Saturday, January 4, 2014

LEO NI SIKU YANGU YA KUZALIWA:-)

Siku  ya Ijumaa tarehe 5/1/1973 Mama na Baba Ngonyani walibarikiwa kumpata mtoto wa kike. Na Wakamwita mtoto huyu YASINTA. Na leo ile siku imejirudia tena ila leo ni Jumapili. Napenda kuwashukuru wazaz/walezi wangu kwa kunitunza/kunilea na sasa nimekuwa MAMA. Namshukuru kwa kuniepusha na mambo mabaya, magonjwa na pia vishawishi. Pia napenda KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU kwa kunilinda na leo natimiza miaka tena. Na halafu napenda kuwapa HERI YA KUZALIWA wote waliozaliwa mwezi huu waliotimiza tayari miaka na watakaotimiza siku zijazo.. Nachukua nafasi hii kuwashukuru WASOMAJI WOTE WA MAISHA NA MAFANIKIO KWA KUTONICHOKA. Mmenitia nguvu sana bila ninyi isingewezekana. 

NA AHSANTE SANA KWA MWAKA 2013. JUMAPILI NJEMA NA NASEMA NAWAPENDENI SANA:-)....AHSANTENI WOTE.

19 comments:

Anonymous said...

Happy Birthday to Yasinta and many years to come! By Salumu

Anonymous said...

HAPPY BIRTHDAY YASINTA. MUNGU AZIDI KUKUBARIKI JINSI UNAVYOANZA KUZEEKA.UBARIKIWE.

Mija Shija Sayi said...

Hongera Yasinta, Mungu azidi kuwa nawe na akupe miaka mingine miiingi ya kuishi..

Happy birthday!

Ng'wanaMbiti said...

Happy birthday Da Yasinta

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salum! Ahsante sana.

Usiye na jina...ahsante ni kweli nazeeeka:-D
Mija ....ahsante ndugu yangu

WanaMbiti ...ahsante
Kaka wanaMbinti...ahsante


Kaka

Mija....akubariki nawe pia nadhani umeniekewa:-D

sam mbogo said...

Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa.kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kaka Sam...:-D

EDNA said...

Hongera kwa siku ya kuzaliwa dada, Mungu akupe maisha marefu na afya tele.

Yasinta Ngonyani said...

Edna ! Ahsante sana.

Anonymous said...

Unazeeka kiumri, ila muonekano hapana hata kidogo, bado unaonekana mdogo sana! niliendakia unazeeka nimeongezea nilimaanisha kwenye miaka. Bado unaonekana kama umemaliza la saba vile! Happy birthday Yasinta.

NN Mhango said...

Pokea diapers wipers and shawls kwa sana toka kwangu da Yacinta. Happy Birthday to youuuuuuuuuuuuuuuu!

Manka said...

Heri ya siku yako ya kuzaliwa Dada Yasinta,Mwenyenzi Mungu akupe maisha marefu na yenye baraka tele.xx

Nancy Msangi said...

Happy birthday Da Yasinta Mungu akupe Maisha marefu. Amina..

John Fisher Kanene said...

Dear Yasinta,
Happy belated birthday wishes. I wish you a blessed future full of joy and happiness. May have many more happy returns.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina nimekuelewa ..Ahsante..ila mmhhh darasa la saba kweli???

Mwl. Mhango! Nimezipokea kwa mikono miwili huko nimepiga na goti:-)

Manka! Ahsante ndugu yangu.

Nancy! Ahsante namshukuru Mungu kwa kweli.

Brother John! Thank you very much.

Mwanasosholojia said...

Happy belated birthday Yasi. Uzidi kuishi miaka mingi ushuhudie vitukuu vya wajukuu zako watakaokuja...:-)

Yasinta Ngonyani said...

Kaka M. Ahsante sana ila du mpaka kuviona vitukuu haya macho yataona kweli..LOL

Juma Thomas Nyumayo said...

Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa, zaidi ni staili ulivyoipamba kwa maneno yenye mvuto, matamu kama asali na kueleweka umuhimu wa siku yenyewe na kazi kubwa iliyofanywa na wazazi walezi kwa msaada wa muumba wetu wenyewe. Hongera sana. Pamoja na kuchelewa kuziweka pongezi hizo hapa, naamini utazipokea kwa moyo mweupe, kofia mkononi.

Yasinta Ngonyani said...

Mlongo wangu Nyumayo...wala hujachelewa. Pongezi zimepokelewa kwa mikono miwili na goti zimepigiwa. Usengwili.