Wednesday, January 15, 2014

WANAWAKE NA HISIA ZA USALITI: ZIJUE DALILI ZAKE!!

Inawezekana ukawa ni mke wa mtu au una mpenzi wako ambaye mna matarajio ya kufunga ndoa na kuishi pamoja. Kuna wakati unaweza kujaribiwa na kujikuta ukikabiliwa na hatari ya kumsaliti mpenzi wako. Kujaribiwa huko kunaweza kukutokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na maeneo yako ya kazi au mahali unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kwa mfano inaweza ikatokea umefahamiana na mwanaume mahali pako pa kazi, anaweza kuwa ni mteja au mfanyakazi mwenzio. Inatokea siku moja anakualika kwa ajili ya chakula cha mchana, baada ya mtoko huo, unajisikia kutoka naye kwa mara nyingine…………………
Kutoka kwenu mara kwa mara kwenda kupata chakula cha mchana, unagundua kwamba huyu bwana ni mtu mwenye kiwango cha juu ya usikivu, katika mazungumzo yenu anaonekana sana kwamba ni mwelewa na mwenye subira. Hana papara katika kuzungumza na mara nyingi huwa ni msikilizaji. Huyu unaweza kumwita rafiki ingawa ni wa jinsia tofauti, (Sidhani kama ni dhambi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti……!) Kuna kitu wenzetu wazungu wanakiita Emotional infidelity, kwa tafsiri yangu naweza kusema ni hisia za usaliti katika mapenzi. Maana yake ni kwamba unaruhusu mtu mwingine wa jinsi tofauti azibe pengo la hisia ambalo lingetakiwa lizibwe na mpenzi wako au mume wako. Kama inavyofahamika kwamba wanawake ni viumbe wa hisia, wanapenda sana kusikilizwa, na wanapenda kuona wapenzi wao au waume wao wanawasikiliza. Inapotokea hitaji hilo halitekelezwi na mpenzi au mume wake, basi ni rahisi sana atakapotokea mtu mwingine ambaye bila kujua akamudu kuziba pengo hilo kuvutiwa naye na kuhitaji kuwa naye karibu mara kwa mara.
Hapa chini nitazitaja dalili ambazo zitakuonyesha kwamba ukaribu wako na huyo rafiki utakupelekea kuisaliti ndoa yako:
1. Unatamani sana kumuona ukiwa na shauku kubwa ya kuwa naye karibuna kutumia muda mwingi kuwa naye
2. Unajikuta ukichagua mavazi na kujikagua sana ukijiuliza jinsiatakavyo vutiwa na mavazi yako pale atakapokuona
3. Unapokuwa naye unajikuta ukimweleza matatizo ya mahusiano yako na mpenzi wako au mumeo
4. Unajikuta ukimgusa gusa wakati mkiongea au kufanya naye utani unaoweza kupeleka ujumbe tofauti kwake kwamba labda umevutiwa naye kimapenzi
5. Unawsiliana naye kwanza kabla ya kuwasiliana na mpenzi wako au mumeo pale unapokabiliwa na jambo lolote lenye kutatiza na linalohitaji msaada wa haraka au ushauri
6. Unajikuta ukiwaza jinsi gani ungekuwa na amani iwapo ungekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi au ndoa
7. Inawezekana ukawa unamzuingumzia sana kwa mwenzi wako au kwa marafiki zako, au inawezekana ukawa humzungumzii kabisaaa na kuficha urafiki wenu.
8. Unajitahidi sana kuficha urafiki wenu na kutomzunguimzia rafiki huyo kwa mwenzi wako kwa sababu unajua kwamba jambo hilo linaweza kukuletea balaa.
Kwa ujumla unapojikuta umempata rafiki wa jinsia tofauti na yako halafu ukahisi kulipukwa na moyo juu yake zikiwemo dalili nilizozitaja hapo juu, basi ujue uhusiano wako na mume au mpenzi wako uko mashakani. Usipokuwa makini utamsaliti.
Habari/mada hii nimetumiwa na mkereketwa/msomaji wa Maisha na Mafanikio kwa kutaka tu mimi nisome lakini mimi nimeona ina mafundisho ndani yake nikaona ni bora niiweke hapa ili wengi wafaidike na ELIMU hii.

3 comments:

Koero Mkundi said...

Mada imetulia dada na nimeipenda. Kusema kweli mtihani huu unawapata si wanawake pekee bali pia wanaume sema kwa asilimia wanawake wanaongoza kwenye usaliti wa kihisia kutokana na mahusiano yao na wenzi wao kuwa na utupu wa kihisia na ndipo hapo atakapojitokeza mwanaume atakayeziba hilo pengo mwanamke anajikuta akitekwa kihisia kiasi ambacho asipokuwa makini anaweza kusaliti ushusiano wake na mwenzi wake.

Ahsante sana dada kwa mada yako nzuri ambayo imeniibua kutoka mafichoni.

Baadaye nitakutafuta mtandaoni tu chat kidogo maana niliku miss sana dada yangu.

Yasinta Ngonyani said...

Duh! Kweli hii mada imekuibua kutoka mafichoni mno. ..nakubaliana nawe si wanawake tu ila wanawake ni dhaifu sana kwa hisia ....na mara nyingi huwa hizo hisia zinapinzwa...nakysubiri kwa hamu kwani nami nimekumiss kuliko maelezo...

sam mbogo said...

Mada ni nzuri kimtazamo kwa huyo aliye kutumia namsifu kwa jinsi alivyo weza kujitambua na kutafakari wajibu wa kila mtu katika mapenzi iwe mke au mume.kwa mtazamo wangu kila kitu kina sababu yake au chanzo chake.sipendi kutumia neno kusaliti kwa msaliti au usaliti katika mapenzi sina hakika kama ni neno sahii kuli tumia. mimi ningependa kutumia neno mapungufu au udhaifu wetu kina kaka na dada katika mahusiano/mapenzi. kwa hiyo ukiona kunatatizo la kiusaliti/udhaifu katika mahusiano pamoja na mifano yote uliyo toa kama vishawishi vya kukufanya uingie kimapenzi na huyo jamaa anaye kusikiliza nk,sidhani nikosa kwani huo ndo ukweli mumeo hana sifa hizo/rafiki,kwa hiyo yawezekana ushajaribu kimaongezi na mumeo/rafiki ili awe na mahusiano kam ya hyo jamaa lakini hukusikilizwa.hivyo naona nibora kuisikiliza nafsi yako inakwa mbia vipi nakama unaona huo ndo ushauri mzuri na unajisikia huru sidhani kama ni usaliti.kaka s