Saturday, January 18, 2014

JUMAMOSI NA MAPUNZIKO MEMA KWA WOTE.

Nadhani wengi tunakumbuka ilivyokuwa enzi za mababu zetu...na pia miaka ya 1980 mpka 1990..Kanisa moja, shule moja rais mmoja Chama kimoja na pia kula na kunywa pamoja na sahani moja na kikombe/robo/kichonjo kimoja. Lakini sasa  mambo haya hakuna kabisa inasikitisha sana. JUMAMOSI NJEMA NDUGU ZANGUNI...PIA KUMBUKENI POMBE SI MAJI....:-) TARATIBU

5 comments:

Anonymous said...

Ni kweli kabisa ila kwa miaka hii na jinsi magonjwa ya milipuko inavyoongezeka kula kutumia kikombe kimoja, sahani moja nk haiwezekani vinginevyo ni kujiweka kwenye hatari za kupata magonjwa. Zamani haikuwa hivyo sana, magonjwa ni mengi mno kwa sasa.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina! Je? ndo kusema miaka ile kulikuwa na usalama/ustaarabu zaidi kuliko miaka hii? Na je? kwa nini unafikiri imekuwa hivi?

Anonymous said...

Aisee hata mimi nasikitika sana ninapokumbuka mambo haya, kweli kipindi kile kilikuwa ni cha "dhahabu" kamwe hakitoweza kujirudia tena, wala sidhani kama ni shauri ya magonjwa wala sijui kitu gani, ni kutokana tu na huu utandawazi, wenye roho ya chuki, ubinafsi na roho mbaya, enzi zile za ujamaa kila kitu kilikuwa shwari.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Lazima utakumbuka tu hayo maisha hata kama hatukuwa na vitu vingi. Tulikuwa na utu na furaha. Juzi nilipata vitabu toka nyumbani vinavyotumika kufunishia Kiswahili shule za msingi. Nilitamani kulia maana ni upuuzi mtupu.
Leo tunatawaliwa na mafisadi, tunaishi kama mafisi na kufikiri kama mufilis tukigawa taifa kwa wachukuaji wanaoitwa wawekezaji. Tumeshikilia uchuuzi wa roho za wenzetu tuliokuwa nao wamoja zama za ujamaa na kujitegemea uliouawa na kuingizwa Uhujumaa na Kujimegea.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye ya jina wa 3:50PM.. naweza kukubaliana nawe ni kwamba kwa sasa wenye roho ya chuki, ubinasi na roho mbaya ni wengi sana si kama enzi zile yaani ujamaa ulijenga udugu sana.
Mwl. Mhango! Kusahau maisha yale si rahisi utakayesahau basi itakuwa hajayapitia kwa ukweli. Pole kwa hivyo vitabu nitakusaidia kwa kila niwezavyo uvipate..tatizo tunaishi mbalimbali ungefika hapa maktaba yangu ya kiswahili na kuchagua tu:-)