Tuesday, February 15, 2011

MAPAPAI :- UTAMU ,FAIDA NA MATUMIZI YAKE!!

Hapa ni mti wa papai, leo nimekumbuka faida mbili za majani ya mipapai moja ni dawa ya tumbo hasa kama una tatizo la choo kubwa . Unachukua hayo majanai na unachemsha na halafu unakunywa yale maji yake. Pili ni sabuni unaweza au niseme mimi nimewahi kufulia nguo ila usifulie nguo nyeupe basi itakuwa kijana. Nguo nyingine zote sawa kabisa.
Na hapa ni tunda lenyewe nalo lina faida zake kwanza ni kwa ajili ya kula ni tamu sana na pia nalo kama una tatizo la choo kubwa ni nzuri. Halafu jambo jinginge papai ni kilainisho kizuri sana cha chama hasa nyama ya ngómbe. Toa hizo mbege weka kwenye chombo, pondaponda papai na uchanganya na hizo mbegu koroga taratibu katakata nyama vipande vidogovodogo weka humu kwenye mpondo na subiri masaa kadhaa. Hakika utaifaidi nyama yako mno itakuwa lainiiii. Ila kusema kweli nimetamani kweli papai ni muda sasa sijala:-)

18 comments:

Albert Kissima said...

Nashukuru dada Yasinta kwa elimu yako nzuri. Dah! Nami sijayala matunda haya kwa muda mrefu kweli kweli. Nilizoea kuyala kule K'njaro kwani yalipatikana kwa urahisi saaana. Ilikuwa ni kuingia tu shambani na kujichumia, huku nilipo, hata la kuuzwa sijaliona.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Albert hapo ndo umezidi kunitamanisha ulivyosema kuingia tu shambani na kujichumia. Yaani we acha tu hiyo ndio kazi niliyokuwa naifanya halafu mpaka unachagua na lililo baya linakuwa chakula cha nguruwe....sasa hata hilo baya halipatikane kaaaazi kwelikweli.

Simon Kitururu said...

MAJANI YA MPAPAI ni kitu nilichowahi kuvuta utotoni katika michezo ya kuiga wakubwa wavutavyo SIGARA.:-(

Ila mpaka LEO sina uhakika ilikuwa ni majani ya mpapai au kipande cha gazeti la uhuru nilichosokotea majani ya mpapai wakati namiaka nane ndicho kiliathiri zaidi mapafu yangu!:-(


Tukiachana na hilo,...
... huku nilipo MAPAPAI yapatikanayo sio matamu kihivyo na PAPAI bomba nilikumbukalo liko BONGO na huku ni fulu vipapai vya kubahatisha!:-(

Mija Shija Sayi said...

Mwenzenu silagi mapapai, nimezaliwa hivyo. Nayatamanigi kweli lakini nikijaribu hata kipande kidogo utanihurumia kwa chafya na mwili kusisimuka na kukosa nguvu.

Unknown said...

pole Da Mija kwani unakosa uhondo!! Nashangaa sana kwani mapapai ya ughaibuni si matamu kama yale ya nyumbani!!

Anonymous said...

Ni kweli kabisa Dada, na mti huu husidia choo nafikiri ni kwasababu umeshasema kuwa kuna sabuni ndani yake, na huwa mahospitalini wanatumia sana sabuni kuwasaidia wagonjwa kusafisha choo yote tumboni, hasa wale wanaoandaliwa kwa upasuaji, na hii hufanyika sana hapa nchini kwetu. Asante kwa elimu hii nzuri.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Simon! katika watu watundu hapa ni kikomo mpaka kujaribu kuvuta majani ya mipapai aise kaazi kwelikweli.

Mija Pole sana kwa kukosa utamu wa papai. Lakini nadhani haupo pekee. binafsi nilikuwa sili tufaa na ukizingatia ndia matunda ambayo yapo mengiiii sana hapa. Namshukuru mwenyezi mungu kuwa sidhuliki nikila ndizi hapo ingekuwa kasheshe.

Kaka Mrope! Ni kweli kabisa hayana radha kabisa na pia ni vidogovidogo na sikilizia BEI yake sasa mbona utakimbia.

