Wednesday, February 23, 2011

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO YATIMIZA MIAKA MITATU LEO!!!

Hapa ni Mwenyewe Mama
Maisha na Mafanikio!!!
Ni kama vile mtoto azaliwapo na kukua katika hatua tofauti tofauti, na mara nyingi hatua hizo huenda sambamba na mabadiliko ya kimwili na kiakili.
Leo hii Blog hii ya Maisha na Mafanikio yatimiza miaka mitatu kamili huku nikijivunia mafanikio niliyoyafikia tangu nilipoianzisha blog hii. Kama nilivyosema hapo awali kuwa mtoto anapozaliwa hukua katika hatua tofauti tofauti na hivyo ndivyo ilivyo kwa blog hii ya Maisha na Mafanikio. Kwani nilianza kama masihara kuandika habari mbalimbali za kijamii, za kufurahisha, za kuhuzunisha na za kuburudisha pia, na kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kujifunza mambo mengi sana. Kwa sababu hii napenda kuchukua nafasi hii na kusema AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU KWANI NAAMINI BILA NINYI, NISINGEFIKA HAPA LEO. KWA KWELI NAAMINI KUWA SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA.UPENDO NA UMOJA WETU UDUMU DAIMA NA PIA MILELE!!!!!

31 comments:

Unknown said...

HONGERA SANA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO.Miaka mitatu si mchezo jamani,wengine ndo kwanza tuko mwanzoni.Imekua ikinielimisha,ikinifurahisha na mambo mengi tu mazuri.Ni moja ya blog zilizonifanya nianze kublogua.All the best na idumu daima.

Christian Sikapundwa said...

DADA YASINTA HONGERA SANA,kuiendesaha Blogu kwa miaka mitatu ( 3 ) si kitu cha mchezo.nakutakia mafanikio mema kwa tuipeperusha Bendera ya Tanzania katika Mtandao wako.

Ni jimbo la kujivunia na Wa -Tanzania woha wanaBlog wa nje na wandani tunapupongeza.Lakini na wana - Lizombe wanakupa Hai ya hali ya juu mmno,Kengerai.Ubarikiwe sana endelea kukaza kamba katika Blog hii.

Chilau mewawa.

Christian Sikapundwa said...

DADA YASINTA HONGERA SANA,kuiendesaha Blogu kwa miaka mitatu ( 3 ) si kitu cha mchezo.nakutakia mafanikio mema kwa tuipeperusha Bendera ya Tanzania katika Mtandao wako.

Ni jimbo la kujivunia na Wa -Tanzania woha wanaBlog wa nje na wandani tunapupongeza.Lakini na wana - Lizombe wanakupa Hai ya hali ya juu mmno,Kengerai.Ubarikiwe sana endelea kukaza kamba katika Blog hii.

Chilau mewawa.

Simon Kitururu said...

Hongera!

Anonymous said...

Hilo pozi mi hoi...

MissPosh said...

Hongera sana

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Hongera sana Da Yasinta!

emu-three said...

HONGERA MAISHA NA MAFANIKIO! Kama jina lilivyo, natumai wengi wamefanikiwa sana kwa kupitia blog yako dada Yasinta, umeweza kuwasaidia watu wengi kimawazo, na kila-namna katika maisha yao kwa minajili ya kupata mafanikio!
Kublog ni hobby, lakini pia inahitaji muda, tafakari na hata wakati mwingine nyezo, na yote haya yanahitaji moyo. Hongera sana!
Katika kazi kama hii, utapendwa na wengi, na pia ukubali kuchukiwa, YOTE NI SAWA, KWANI NI SEHEMU YA MAISHA, NA YOTE NDIYO BAADAYE YANAKUJA KULETA MAFANIKIO...
Ni hayo tu dada yangu mpendwa, YASINTA: Happy birthday MAISHA NA MAFANIKIO!

Baraka Chibiriti said...

Hongera sana Dada Yasinta, kwa miaka 3, pia kwa kazi nzuri ya Blog yako.
Chibi.

Kibunango said...

Hongera sana...!

John Mwaipopo said...

'ongela' mwanakwetu kijiwe hiki ni maskani ya wengi. ni kusanyiko la tunaopotea-ga. 'lisongeshe' bibie

EDNA said...

Hongera sana mdada kwa kutimiza miaka mitatu ya kublog na hongera kwa kazi nzuri.

PASSION4FASHION.TZ said...

HONGERA SANA YASINTA.

Rachel Siwa said...

Hongera sana dada Yasinta!Blog ya Maisha izidi kusonga mbele!!!!!!!!!

Nova said...

Hongera sana kwa kazi kubwa unayofanya ya kutuelimisha na kutuhabarisha ndugu zako.

Maisha na mafanikio imekuwa ni faraja yangu, kutokana na kuandika mambo yanayofurahisha na kuelimisha kwa kiasi kikubwa kwa kutumia mazingira na lugha ya kawaida kabisa.

Asante sana Dada Yasinta, Mungu akubariki na kukuimarisha uendelee kutuelimisha nduguzo.

Pd. Nova Ngonyani, OSB

Mija Shija Sayi said...

Yasinta halafu ukianguka na hilo pozi utamlaumu nani??

