Friday, February 25, 2011

PICHA YA WIKI:- DAIMA KUNA KUWA NA UFUMBUZI!!!!

Harusi yako haiwezi kushindikana kwa sababu ya keki. Daima kuna kuwa na ufumbuzi.Hebu angalia hiyo picha hapo juu. HAKUNA LISILOWEZEKANA:-)
NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA!!!!

11 comments:

Anonymous said...

Safi sana, ni ubunifu mzuri.

Mzee wa Changamoto said...

Mimi nadhani watu hawawezi kushindwa kuwa katika NDOA eti kwa kuwa hawawezi kufanya HARUSI.
Harusi na NDOA ni vitu viwili tofauti na wala havitegemeani.
Na havina ushirikiano hata kidogo (zaidi ya kulazimishwa kushirikiana).
Ndio maana HARUSI ZOTE HUFANANA japo KILA NDOA NI YA KIPEKEE.
Nadhani jambo la kwanza ni kuwa UNAWEZA KUWA NA NDOA NZURI BILA HATA KUFIKIRIA HARUSI. Kisha ndio tuseme hata ukifikiria harusi, si lazima uwe na sherehe,
na ukifikiria sherehe si lazima uwe na watu wengi,
na ukiwa nao, si lazima wale, na ukiamua kula si lazima wale kile wanachotaka ama wanachokula(ga) kwingine,
na hata wakila hicho, si lazima kiwe kama walichozoea,
NDIO MAANA.... hata MABOGA hutumika badala ya keki.
Ni ISHARA kuliko LADHA

Aaaaaaaahhhhhh
Nawaza kwa sauti tu

Mtesuka said...

Asante dada, hiyo ndiyo elimu tunayohitaji.Asante Mzee wa Changamoto, walao nimeelewa kuwa HARUSI ni tangazo tu (territorial decree) la NDOA.

EDNA said...

Ubunifu wa hali juu,kweli hakuna lisilowezekana...

MissPosh said...

kweli yasinta hakuna lisilo wezekana nimeipenda hio cake.

Rachel Siwa said...

Imekaa vyema na Hrusi imepita!!!!.

Celestina said...

Yeah dada hakuna linalosindikana wengine waliweka ndafu ya kuu.lakin kwani lazima kukawa na keki siku ya harusi?

Mija Shija Sayi said...

Si mchezo!! Yasinta sikuwezi dada...

Ubarikiwe sana.

Simon Kitururu said...

@Nafagilia kweli pointi za Papaa Mubelwa a.k.a Rasta MUBELWA BANDIO a.k.a Mzee wa Changa Moto !:-(

Anonymous said...

umenikumbusha,nilifanya sherehe ya kubatiza mwanangu,badala ya keki ilikuwa tikitimagi.mc baadaye aliniuliza kwanini tikitimaji? jibu lilikuwa hivi.nilimwambia kabla ya mimi kujuwa keki sherehe zilifana,bila hiyo keki,keki/tikiti vyote nichakula.si dhambi wala kosa kwenye sherehe badalaya keki ukatumia chakula chochote ilimradi kinalika na umekichagua wewe.wengi tu baada sherehe na hata wakati wa maandalizi hawakuelewa kwanini ghalama za keki haziku tajwa, na walipo kuwawanakumbushia niliwajibu, hakuna keki tutakula tunda tikitimaji.kaka s

penina said...

mbona kama bibi harusi anaonekana mtoto mdogo au?