Thursday, June 24, 2010

Salaam kutoka Seminary ya Likonde!!

Jengo la Seminary kuu ya Likonde


Nimtume nani unatume mimi nitume bwana.
Leo nimetembelea Likonde Seminary na nimeona iwe picha ya wiki hii. Najua wengi mtakuwa na kumbukumbu nyingi kuhusu Likonde. Tukutane tena wakati mwingine.


9 comments:

Jacob Malihoja said...

Likonde mimi sijawahi kufika! ila nimefika Peramiho. Naifahamu Seminari ya Peramiho kwasababu niliwahi kutembelea mnyonga mara kadhaa kwahiyo nilikuwa nashukua Seminari na kukatisha katika barabara yao ya Lami na misitu yenye maelfu kwa malaki ya Popo iliyopo mbele Seminari! Misitu yenye miti ya aina mbali mbali yakiwemo Mapotopoto matunda ya asili yenye utamu kama Asali!!!

Unknown said...

Mimi hata hiyo Peramiho sijawahi fika. Siku moja nitatembelea huko bondeni na kujionea mwenyewe. Ahsante kwa taswira murua.

Maisara Wastara said...

Dada, nakutakia siku njema, na ahsante kwa picha nzuri.....

MARKUS MPANGALA said...

UMENIKUMBUSHA mbali kweli kweli enzi zileeee. we acha tu yaani kabla sijatua lUNDO SEKO. Ila mdogo wangu yupo Likonde seminari, naye anataka kutumiza ndoto.
mwaka 2005 nilikuwa Major Seminary pale Peramiho, niliongea na washkaji zangu, tulikumbuka mengi sana. Duh! enzi za kuvaa makanzu jamni we acha tu. enzi za kuongoza sala za zamu na Abate Lambert? kaka Malihoja, nakwambia misitu ni uhai, mimi napenda sana ile misitu ila popo ndiyo haooooo kama nini sijui. Umenikumbusha mbali sana. Ngoja nikaangalie picha zangu za jimboni Mbinga. aiseeeee Yasinta umenikuna sana sana

Anonymous said...

Asante kwa picha dada! pamoja na asante, naomba kukusahihisha mambo mawili muhimu. Seminari ya Likonde sio seminari kuu. Kusema Likonde ni Seminari kuu ni sawa na kuita Sekondari chuo kikuu. Seminari ya Likonde ni seminari ndogo, natumaini utasahihisha hilo. Jambo la pili, hiyo picha ya chini sio Seminari ya Likonde, hapo ni jimboni Mbinga na inaonyesha ni wakati wa sherehe fulani, au upadrisho au sherehe nyingine yeyote ile ambayo inakusanya mapdre karibu wote wa jimbo. Labda hiyo picha ya pili inaweza kuleta kumbukumbu ya Likonde endapo utaamua kuweka msisitizo wa wahudumu wa Likonde seminari ambao ni pamoja na mkuu wa shule (wa tano toka kulia katika huo msitari wa mbele ya mpiga picha. ukiondoa hizo kasoro, tunashukuru kwa picha. Labda kwa kujazia, kama hizo picha hukupiga wewe ni vema ukaweka nukuu ya mpiga picha, ni jambo la lazima sana hilo!!!

Matha Malima said...

asante kwa picha nzuri kwani umnikumbusha nyubani songea ndio kwetu mnafarijika sana ninapoona mazingira hayo. chao.

Yasinta Ngonyani said...

Napenda kuchukua nafasi hii na kuwashukuruni wote kwa kutochoka kutembela kibaraza hiki. Karibuni tena na tena.

paul luambano said...

big up sana lakini Likonde sio Seminari Kuu

Mbele said...

Nilisoma hapo, miaka ya 1967-70. Enzi zile seminari ya Likonde ilikuwa tishio Tanzania kwa kufaulu mitihani. Tulikuwa na bendi yetu, ambamo nilikuwa napiga "first trumpet," na tulikuwa tunachapisha jarida la historia lililoitwa "Our Past," chini ya mwalimu wetu Fr. Lambert Doerr OSB, ambaye baadaye alikuja kuwa "Abbot."