Sijui ni kaka au dada ambaye huna jina. Ahsante kwa kuipenda elimu hii. Na karibu tena na tena.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hapa hapo yanatoka nchi za Latin Amerika. Tatizo ni bei. Paundi moja dola 2.99. Kwa hivyo papai la wastani ni lazima uteme dola 10 na wakati mwingine unakuta wala siyo "organic" kama ulivyoahidiwa. Basi mtu unakula lakini ladha yenyewe mmmmm! Baadaye unagundua kwamba papai hilo limechakachuliwa kisayansi ili likue haraka, litoe matunda mengi...Shida tupu unaambiwa

Rachel Siwa said...

Jamani tupo wengi hata mimi papai linanishinda kabisa,nimejaribu siwezi kumeza silipendi,
Asante da Yasinta kwa kutuelimisha,nitajitahidi nile papai niache SUKARI DADA!

@kaka MATONDO LIMECHAKACHULIWA HAHAHA!Hata baba watoto na watoto wanapenda sana papai lakini ya ughaibuni yanawashinda!

ooh narudi nyumbani eeeeeee!

Rachel Siwa said...

Nimesahau kumpa pole kaka Kitururu!pole kaka,lakini naumgana na da Yasinta wewe ulikuwa kiboko!

Anonymous said...

Mpendwa Yasinta,
asante kwa elimu pacha inayoambatana na utamu wa tunda hili ambalo ni my favourite.

Miaka minane nyuma kabla sijaanza kujichakachua na matunda 'ready-made' i.e yasiyohitaji hassle za umenyaji kama apples na mengine, papai lilikuwa ni my favourite.
Ingawa hadi leo kusema kweli.

Pia kwa upande mwingine, hongera kwa kazi njema unayoifanya hapa. Kwa kweli huwa nabarikiwa sana na blog yako na siwezi pitisha siku bila kupita hapa though ni leo tu nimevutwa kuacha comment hapa.

Shukrani pia kwa watoamaoni-wakazi ( ha ha ha resident commentors) kama Mrope, Mija, kakangu Matondo, Prof. Mbele, Chautundu Kitururu, Kamala na wengineo ambao nao pia huwa nawatembelea huko kwao.
Mnaonesha kuwa blogging ni zaidi ya kedi, matusi na ushauzi.

Keep up the good work.
Ni mie,
Msukuma mwenye Swagga

Penina Simon said...

Ahsante sana best, halafu faida nyingine, Hizo mbegu zake ni dawa nzuri sana ya minyoo ya aina zote. Pia papai hivyo lilivyo ni kilainisho cha ngozi, chukua papai lililoiva, lisage na kijiko, osha uso wako then paka baada ya dk15,20 osha uso wako, utafeel ulaini kama mtoto mchanga na wala hutahitaji cream tena.

chib said...

Mpapai ni sabuni!!

Anonymous said...

Mpapai unasaidia kutoa magaga miguuni kule vijijini tulikuwa tunasugua miguu kwenye jiwe tukichanganya na majani ya mpapai,miguu ilikuwa bomba.Hee kijijini raha sana jamani, Dada umetukumbusha mbali sana wewe. Mimi nipo hapa nje ya Tz,ukienda sokoni tuite unakuta vipapai vya ajabu ajabu na viembe,halafu hiyo bei yake ni kama sh.elfu saba hadi kumi za nyumbani,hamu inaisha kabisa. ukizingatia nyumbani ni chakula cha ndege loh.

EDNA said...

Yam yam ni moja ya matunda ambayo nayapenda sana.

John Mwaipopo said...

penina dawa ya minyoo inatayarishwaje?

Unknown said...

Helloo... Naona comments hizi ni za muda kidogo! Bahati mbaya nimechelewa kuziona, lakini nishaanza kilimo tayari. Nina kama heka mbili ama tatu hivi. Napatikana kwa moddyguyz@yahoo.com au 0787519910.

Natanguliza shukurani kwa kazi yenu nzuri...

Unknown said...

Helloo... Naona comments hizi ni za muda kidogo! Bahati mbaya nimechelewa kuziona, lakini nishaanza kilimo tayari. Nina kama heka mbili ama tatu hivi. Napatikana kwa moddyguyz@yahoo.com au 0787519910.

Natanguliza shukurani kwa kazi yenu nzuri...