Monday, December 2, 2013

AKIBA HAIOZI HAPA MVUA IKIKOLEA HAKUNA SHIDA HAPA!!!

Ni Jumatatu ya kwanza ya mwezi huu nami nimeona tuanza kihivi. Akiba haiozi si mnajua mvua zikianza. Ila hapa kajiandaa haswaa hakuna shida kwa kweli.......NAWATAKIENI JUMATATU NJEMA NA MWANZO MWEMA WA JUMA. TUPO PAMOJA...KAPULYA/KADALA:-)

3 comments:

ray njau said...

Hai,hai nawapa hai na mzidi kuwa hai maana bila uhai hakuna kupeana hai.Hai,hai,hai!!!Hili ni wazo ndani ya wazo katika mawazo ya msingi yenye ushauri wenye manufaa kwa jamii.Acha mwenye masikio ayasikie maneno ya Yasinta.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! yaani hapo nimekumbuka enzi hizooo. Wakati wa masika wewee mtu anaweza kushinda njaa kama hujaweka akiba ya kuni. Msimu huu nauheshimu sana.

Salehe Msanda said...

Habari!
Msemo huu wa akiba haiozi mimi unaniaminisha kuwa toka Enzi hizo babu na bibi zetu walikuwa wanafahamu umuhimu wa kuweka akiba kwa ajili ya kesho na kesho kutwa. Hii Maana yake kuwa tunaasilii ya kujua kuweka akiba. sasa inakuaje katika suala la Pesa tuliowengii tunashindwa kuweka pesa kwa ajili ya matumizi ya kesho na kuwekeza katika maeneo yanaweza kutupatia kipato? Badala yake katika suala hili hata watumishi wa umma kwao ni Mtihani Mkubwa.
Nadhani tunaponzwa na kuishi kwa Utashi na kwa kuwa pesa ina tabia ya kutokutosha na kumaliza kiu kuna kazi kubwa k ufikia katika kuwashawishi waliowengi umuhimu wa kuweka akiba ili Msemo wa akiba haiozi uendelee kuwa na maaana kama ilivyokuwa tangu Enzi za babu na bibi zetu