Thursday, June 10, 2010

Jinsi lugha inavyotatanisha ukiwa mgeni!!!

Ngoja leo niwasimulia kajambo:- Siku moja nikiwa nimekaa nimetulia nikijisomea kitabu changu, mara akatoka kijana mdogo akinitazamana kwa huruma. Akaniambia NAAZIMA choo, nikabaki mdomo wazi , na nikamuuliza unaazima choo utanirudishia lini? Naye akabaki mdomo wazi huku akijifinyafinya kuonyesha amezidiwa sana na haja kubwa.

Nikaendelea kumwuuliza kwa nini asiingie ndani na kutumia choo na kuondokka ni lazima AKIAZIME? Akaniambia ndo alikuwa na maana hiyo kuwa ana-OMBA atumie. Nikaona hiii ni kaazi kweli kweli katika kuelewana. Sasa hapa ninachoomba kwa wewe msomaji uniambia kama nimekosea maana kwa ueleo wangu neno haya maana mimi nimeelewa hivi:- KU-AZIMA maana yake utarudisha tena na neno KU-OMBA maana huhitaji kurudisha. Swali:- Je kuna maana nyingine?

11 comments:

Subi Nukta said...

Naazima choo? Naomba choo? tehe, nadhani hapana.
Nadhani sentensi sahihi ilipaswa kuwa, 'naomba kujisaidia katika choo chako' au 'naomba kwenda haja chooni kwako/mwako' au 'tafadhali uniruhusu kutumia choo chako kujisaidia' nk.

Unknown said...

Inategemea na mahali kwani watu wengi wa mikoa ya kusini hutumia neno kuazima ikiwa na maana 'anatumia' na kuwa pale yeye si mkaazi. Maneno mara nyingi hutofautiana mahali na mahali. Mara nyingine lugha za makabila huingilia kati kwani watu hutafsiri maneno ya hizo lugha moja kwa moja kwenda kiswahili. Maneno haya hukubalika na wenyeji lakini kwa wengine hubaki mdomo wazi.

Lulu said...

"Naomba kutumia choo chako" Huwezi kuazima choo.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Labda angesema: Naomba sehemu ya kutupa UCHAFU wangu!!!!!! :-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mh, namboa nikae kimya kama vile sina cha kuongea

EDNA said...

Haahaaa kinachoazimwa lazima kirudishwe,naona alikosea tuu kujieleza.

Anonymous said...

MIMI NAONA HAJAKOSEA KWASABABU KWA MDA HUO ANAAZIMA CHOO KWA VILE ATAKUWA ANAKIMILIKI YEYE KWA MDA HUU BAADA YA MUDA ATAACHA KWAHIYO NI KAMA AMEKURUDISHIA MIMI NAONA HAJAKOSEA HATAKIDOGO NI SISI TU NDIO HATUJUI KISWAHILI SAHIHI YEYE KATUMIA SAHIHI LAKINI TATIZO LETU HATUJUI KAMA HATUELEWI

Anonymous said...

msizunguke saana,angesema nataka kunya kwenye choo chako

Mija Shija Sayi said...

Anony wa June 10, 2010 6:00 PM,ameongea yote. Ninamuunga mkono.

Blackmannen said...

Kiswahili ni lugha ngumu sana, na inastawi kama mmea kila siku kutegemea na sehemu unayokaa.

Maneno mengi mliyoyasema hapo juu kama utayazungumza hapo Mtaani kwetu "Buguruni-Malapa", watu watashtuka na kukuomba ufafanuzi zaidi.

Mtu huwezi kusema "...chooni kwako" au "...chooni mwako". Mtu sema vyote, lakini usiongeze neno "kwako" wala "mwako", maana wengi watakukaribisha kwao kwa kugombewa kama mpira wa kona.

Mimi nakubaliana kwa asilimia miamoja na "Mfalme Mrope", kasema vizuri sana.

Kama huyo mgeni angesema "naomba kwenda chooni au kujisaidia", isingeleta mtafaruku wa aina yoyote. Hata vijana wa Mtaani kwetu wangeelewa bila maswali na wangemwonyesha bomba la maji na kopo lilipo.

It's Great To Be Black=Blackmannen

Anonymous said...

nathani alikuwa anaazima pot