Sunday, June 13, 2010

Iweje tujitie kitanzi wenyewe?

Watu tuliojitambua tunaishi leo sio jana ambayo imeshapita na sio kesho ambayo sio yetu. Ishi leo sasa hivi ndio yako. Je? Ulishawahi kujiuliza mapungufu ya Dini juu ya mapenzi? Wakrito, NDOA YA MILELE. Padre au Askofu anajua wanaume na wake wakorofi. Waislam nao eti kuoa wake 4 ruksa. Wanajua wivu au ubabe ambao umetawala katika ndoa? Kuwa huru usitishwe na sheria hewa za dini. Usifujwe kwenye ndoa na mumeo au mkeo kwa kisingizio cha dini, ishi huru. Dini ni maandiko tu. Hata wewe kuandika unaweza. NAWATAKIENI DOMINIKA NJEMA WOTE

17 comments:

Anonymous said...

leo umeamua kuchokonoa nyongo eeh? nhe he, nimependa uthubutu na ujasiri wako katika hili, safi sana, nasema, saaafi sana! I wish wale wasomaji wa blogu maarufu wangeona hii posti, kusingekosekana maoni 100 mchanyato.

SN said...

Kweli, mimi sipingi wala kuunga mkono, ila nitaongeza swali. Ni kama nundu juu ya nundu.

Hivi, hivi vitabu vyetu vya dini viliandikwa na watu walioishi wakati wa zama za utumwa. Kwa maneno mengine, wakati ule biashara ya utumwa ilikuwa sawa machoni mwa watu.

Sasa, swali ni hivi:

Mbona - mfano, Yesu au Nabii Issa - hajawahi kukemea biashara ya utumwa? Vipi, na watume au manabii wengine je?

Anonymous said...

cheza na vingine siyo na vitabu vya mungu,Kwa nini technology inataka kumchokonoa mungu? Mke ni mmoja ukizidiwa ongeza wa pli basi.harafu watofautiane miaka yaani under 18 na above. aise angalia!

Anonymous said...

nisawazishe ukisema ETI kwa lugha ya kiswahili ni kama huna hakika nolo jambo
kwa hivo sio eti wake 4 ruksa
unajuwa sababu moja ya kuwa ruksa
kuowa 4 ni wanaume wanatafautiyana ki nguvu za kiume wengine wanaweza maliza kuku 2 na chips na wengine ni kuku mmoja yupo hoi

Ramson said...

Ingawa siamini sana katika dini, lakini naamini wale wenye kitabu kilichoaidhinisha wake wanne waliona mbali.

Kama ukingalia kitakwimu, wanawake ni wengi sana ukilinganisha na wanaume hapa duniani.

Na hata ukitoa wale wanaume mashoga, bado utabaki na idadi ya wanawake ya kutosha ukilinganisha na wanaume.

Hii ina maana kwamba, kama wanaume wote duniani wakiamua kuoa mke mmoja ina maana kwamba kutakuwa na idadi ya kutosha ya wanawake ambao hawana wanaume wa kuwaoa.

Sisiti kusema kuwa hiyo ndiyo sababu ya kuwa na makahaba na wale waviziaji wa waume za watu almaarufu kama Nyumba ndogo.

Kuhusu kuzidiana nguvu katika swala la la kufanya mapenzi kati ya mtu na mtu (Sexual Motive)halipo kwa wanaume pekee bali pia wapo wanawake wenye tatizo hilo. Sasa je nao wanaruhusiwa kuolewa na wanaume wangapi?

Hiyo ni changamoto nawaachia wadau nao walete changamoto zao hapa.

Anonymous said...

Ranson anasema
wanawake Sasa je nao wanaruhusiwa kuolewa na wanaume wangapi?

wanawake hakuna dini inamruhusu kuolewa na zaidi ya mume mmoja

ili tusipate taabu ya kumtafuta babawa mtoto atakaezaliwa

sasa waume watatu tutajuwaje mtoto wa nani
wacha nikupe mfano mmoja chukuwa maziwa namaji na juice halafu yaweke pahala pamoja kwenye glass

halafu koroga sasa yatowe maziwa peke yake kama utaweza itakuwa suala lako limejibiwa

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hii mineno ya hayati Munga huwa inanichengua sana. Ntalifanyia kazi ili nami nivute kumi na ushei ndani ya nyumba....lol!

SN: Labda wakati wao hakukuwa na utumwa...lol!

Anonymous said...

Chacha, katika Biblia Yesu alitoa mifano mingi juu y Watumwa.

Kwa kifupi Manabii wote waliujua utumwa na waliuridhia.

Maandiko ya hivyo vitabu vyao yanadhihirisha ukweli huo!

Lulu said...

Dah!!! Yasinta mkatoliki safi lakini leo umeonyesha "uthubutu" wa hali ya juu!!! Nakuunga mkono ndoa ni mapenzi na makaubaliano kama mapenzi yakiisha its obvious makubaliano hayatakuwepo tena. Mke/ Mume achia ngazi angalia ustaarabu mwingine. Hivi Dunia ya leo madada wa kisasa wameenda shule bado wanakubali uke wenza? Wameona kwa mke wa Zuma yaliyotokea? Sasa hata maradhi yanabebeka kama mimba tu. Kazi kwenu kama mwakubali uke wenza. Hivi siku mume yupo kwa mke mwenzio unajua kabisa kaenda chovya akirudi nawe wamuachia achovye kwako? Haaaa haa na wivu wangu nisingeweza.

Lulu said...

Chacha kama nakuona unavyofurahia kuongeza mke.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

@Lulu: akiwa kwako ni wako

Akitoka tu langoni si wako huyo tena atiii...lol!

Yep furaha mtindo mmoja, yaani we acha tu

Anonymous said...

Hii ni kwa mkatoliki aliyeasi! mkatoliki safi hawezi kuropoka hivi!! huku ni kutetea uzinzi kama hamjafunga ndoa inayotambuliwa na kanisa!!!

Anonymous said...

Wazinifu safi utawajua tu! hizi blog zenu hizi zitumieni vizuri "sheria hewa za dini mnazijua ninyi?" kwa mtaji huu kila mtu ajiwekee kasheria kake!! sikutarajia kama huyo anayejiita mkristo anaweza kuja na habari kama hii!!!

Anonymous said...

du! ndugu kama weye wazini haina haja ya kufundisha na wengine. ingetosha tu ukabaki na imani au msimamo wako moyoni hasa kama unajua fika huo msimamo wako unahusisha imani za watu!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yaone yanaamini dini

Penina Simon said...

Kha! na kweli dini na ndoa ni shughuli, ila nafurahi kwa vile mbinguni hakutakuwa na kuoa wala kuolewa, vinginevyo ingekuwa kasheshe

Mija Shija Sayi said...

Yaani ingekuwa kasheshe, kasheshe... Penina umejisemea ukweli.