Monday, February 28, 2011

MWANAFUNZI WA MIAKA 12 KUWA MKE WA TATU WA MZEE VISENTI HAULE

Habari hii imenigusa sana sana sanaaaaaaa na nimeona niiweke hapa Maisha na mafanikio ili tuweza kujadili pia kwa pamoja. Jamani hivi SHERIA zinatungwa ili iweje??? Baada ya kusoma habari hii nimekuwa ninajiuliza:- Hivi huu ni mwisho wa dunia? Au wanawake wamekwisha? Miaka 12 kuanza maisha ya ndoa halafu mke wa tatu kweli huu ni uungwana/utu kweli?
Makala hii nimeipata hapa kwani naamini wote tuna nia ya kueleimisha jamii.
Haya hapa ni habari yenyewe tuwe pamoja.

Binti wa miaka 12 katikati Veronika Charlle wa darasa la tano, akiwa na mwenye kiti wa kijiji cha Sinai Talisis Mkanula na mhudumu wa afya msingi Christina Njovu.walijaribu kumsaidia mtoto huyo lakini kukawa na urasimu wa kushindwa kumchukulia hatua mtuhumiwa Bwana Vinsenti Haule kwa kesi ya ubakaji maana huyu mtoto ni sawa na mjukuu wake.

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Vinsenti Haule mkazi wa kijiji cha Sinai Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma ambaye ana wake wawili amemuoa mwanafunzi wa darasa la tano wa shule ya msingi Nakahuga Veronika Challe(12) kuwa mke wake wa tatu.Imeripotiwa na Albanos Midelo.

15 comments:

Anonymous said...

Huyu baba atakuwa anapepo wa Ngono(samahani), au ni mwanga huyo. Maana sasa haieleweki Dunia hii inakwenda wapi jamani,sasa huyu tayari anawake wawili lakini bado anamkatizia masomo mtoto wa watu masikini, huu ni unyanyasaji wa kijinsia Haki za wanawake ziko wapi? tunaomba sana wahusika wafuatilie mambo haya kwasababu kila siku yanaongezeka. Sijui hana wazazi au ni halingumu ya maisha ya wazazi, jamani yaani maswali ni lundo kuliko majibu.

mumyhery said...

Jamani sina hata la kusema!!!

Simon Kitururu said...

Mmmh!

emu-three said...

Mhhh, haya ukistaajabu ya nanihii, utashngaa ya nanihino....ndio maisha !

Nampangala said...

Jamani huu ni ubakaji wa ali ya juu sana, nashangazwa sana na serikali yetu kwanini wanashindwa kumsaidia uyu mtoto. sijuwi nani wa kulaumiwa apa wazazi wa mtoto kwa dhiki yao kubwa walionayo au uchafu wa uyu mzee. mambo aya nilikuwa nayasikia kutoka nnchi za urabuni uko mbaaaaaali sana, inatisha sana kusikia sasahivi inatokea nyumbani kwenu. nimekasilishwa sana na hii habari ya uyu mtoto.

PASSION4FASHION.TZ said...

Eeeh mungu! nimeumia sana kusoma hii habari kisha nimegeuka kumuangalia binti yangu nae ana umri huo nguvu zimeniishia kwakweli,huyo sio mzima na wazazi wa huyo binti nao sio wazima pia.

chib said...

Yaani huyo SIJUI VISHILINGI au vijisenti potelea mbali kama jina lake nimelikosea, pambaf zake kabisaa, kwanza kumuachisha mtoto shule ni kosa, pili umri wa kumtamani na kumficha kinyumba ni kosa pia. Tatu, kujaribu kuficha uovu huo ni kosa tena, na tena..., hivi huko hakuna watu wenye hasira za cobra!!

Aunt Ndaga, UK said...

jamani dunia imekwisha!!!! hivi watu wa ustawi wa jamii bongo wanafanya nini? kila siku kuna kesi za watoto kuwa abused lakini hatusikii chochote kikifanyika, jamani tunaomba sasa watu wanaoshughulikia haki za watoto wafanye kazi tusije laumiana baadae, inasikitisha sana

Mtesuka said...

Tumevamiwa na mmomonyoko wa maadili na dhambi kubwa iliyo mbele yetu ni kuona kuwa "kila jambo kuwa ni la kawaida". Hatuta weza kuushinda uozo huu kwa kufikiri tunasheria au watu wengine wachukue hatua bali jamii nzima kushiriki kikamilifu kukomesha tabia hizi.

Rik Kilasi said...

Yaani hasira niliyopata pata hapa siwezi elezea ila wazazi wa huyo binti pamoja na huyo mzee wagonjwa wa akili.serikali iko wapi??? au huko serikali haipo?

sitaki kuamini kama wanapata shida kusuruhisha hili, huyo mzee kisheria anabaka huyo mtoto, pili achukuliwe hatua kwa kuoa mwanafunzi.hana utu huyo mzee na alaaniwe!

Flora Wanna said...

zalelo dada, tatizo hapa si mtoto ni wazazi waliokubali kumwozesha huyo babu, kwakweli wadau inatakiwa wamchukulie huyo mzee hatua kali, pamoja na wazazi wa mtoto huyo, kweli umaskini utaisha kwa mtindo huu? da! hadi mwili unanisisimka, mbaya sana.

Anonymous said...

Ndugu wapenzi wa blog hii imenisikitisha sana tena sana. Ila Nchi hii sijui inatupeleka wapi.Hapa jamani nchi hii imeshatuuza bila kujua. haya unapoona yanatokea siyo tu lawama kwa mtoto wala wazazi,tujiulize hivi huyu mtoto anapata mahitaji yake ya msingi? je? mzazi wake ana uwezo? hivyo wakulaumu ni serikali amabayo imesshindwa kuwawezesha hawa watanzania mpaka wanakataa tamaa ya maisha na kuamua kufanya mambo kinyume na sheria. Watu nao wenye uwezo msiwanyanyase hawa watoto kwani si kwamba umasikini wanapenda ila ni mfumo duni wa utawala yaani wachache ndo wafaidike tu na hii nchi bila kujali maslahi ya wengi. Naomba tuwe macho tushirikiane nchi hii ibadilike lasivyo yanakuja mbeleni mazito zaidi ya haya.

Goodluck

Sara Chitunda said...

Hii habari imenigusa sana mimi nikiwa msoma wa blog hii ya maisha na mafanikio najiuliza maswali mengi nashindwa kupata jibu. Ina maana wazazi wa huyo mtoto wameridhia kitendo hicho cha kumuoza binti yao au inakuaje? Halafu mtoto mwenyewe amekubali au kalazimishwa! uongozi wa shule yake unasemaje na umechukua hatua gani? kisha hao viongazi ambao wako nae watamsaidiaje kama wanashindwa kumchukulia sheria huyo mzee?

Penina Simon said...

Huu ni umasikini uliokithiri, mtoto anaozwa na wazazi wanajichukulia mali.
Kwa mtazamo wangu nahsi hata wale wake wawili wa huyo mzee muoaji ni masikini, Yasinta unajua umasikini ni utumwa mkubwa sana, huna maamuzi na kitu chochote sababu huna kitu, unavyopelekwa unakwenda tu.
Tunapaswa kujikwamua na huu ujinga tufanye kazi kwa bidii, ili kuondokana na watu wanaotumia hiyo fursa ya uonevu.

cytotec said...

obat cytotec i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat telat bulan