Monday, July 25, 2016

NASIKITIKA SANA MWAKA HUU BUSTANI YETU HAISTAWI KAMA MIAKA MINGINE....

 ...Nimejaribu mara zaidi ya mara sita kupanda mbegu za mbogamboga kama nifanyavyo lakini zimenigomea. Nikaona labda nijaribu kupanda kwenye kopo nikafanikiwa ndo hili/ huu mmea wa boga muuonao:-(. Kwanza nilifikiri ardhi  imechoka nikaweka mbolea lakini wapi....

 Viazi mviringo afadhali vimekubali na kama muonavyo nitavuna karibuni maana majani yameanza kukauka pia....
 Nikajaribu na njegere ...aaahhh mama yangu nusu nilie ndo kama muonavyo sijui kama tutakula.   pia kumezuka konokono wanakula mimea yotr walayo binadamu kwa hiyo mie nikipanda ikijitokeza tu wao wanafyeka/kula tu....Inakatisha tamaa
Na mwisho nikaona nijaribu kutumia makopo/ndoo ili kuweza kupanda  na kuona kama itakuwaje matokeo  yake ni haya Nyanya,  pilipili, pilipili hoho na maua  na kuviweka kwenye varanda vimekubali. Lakini sasa nitakulaje viungo tu bila mboga na ugali?:-)
Naomba kwa yeyote mwenye ushauri anishauri la kufanya.... JUMATATU NJEMA!

2 comments:

Anonymous said...

Duh pole sana kwa kuhangaikia bustani yetu ila na mazao yamegoma! Sasa itakuwa ni ubaridi baridi bado iko namaanisha hali ya hewa si rafiki? Au kweli udongo umechokaaaa? Au ni hao wadudu konokono? Jamani jamani viachie bustani yetu. Ila nakupongeza kwa kutokata tamaa na kutumia makopo kuendeleza kilimo kwanza ama kweli mtu kwao, haya tutakula hivyo vitakavyopatikana. Karibu tz ardhi kubwaaaa na hali ya hewa rafiki kwa mazao.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana kidogo napata hamu tena ya kutafuta ni mbinu gani nifanye maana nina hamu sana ya mchicha na mboga nyingine ambazo ni tamu kuzilima mwenyewe.