GANI HUU WA MAJI KUPWA MAJI KUJAA!!

Kwa kawaida sisi wanaadamu huwa hatuna hisia za aina moja wakati wote... kuna wakati tunakuwa na hisia za upendo kwa wake au waume zetu na wakati mwingine hujikuta tukiwa na hisia za chuki bila sababu. Kama vile bahari klupwa na kujaa , basi ndivyo zilivyo hisia zetu-

Je? twawezaje kupunguza hisia hizi za chuki kwa wenza wetu? Nasema kupunguza kwa sababu ni vigumu kuziondoa kabisa. Sisi tumeumbwa na hasira, hata Yesu pia alikuwa na hasira, na ndio maana alimwaga bidhaa za wale wajasiriamali kule hekaluni. Kwa sababu waligeuza hekalu lla kuabudia kuwa pango la wachuuzi. Je? tutawezaje kujiepusha na hasira?

10 comments:

Anonymous said...

Upendo na chuki ni kitu kimoja, ili upendo uwe upendo halisi ni lazima uzungukwe na chuki. kwani upendo usiozungukwa na chuki haufai hata kuitwa upendo, tunachotakiwa kutoa ni attention kwenye upendo na siyo kwenye chuki.
Kwa mfano
kama kusingekuwa na chuki basi tusingekuwa na upendo, utoke wapi?
ni sawa na usiku na mchana, bila kuwepo na usiku, tusingekuwa na mchana,
au kifo na uhai, bila kifo hakuna uhai,

watu wa utambuzi tunaita Ying na Yang.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

haSira ni muhimu sana kwetu, bila hasira basi maisha hayana maana. muhimu ni kuidhibiti hiyo hasira yenyewe, kuitawala isikutawale. ikiutawala utaishi maisha ya majuto ni mjukuuu

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

duh! Haya! kaazi kweli kweli!

hasi na chanya zote ni sawa tu ila tu kama huwezi kujiweka katika chanya zaidi utajuta

chib said...

Kamala, big up. Hasira haiepukiki. Ni wewe mwenyewe tu kuituliza

MARKUS MPANGALA said...

uzuri wa upendo ni ubaya wa chuki, na ubaya wa chuki ni uzuri wa upendo. Na ukichukia inawezekana inatokana na kujijengea mazingira kwamba una chuki. Na kama unakumbana na watu wanaokuonyesha chuki wakati unajulikana kwamba wewe ni bingwa wa upendo, kwa vyovyote utachukia au utakuwa na hasira. Wanasaikolojia wakati mwingine husema ukitaka kumfahamu mtu jaribu KUMDHAARAU kwani atajitahidi kila namna kukuonyesha yeye ni nani. Na endapo ukimpuuza zaidi utaona anachukia/anahasira. Kwahiyo ukamilisho wa upendo ni kitu kinachotoka kwa mwingine na chuki ni kitu kinachotoka kwa mwingine.

Ubaya wake ni pale mtu anaporuhusu chuki kumtawala na kujitapa yeye ni bwana/bibi chuki/hasira au upendo. HAPO NDIPO PENYE HEKIMA NA AKILI inahitaji kujiangalia zaidi kwakuwa hakuna umuhimu wa kuchukia/hasira.......

ngoja nikambie kwanza uwanjani najiskia kuchoka sana. haya kilau basi anuuuu!!

Simon Kitururu said...

Sijui KWANINI ila naamini kuwa HASI na CHANYA ni tofauti.

Kwa wasiojua kimaandishi:

HASI ni: -
CHANYA ni : +


Swali:

UPENDO GANI huu wa MAJI KUPWA na maji KUJAA ambao MUNGU wa KIKRISTO anaufuata kiasi kwamba inawezekana ukafuata ukristo mpaka dakika moja kabla HUJAFA maji ya kafanya KUPWA kimapenzi yake ukaenda MOTONI kama baazi ya WAPADRI, MAASKOFU, PAPA, wachungaji wafundishavyo?

Si inasemekana dakika ya mwisho wakati YESU anasulubiwa kuna mjanja aliyekuwa hafanyi mazuri ya KIYESUYESU aliokolewa palepale MSALABANI kama unaamini BIBLIA sio kitabu cha JUMA na ROZA?

Hivi kuna uwezekano MUNGU wamfuatao WAKRISTO staili yake ya upendo ni kama ya MAJI KUPWA na MAJI KUJAA na ujanja ni TAIMINGI(KIDOKEZO -taimingi ni kingereza ikiwa na maana kujulia muda) za unakufa wakati wa KUPWA kipendo au KUPWAA?

Nampenda YASINTA lakini ingawa sijawahikukutana naye na sijui penzi lake likikupwa inakuwaje.:-(

NI MTAZAMO tu huu kwa sauti na hata nisingeuandika hapa ningeuwaza.:-(

Anonymous said...

kazi kweli kweli, kila la heri na mapenzi ya mtindo wa bahari!!

Blackmannen said...

He he he he heeeee, wewe "Mtakatifu Simon Kitururu", bado hujatulia kabisa wewe. Wewe ni "Mtakatifu", lakini bado unamweka "Mawazoni" dada Yasinta?

Kwanza mbona hukuja "Bongocelebrity" kuelezea jopo gani la Maparoko waliokutakatifuzisha? Kasome sehemu ya "Mtakatifu Nyerere".

Lakini hata hivyo si kitu ni "Blackmannen - Mawazoni"

This Is Black=Blackmannen

Penina Simon said...

Yes Yasinta, sikubaliani nawe moja kwa moja.
Kama upendo upo kati yenu hasira haina nafasi, labda uhisi mwenza wako anafanya kinyume na mahusiano yenu.

Yasinta Ngonyani said...

Hakika katika ujumbe huu nimejifunza mengi ahsanteni sana maana kuna mengine nilikuwa sijayajua kabisa. Upendo Daima.