Tuesday, June 22, 2010

Je? barabara hii itakufikisha wapi??

Barabara hii imenikumbusha mengi sana wakati wa utoto /zamani mtu umechoka una mzigo kichwani na barabara unaiona ndefuuuuuu. Haya karibu ni wapi hapa?

11 comments:

Anonymous said...

mie napajua ila sisemi kwa vile sina kawaida ya kuwatajia majibu watu wengine. Kila mtu ajijue mwenyewe!!

chib said...

Hapo ni sehemu fulani hapa duniani, na wala sio Mars kama wengine wanavyofikiri

John Mwaipopo said...

uyole, mbeya. kule juu ni vilima vya isyonje kuelekea simambwe na uporoto.

Koero Mkundi said...

Hapo ni Korogwe, kuelekea kona za Msambiazi ili utokee mkomazi......LOL

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mh! nahisi kama ni mwitongo...lol!

chib said...

Bado nafikiri nipo sahihi, maana kila mtu anataja sehemu iliyopo duniani!!!

Baraka Chibiriti said...

Kwangu ni giza tu...Nitakupa mji dada Yasinta ili uitajie.

Maisara Wastara said...

Wote mmekosea.......
Hapo ni Mkwaja njia ya kuelekea Pangani

Fadhy Mtanga said...

mi ndo mwenye matokeo.

John Mwaipopo ndo kaongoza kwa kupatia jibu la kweli na kupata alama 83%

Ni kweli ni Uyole na unaitazama milima ya Uporoto lakini siyo Simambwe pale mlimani bali ni Iwalanje.

Niliipiga picha hiyo nikiwa nimesimama usawa wa kanisa Katoliki Uyole nikiwa naitazama Igawilo.

Hiyo ni barabara kuu inayokupeleka Tukuyu, Kyela na Malawi.

Picha imetunguliwa mwezi Aprili 2007.

Ahsante da Yasinta kwa kunishtua maana nilikuwa sifahamu kinachoendelea humu. Mambo ya weldi kapu aka Zakumi aka vuvuzela.

John Mwaipopo said...

fadhy ukiwa mwalimu wanafunzi watakukoma. 83 tu!

hakika mambo ya Kee Naaako!

Yasinta Ngonyani said...

Naona wote tumepata jibu kuwa ni Uyole. Na kaka John ulibaki kidogo tu kupata 100% kweli mtani Fadhy ni kiboko yaani 83 ty:-) Ahsanteni wengine wote makofi wa wa wa!!