Tuesday, January 14, 2014

NIMEOTA NDOTO KUWA NIPO LUNDO NA KINGOLI KWENYE SHAMBA LA MPUNGA NALINDA ILI NDEGE WASILE NA PIA NAVUNA MPUNGA...

 Hapa ni mwezi wa nne mpunga huwa unakuwa umekomaa kiasi hiki kwa hiyo walaji ni wengi kama vile ndege...Kwa hiyo kwa kuokoa mpunga ni lazima kila siku kwenda shambani kulinda/kufukuzia ndege..Duh nimefanya kazi hii ...mpaka sasa naota ndoto--Maisha ya zamani kweli ni dhahabu.
Hapa mpunga umeshakauka ni mwezi wa sita na ni wakati wa kuvuna sasa kula ubwabwa/wali...Sijui kati ya hawa nipo wapi?..Mnaniona au?...Kuvuna ni raha zaidi kuliko kulinda ndege:-)KILA LA KHERI NA LOLOTE UFANYALO:-)

2 comments:

Anonymous said...

Da Yasinta! Mimi nahisi ni wewe mwenye gauni nyekundu. Sasa vipi, ubwabwa teyari? By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Hahaaaa! kaka Salumu eti ni mimi huyu labda:-)...we njo tu ubwabwa tayari kabisa...