Hongera sana kwa kutimiza miaka 3 ulingoni. Mungu azidi kukuongoza na kukubariki ili nasi tuzidi kufaidika na kibaraza hiki.

Hongera kwa siku ya kuzaliwa Blogu yetu.

Mbele said...

Umetoka mbali. Hongera sana na kila la heri.

Faith S Hilary said...

Jamani siku zinakwenda kuliko upepo!!! Juzi juzi tu nilishuhudia kuwa mwaka mmoja, mpaka miwili, sasa mitatu...angekuwa mtoto sasa anaenda nursery school! Hahaha...hongera sana dada kwa hilo, kuendesha blog kwa miaka na miaka na bado iko safi si kitu rahisi, tupo pamoja! Much love sis! x

Mwanasosholojia said...

Hongera sana da Yasinta na MAISHA NA MAFANIKIO yetu!

Unknown said...

Wanadamu Tuna Asili ya Uoga Baada ya Dhambi. Maandalizi ktk Maisha ni ya Muhimu Sana. Umoja Ktk Familia unaleta Mafanikio Makubwa Mno. "AHADI ZA BWANA HUWA TUNATEMBEA NAZO LAKINI HATUJITAMBUI".

Bubu hupata kusema, mambo yanapomzidi. Na kiwete husimama, akakimbia baidi. Hata kuku huchachama, unapomtia kedi. Na jorowe takuuma, iwapo hapana budi. Nyundo ni nyundo kwa chuma, japo kisiwe baridi. MUNGU WETU JE?

Katika Dunia Hii Hakuna Mtu wa Ziada Atakayeweza Kufikiria Kwa Niaba Yetu Dadaaa.

H O N G E R A RAFIKI.

Baraka Mfunguo said...

HONGERA SANA BLOGU YA MAISHA NA MAFANIKIO

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hongera da Yasinta!

Nikipata nauli nitakuja kula keki ya hepibesdei!...lol!

Anonymous said...

Nilikuwa Mbali sanaaaa,anyway hongera saniiiii.
kaka s

mumyhery said...

Hongera sana Mama
Erick

Albert Kissima said...

Hongera sana Dada Yasinta. Uzidi kuwa na moyo huo wa kutenga muda wako kwa ajili ya kuifunza na kuiburudisha jamii

Blackmannen said...

Hongera sana 'Mtani' wangu Yasinta kwa kazi ngumu kama hiyo kwa kuifikisha miaka mitatu na ikiwa inaendelea kuishi na kuneneepa kwa kupata watembeleaji lukuki.

Wa-Bongo wengi wamekuwa wakianzisha blogi zao, na mwisho wake wamekuwa wakiishiwa cha kusema. Badala yake wakaanza kuweka picha za watu mashuhuri katika blogi zao ama kurukia kuandika mambo ya "Siasa" ili kuvutia wasomaji.

Lakini wewe "Yasinta", hujafilisika kiasi hicho. Kila siku tunapata tunavyovihitaji kuvipata kutoka kwenye "Maisha Na Mafanikio".

Wenye blogi zao wengi wao wanapata watembeleaji kupitia blogi ya "Maisha na Mafanikio". Hilo halina ubishi.

Hongera sana dada Yasinta endelea kama ulivyo hadi uwafikie akina "Ankal".

It's Great To Be Black=Blackmannen

Goodman Manyanya Phiri said...

Na amini hiyo miaka mitatu ilikuwa ya jasho nyingi kukutoka. Mimi nakuombea afya nzuri zaidi kwa minyaka mitatu ijao tena ili msukumo au ile MOMENTUM uliyenzisha kwenye blogi yako maarufu ukae pale pale ulipo au uongeze mwendo zaidi. Ni Mungu tu! Ubarikiwe daima, Mkuu!

Koero Mkundi said...

Namini sijachelewa.....
Nami nasema Hongera dana dada Yasinta kwa kuumiza kichwa kwa miaka mitatu ili kuwahabarisha wasomaji wa kibaraza hiki cha Maisha na Mafanikio.

SWALI: Je ukifanya tathmini ya hiyo miaka mitatu ya kublog, Je umepata mafanikio gani ya kujivunia?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

eti sisi sote ni watoto wa baba mmoja, kwanini sio mama????

Yasinta Ngonyani said...

Woteeee nawashukuruni sana kwa maoni mazuri nimeyasoma na nilichofanya ni kutokwa na machozi yaani machozi ya furaha. kublog ni kama hobby lakini pia ni kazi ambayo inahitaji muda nami nimejaribu kupata huo muda yaani pake nipatapo muda basi narusha mawili matatu. Na ninachojivunia zaidi katika blog hii ya Maisha na Mafanikio ni kwamba nimejuana na watu wengi sana ambao sikutegemea kama nitajuana nao. Hili ni moja na pia huwa nafurahi pale wasomaji wanapofurahia niandikacho. KWA MARA NYINGINE TENA AHSANTENI SANA.UPENDO DAIMA. mnaweza kuendelea kutoa maoni!!!

Salehe Msanda said...

Hongera na kila la kheri
kwa kuiwezesha blog kutimiza miaka 3.