Sunday, January 19, 2014

MAOMBI YANGU YA JUMAPILI YA LEO NI KAMA YAFUATAYO.....

Mwenyezi Mungu nakuomba ulisikie ombi langu. Nakubali kwamba mimi ni mtenda dhambi. Na ninaamini ulimtuma Yesu Kristo kuniokoa, ninamkubali Yesu kama Bwana na Mkombozi wangu. Nisamehe dhambi zangu unifanye safi. Nipe nguvu za kutembea katika njia zake. Naomba hivi kwa jina la Yesu Kristo. AMINA...,,,KWA MAOMBI YANGU HAYA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII IWE YA UPENDO NA FURAHA. jUMAPILI NJEMA KWA WOTE.

5 comments:

Anonymous said...

Da Yasinta mbona mbahiri sana. Tuombee na sisi! By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu...usikondo jumapili ijayo itakuwa zamu yenu...hata hivi ni sala/maombi ya wote....ahsante kwa kuliona hili..

NN Mhango said...

Amina dada akufanye uwe safi na kutembea kwenye njia zake akiwa bwana wako. Amina kwa saaaana.

Anonymous said...

Kaka Salum hujui kuwa kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe mbele za Mungu, na kila mtu atatoa habari zake mwenyewe na siku hiyo itafika! Jiombee kwani Yasinta ameomba maombi ya kutubu sasa iweje atubu on our behalf? jamani namtetea kuwa haiwezekani! Maombi mengine sawa ila ya kutubu inabidi kila mtu ajiombee na kuubeba msalaba wake mwenyewe kwa yake mtu aliyofanya. Samahani wandugu nadhani sijakwaza mtu.

Yasinta Ngonyani said...

Prof. Mhango. Amina.

usiye na jina ni kweli kila mtu ataubeba mzigo wake mwenywe...lakini pia waweza kuwaombea na wengine si mbaya...na wala hujamkwaza mtu hapa.